KERO Wanafunzi UDOM wanaobaki wakati wa likizo wanalazimishwa kulipia tena hostel?

KERO Wanafunzi UDOM wanaobaki wakati wa likizo wanalazimishwa kulipia tena hostel?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Vijana mbona mnapenda kukichafua chuo bila sababu za msingi??msomi gani unakurupuka ?? Au ni first year wewe.

Chumba unachokaa kwa siku ni 750 tsh hiyo pesa zidisha na muda utakaa kaa kipind chote cha masomo ndio inakuja hiyo pesa ya hostel bila kuwepo mambo ya likizo ......umekosa nauli ya kurud kwenu kotokana na umasikin wenu na umasikini wako wa akili chuo kimekuhurumia sehemu ya kulala ambayo ni ( 750× likizo siku7 ) wastani wa 5200 kwa punguzo la tsh 50 bado nyokonyokonyoko. UDOM.
Wengi mnaweza kucomment kulingana na hosteli mlizowahi kuishi ama uzoefu, binafsi nadhani cha msingi hapa nikuangalia mkataba unasemaje? MIMI nimekutana na scenerio kama hiyo kwa kijana ambaye namsponsor na anasoma kwenye chuo cha MNRT Arusha. Joining instructions inasema hostel ni shilingi elfu 50 kwa mwezi. Huyu binti aliiingia chuoni kwa second selection kutokana na makosa ya kuomba kujiunga na chuo, ambapo kwa kuwa anatarajia kusoma miaka miwili aliomba kupitia online na kumbe hii online ni kwa ajili ya form six hivo mfumo ukamtema.

Hivo ailibidi aombe tena upya kwa kujaza form nakuipeleka chuoni kwa mkono,nakuchaguliwa ktk second selection ambapo aliripoti chuoni mwezi 11 na hostel ikalipwa shilingi laki 2 ambayo ni kuanzia mwezi 11 mpaka mwezi wa pili. tarehe 10/02/2025 chuo kikafungwa na kwa kuwa wao waliingia chuoni kwa kuchelewa chuo kikawataka kusubiri kwa wiki mbili ili matokeo yatoke na kama wana Sup wafanye kabisa.
Ajabu tarehe 11/02/2025 mwenye nyumba zake anawafukuza watoto na anayetaka alipe shilingi 5200 kwa kigezo kuwa malipo ya hostel hayahusishi siku za likizo na field. Kutokana na hiyo hali nikamuondoa mtoto na akaenda kukaa kwa ndugu na kesho anarudia somo moja la Hospitality mathematics lakini nimekomaa na chuo kwa sababu wao ndo waliotafuta hizo hostel na mkataba unasema kodi ni shilingi elfu 50 kwa mwezi na siyo kwa siku za masomo.

Chuo wao wameniahidi huyo mama atarudisha hela mwezi mmoja na mtoto wangu atafutiwe hosteli kwingine. Hivo kabla ya kumuona mleta mada kama mshamba asiyeelewa tulipaswa kuhoji mkataba wake unasemaje?
 
Back
Top Bottom