KERO Wanafunzi UDOM wanaobaki wakati wa likizo wanalazimishwa kulipia tena hostel?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wanafunzi wa UDOM college ya Education, wakati chuo kinafungwa kwa wiki moja tu, wanafunzi wanaobaki wanaambiwa kulipia tshs 5,200 ya hosteli ilihali malipo ya hosteli yamefanyika kwa mwaka.

Swali la kujiuliza tutalipia mara ngapi kwa mwaka? Sisi hatuelewi kabisa
 
Wapo sahihi. Km unahitaji msaada, omba usaidiwe
 
Vijana mbona mnapenda kukichafua chuo bila sababu za msingi??msomi gani unakurupuka ?? Au ni first year wewe.

Chumba unachokaa kwa siku ni 750 tsh hiyo pesa zidisha na muda utakaa kaa kipind chote cha masomo ndio inakuja hiyo pesa ya hostel bila kuwepo mambo ya likizo ......umekosa nauli ya kurud kwenu kotokana na umasikin wenu na umasikini wako wa akili chuo kimekuhurumia sehemu ya kulala ambayo ni ( 750× likizo siku7 ) wastani wa 5200 kwa punguzo la tsh 50 bado nyokonyokonyoko. UDOM.
 
Malipo ya hostel hufanyika kulingana na idadi ya siku za masomo hivyo hizi siku za likizo hazikulipiwa ni sahihi kabisa kulipia hiyo huduma
Ndio wasomi wetu hawa kwani unadhani bylaw haijaleza haya mambo.
 
Chuo cha UDOM kimejengwa kwa pesa ya wastaafu na zinabidi zirudi. Ela unayolipa inapigiwa hesabu ya siku utakazotumia hicho chumba hivyo kama huendi likizo lazima wakuchaji.
 
Hiyo pesa unayotakiwa kulipa ni kwa ajili ya kuwalipa wafanya usafi wa chuo. Ni utaratibu wao wa Kila mwaka Wala si kero. Acha kuchafua chuo kwa sababu zako za kuwa na uwezo mdogo wa kufikili. Hata kabla hujapost, uliza hata kwa uongozi wa serikali ya wanachuo ili upatiwe ufafanuzi bayana.
 
Wee Dogo kama ulikua hutaki kusoma CHUO CHA KATA usingejiunga😅😅
 
Lakini naona ni sawa, gharama za kuendesha hizo hostel ni kubwa. Kama huna hiyo pesa nenda tu nyumbani
Kipindi chetu ilikua 500 kwa siku, sijui kama wamepandisha sasa hivi, hio hela mwanafunzi unachangia tu, ila value unayopata ni kubwa kushinda hio.

Imagine unapewa kitanda, Godoro, Kabati, Choo, Maji taka, Sehemu za kufulia etc kwa 500 tu kwa siku.
 
Kipindi chetu ilikua 500 kwa siku, sijui kama wamepandisha sasa hivi, hio hela mwanafunzi unachangia tu, ila value unayopata ni kubwa kushinda hio.

Imagine unapewa kitanda, Godoro, Kabati, Choo, Maji taka, Sehemu za kufulia etc kwa 500 tu kwa siku.
Umeme,ulinzi
 
5200 kwa wiki nzima unakuja kuiandikia siredi...
Halafu unahonga changu 5000 kimoja kwa dakika 10
 
Watu kama wewe hamkupaswa kufika chuo kikuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…