Tetesi: Wanafunzi shule ya Sekondari Kyimo waambiwa kuchangia pesa za chakula, madawati na mwalimu wa kujitolea

Tetesi: Wanafunzi shule ya Sekondari Kyimo waambiwa kuchangia pesa za chakula, madawati na mwalimu wa kujitolea

Joined
Jan 19, 2018
Posts
7
Reaction score
5
Diwani wa kata ya Kyimo na mkuu wa shule ya Sekondari Kyimo wamefanya mkutano leo tarehe 23/01/2018 na wazazi wenye wanafunzi hapo shuleni wakilazimisha kuchangia TZS. 70,000/= kwa ajili ya chakula wakati wa muda wa masomo.

Pia wametaka michango TZS 10,000/= kwa kila mwanafunzi kama malipo ya mwalimu wa kujitolea, pia michango ya madawati imewekwa kiporo ila imependekezwa kila mwanafunzi kuchangia TZS 25,000/=.
 
Ndio kote staili hii inavyoendelea sehemu nyingi, nadhani ni kwa kua mpiga marufuku hakuiainisha ni michango ya aina gani!
 
Diwani wa kata ya Kyimo na mkuu wa shule ya Sekondari Kyimo wamefanya mkutano leo tarehe 23/01/2018 na wazazi wenye wanafunzi hapo shuleni wakilazimisha kuchangia TZS. 70,000/= kwa ajili ya chakula wakati wa muda wa masomo.
Kosa liko wapi hapo sasa? Kwani serikali inatoa fungu la chakula? Huyo Mh. Diwani ni wa kuigwa kabisa, anajitambua sana. Elimu, elimu, elimu.
 
Kosa liko wapi hapo sasa? Kwani serikali inatoa fungu la chakula? Huyo Mh. Diwani ni wa kuigwa kabisa, anajitambua sana. Elimu, elimu, elimu.
Kweli serikali haitoi fungu lakn isiw lazm kuchnga kwan wngine watabeba makande kutok nyumban .
 
Diwani wa kata ya Kyimo na mkuu wa shule ya Sekondari Kyimo wamefanya mkutano leo tarehe 23/01/2018 na wazazi wenye wanafunzi hapo shuleni wakilazimisha kuchangia TZS. 70,000/= kwa ajili ya chakula wakati wa muda wa masomo.
Maskini! Tayari diwani keshamponza mkuu wa shule!
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Wazazi eleweni serikali haina pesa ajiri ya chakula cha watoto wenu sema hapo kuna harufu ya wizi elfu 70 y'all chakula cha miaka mingapi minne au hapo kuna upigaji
 
Chakula ni kwa ajili ya watoto wao wenyewe, serikali haitoi pesa wala haina shamba kulisha wanafunzi, waacheni wazazi wajiletee maendeleo yao wenyewe!

Unasema Elimu Bure halafu wewe mtoto wako umempeleka Feza au Marian!

Kwanini watoto wale chakula shuleni?

Kuna baadhi ya maeneo watoto inabidi watembee umbali mrefu ili kuifikia shule, wakati huo huo hana uhakika wa kula mchana mahali popote.

Wazazi kuchangia chakula ni wajibu wao.
 
20180123_201655-BlendCollage.jpg
 
Binafsi nashangaa mzazi anapolalamika michango km hyo,,, hamisha mwanao peleka shule ambayo haina michango ambayo Mh Rais talipa kwaajili yako

Elimu Tanzania ndo inakufa hivyo kaeni mkilalamika lalamika vitu ambavyo ni manufaa ya mwanao
 
Back
Top Bottom