Tetesi: Wanafunzi shule ya Sekondari Kyimo waambiwa kuchangia pesa za chakula, madawati na mwalimu wa kujitolea

Tetesi: Wanafunzi shule ya Sekondari Kyimo waambiwa kuchangia pesa za chakula, madawati na mwalimu wa kujitolea

Nawapongeza sana huyo Diwani na Mkuu wa Shule.

Hili suala la burebure lipo kisiasa sana...

Mtoto anatembea km kadhaa to and fro daily....ashinde njaa!??

Wanafunzi hawajawahi mouona Mwl wa sayansi.....wakae tu wasubiri necta.!??

Tuache mikurupuko ya wanasiasa.
 
Kwan kula shuleni ni lazma hizo ni dhana za kupiga Cha juu mm nimesoma mwanzo mwisho tulikuwa tunakula home but now chakula ndo best important na ambae Ana mtoto asisome hapana
 
Hivi wazazi wakiamua watoto wao wale chips na kuku mchana halafu wakakubaliana kuchangia hizo chips 5000 kwa siku. Halafu watoto wao wote wakafaulu with flying colours. Kuna uvunjifu wa amani hapo ?
Na ndio tunavyolipia private schools
 
RAIS KASEMA, MICHANGO ILE AMBAYO WAZAZ WATASHRIKISHWA NA WATAKUWA TAYARI NI RUKSA, ILA ADA MARUFUKU NA MICHANGO MINGNE ISYO NA ULAZMA. MIMI NAFIKIRI WAANDISH WA HABARI WATANGAZE HABARI KWA KINA NA KUWAELIMISHA WANANCH BADALA YA KUISHIA KUANDKA HABARI KIUDAKU NA KUWACHANGANYA WATU KAMA MTOA MADA.
 
Hiyo Shule wanao utaratibu mzuri Wa chakula cha wanafunzi tokea muda mrefu .na matokeo yao ni mazuri kila mwaka nadhani kama utaharibiwa huo utaratibu hasara nikwa watoto na familia zao.kikubwa utaratibu tu uwekwe vizuri na kuwe na muhtasari Wa vikao vya maafikiano na wazazi.
 
Tokea enzi ya mama Dunda wanakula chakula na ni Shule pekee iliyokua na huo utaratibu tokea zamani wilaya nzima.wasimamizi Wa huo mpango Wa chakula watiwe moyo na sio kuwavunja moyo.
 
kwa staili hii wazazi pia tumepigwa marufuku kuchangia miundo mbinu ya shule kama ujenzi wa madarasa n.k.hivi wanajua kuna shule ina walimu wa 4 tu hapa nchini?watoto wanashinda njaa hadi saa 8 ndo waende nyumbani km kadhaa kwa hili mkulu sikubaliani nae
 
mie nilisema waweke percentage labda 3% ya kipato cha mzazi,kila mtu alipe kile ambacho anaweza kutoa,kusema wote walipe 70,000 ni kuwaonea,unajuaje hicho ndicho anachopata kwenye shughuli zake?
 
solution ni wakae sakafuni ,washinde njaa, wajifundishe wenyewe !
 
Kyimo ni wa kuigwa na wapenda maendeleo ya elimu wote! Majuzi kuna shule za kata zilijenga hostel kwa watoto wa kike ili iwasaidie katika kuwalinda na jamii dharimu lakini tamko la mkuu likawakumba na hizo hostel zikafungwa huku watoto wa kike wakilazimika kutafuta vyumba vya kupanga mtaani. Iliniumiza sana kichwa lakini baadhi wa watendaji wakijiongeza kihivi na baadhi ya wazazi kupitia kamati ya shule wakasimamia hili sheria itawalinda.
 
Mtoa mada umenichefua sana, umekurupuka au umeamua kuficha ukweli ili upate sapoti, watu wana akili zao humu na mbaya zaid inaonesha hata wanakijiji wenzako hapo wamekuzid akili, umefcha kusema shule inawanafunz wangap? 70k kwa mda gani? Mwl mmoja wa kujitolea analipwa sh ngap? Walimu wa kujitolea wapo wangap? Shule inaupungufu wa madawat kwa kiwango gan? 10000 kwa mda gani?, majibu yote unayo na unajua ni halali ndo mana huweki hapa hicho ulichoficha, endelea kupigania wanao kushnda njaa na aishie kusoma kiswahili na history a.k.a fuvu mpaka amalize halaf baadae ulete sharubu zako zenye mvi humu kuomb ushauri wa je mwanao areseat(PC) au arudie 4m2? Au hata nafas akose upishane nae mlango wa chooni na kiduku mpk cha ndevu, Huku mwenzako yupo awamu ya pili ya uongozi wake akifurahia kauli yake ilifanikiwa na mwanae aliyesomea feza yupo nje, shda zote zitakazo mwandama mwanao na uzao wake zitakufuata wewe popote. BTW shkamoo hii ni Jf.
 
Kikao kimefanyika leo 23/1/2018 na kaazimia sh.10,000 mwl wa kujitolea shule nzima?? Na ,70,000 chakula na hili la kipolo 25000 dawat??? Jamani mkuu wa shule umeponzwa kwenye siasa tena kwani hujasikia agizo la RAIS????
Hakuna tatizo hapo! Tatizo wazazi/walezi wengi ni vichwa maji, wanapenda mteremko. Hawaelewi waraka namba 2.
Diwani anapaswa kuitisha WDC, kupitia muhutahsari na kupeleka wilayani ili kupatiwa kibali.
3. Je wasipolazimisha nani atachangia? Huwajui Wabongo
 
Wakuu wa shule wengi wanahitaji elimu,jukumu la michango waziachie serikali za mitaa na kata baada ya kutoa taarifa ya mapungufu yaliyopo shuleni kwenye kamati.

Lakini kwa vile waalimu wetu tz walishageuka tra acha yapukutishwe.
Ni rahisi kuropoka kwa kuwa haupo field!!! Usamehewe bure. Ahsante kwa kuonyesha ulivyo mweupe kichwani.
Ikiwa kama wewe ni Mkuu wa shule, wanaripoti F.I 300 wasio na mahali pa kukaa utaendelea kuwaambia tu waalimu waendelee kufundisha?
Tuna safari ndefu sana.
 
Wazazi eleweni serikali haina pesa ajiri ya chakula cha watoto wenu sema hapo kuna harufu ya wizi elfu 70 y'all chakula cha miaka mingapi minne au hapo kuna upigaji
Wewe naye wa ajabu yaani 70,000 ya chakula kwa mwaka mzima unasema kuna upigaji?!!!mbona shule nyingi za kata ambazo zipo vijijini wazazi wanachangia gunia moja la mahindi tu mwaka mzima?
 
Back
Top Bottom