DOKEZO Wanafunzi Shule ya Msingi Bunge (Kivukoni – Dar) ambao hawajalipa michango wanazuiwa kuingia darasani

DOKEZO Wanafunzi Shule ya Msingi Bunge (Kivukoni – Dar) ambao hawajalipa michango wanazuiwa kuingia darasani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna jambo ambalo linaendelea hapa kwenye Shule ya Msingi Bunge iliyopo Kata ya Kivukoni, Mtaa wa Shaaban Robert, ndani ya Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam, Wanafunzi zaidi ya 30 wa Darasa nne ambao inadaiwa hawajakamilisha malipo ya michango mbalimbali wamezuiwa kuingia darasani kusoma tangu Jumatatu 17 August. 2026.

Sababu kubwa ni kuwa kiongozi wa shule ametoa maagizo kwa Walimu wa madarasa kuwapeleka Wanafunzi hao katika uwanja wa michezo wa shule, ambapo hukaa hapo hadi jioni bila kusoma.

Najiuliza Wanafunzi hao watafaulu vipi mtihani wa Taifa endapo wananyimwa haki yao ya kusoma!

Je, ni sawa kiongozi huyo kutoa agizo la kuwazuia wanafunzi kuingia darasani kwa sababu ya kutolipwa kwa michango hiyo?

WhatsApp Image 2026-08-19 at 12.56.45.jpeg
WhatsApp Image 2026-08-19 at 12.56.45o.jpeg
WhatsApp Image 2026-08-19 at 12.56.46oo.jpeg
WhatsApp Image 2026-08-19 at 12.56.46.jpeg
 
Kuna jambo ambalo linaendelea hapa kwenye Shule ya Msingi Bunge iliyopo Kata ya Kivukoni, Mtaa wa Shaaban Robert, ndani ya Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam, Wanafunzi zaidi ya 30 wa Darasa nne ambao inadaiwa hawajakamilisha malipo ya michambo mbalimbali wamezuiwa kuingia darasani kusoma tangu Jumatatu 17 August. 2026.
Sababu kubwa ni kuwa kiongozi wa shule ametoa maagizo kwa Walimu wa madarasa kuwapeleka Wanafunzi hao katika uwanja wa michezo wa shule, ambapo hukaa hapo hadi jioni bila kusoma.

Najiuliza Wanafunzi hao watafaulu vipi mtihani wa Taifa endapo wananyimwa haki yao ya kusoma!

Je, ni sawa kiongozi huyo kutoa agizo la kuwazuia wanafunzi kuingia darasa kwa sababu ya kutolipwa kwa michango hiyo?
Elimu bure, bure hewa
 
Hapa ndipo unapogundua walimu ni zero brain.

Sasa michango inahusiana vipi na mtoto kutoingia darasani kupata haki ya elimu?

Kwanini usiwaandikie barua wazazi kuwahimiza walipe michango hiyo huku watoto wakiendelea na masomo?

Hapo akitokea mkuu wa wilaya ama mkoa akamsimamisha kazi kupitia kwa mkurugenzi walimu wataanza kulalamika kwba wanaonewa wakati wao hawajitambui hata kwa mambo madogo kama haya.
 
Hakunaga elimu bure, wazazi muwajibike Kwa gharama za watoto wenu.
 
Wazazi tukubali kwamba ukizaa mtoto jua utawajibika. Serikali inasema elimu bure, wazazi tunataka ufaulu ila mazingira ya shule za serikali hata walimu wanatia juhudi binafsi wakati mwingine wanahitaji posho.
 
Kafulila kasema tuzingatie uzazi wa mpango.

Anyway hii nchi mambo yanajiendea tu.
 
Kuna jambo ambalo linaendelea hapa kwenye Shule ya Msingi Bunge iliyopo Kata ya Kivukoni, Mtaa wa Shaaban Robert, ndani ya Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam, Wanafunzi zaidi ya 30 wa Darasa nne ambao inadaiwa hawajakamilisha malipo ya michango mbalimbali wamezuiwa kuingia darasani kusoma tangu Jumatatu 17 August. 2026.

Sababu kubwa ni kuwa kiongozi wa shule ametoa maagizo kwa Walimu wa madarasa kuwapeleka Wanafunzi hao katika uwanja wa michezo wa shule, ambapo hukaa hapo hadi jioni bila kusoma.

Najiuliza Wanafunzi hao watafaulu vipi mtihani wa Taifa endapo wananyimwa haki yao ya kusoma!

Je, ni sawa kiongozi huyo kutoa agizo la kuwazuia wanafunzi kuingia darasani kwa sababu ya kutolipwa kwa michango hiyo?


Hawajalipa michango, sawa, lakini je kuwanyima watoto haki yao ya elimu (kuwatoa darasani) ndiyo suluhisho sahihi?

Je hiyo hela itapatikana kwa kumtoa mtoto darasani na kumkosesha vipindi?

Kama watalipa baadae, hivyo vipindi walivyokosa kwa kuondolewa darasani kwa hizo siku watafundishwa au kufidiwa?

Busara na hekima inahitajika sana katika kuyaendea haya mambo.
 
Back
Top Bottom