Wanafunzi wa Darasa la 2 kufanya Mtihani wa Taifa

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
14,593
Reaction score
5,581
Naibu waziri wa Elimu bwana Mulugo amesema kuwa serikali ya Tanzania Bara ina mpango wa kuanzisha utaratibu wa kuwa na Mtihani wa Taifa kwa wanafunz wa darasa la 2,
Amesema lengo la kuja na mpango huu ni kupunguza tatizo la wanafunzi wasiokua na maarifa ya kujua KUSOMA,KUANDIKA na KUHESABU(KKK) ambapo inaonesha kwa sasa wanafunzi(baadhi yao) wanaingia sekondari bila kuwa na maarifa ya KKK.
Sosi:Habari Leo 10/09/2013
 
makubwaaa!! sasa mbona wengi watarudia! kwani wa lanne hautoshi? mi naona wangeufanyia kazi vizuri mtihani wa darasa la nne! sasa na lapili nao wanafanya necta jamani si majanga haya! haya kila laheri!
 
wanaenda na kasi ya BIG RESULT NOW,kwa mujibu wa filipo Mulugo
 
mh! iyo big result mwaka huu! haya tusubiri tuone! ila mi ka sijawakubali vile na hiyo necta ya std II

yaani wizara imeona mtihani wa taifa ndio suluhu,lengo ni kuchuja,sasa watakaochujwa na wakaendelea kutojua kusoma,kuhesabu na kuandika watafanywaje???nadhan wanapaswa(serikali)kuongeza vitabu na mazingira bora ya kusomea
 
Necta ni baraza la mitihani Tanzania. Ni chombo kinachosimamia mitihani mbalimbali ya kitaifa. Wala necta siyo mtihani. Si lazima mtihani wa taifa usimamiwe na necta. Ipo baadhi ya mitihani ya taifa haisimamiwi na necta hata huo wa darasa la pili si lazima ukasimamiwa na hicho chombo. Mtihani huo ni muhimu unaweza kuwakumbusha wazazi wajibu wao katika elimu ya watoto wao. Mtoto anafika darasa la nne hajui kusoma na kuandika kwani darasa la nne wanajifunza kusoma na kuandika? Pia unakuta mzazi mwingine hajui mwanae yupo darasa la ngapi. Kwa mtihani huo wazazi na walimu watashirikiana bega kwa bega kuhakikisha mtoto anajifunza anayotakiwa kujifunza, chekechea, darasa la kwanza na la pili na kuyazingatia.
Siyo mtoto anatoka shule anaenda kushinda kwenye vibanda vya video na internet cafe wanacheza games.
 
na ninahisi watakaofeli watakuwa wengi, mwisho wa siku watawakatisha tamaa ya kusoma, we mtu darasa la pili unampa necta khaaaaaaaahh!! wajipange tena ka vipi
 
huwezi kutumia mabilioni ya pesa kurepea paa wakati tatizo liko kwenye msingi,

waboreshe elimu, walipe walimu mishahara mizuri haya mengine yote yatajirekebisha yenyewe.

uvivi wa kufikiria wa serikali yetu unaweza ukawasababisha watoto wadogo kuiogopa elimu na wengi kuacha shule mapema kutokana na mitihani kama hii isiyo na tija
 
Necta ni baraza la mitihani Tanzania. Ni chombo kinachosimamia mitihani mbalimbali ya kitaifa. Wala necta siyo mtihani. Si lazima mtihani wa taifa usimamiwe na necta. Ipo baadhi ya mitihani ya taifa haisimamiwi na necta hata huo wa darasa la pili si lazima ukasimamiwa na hicho chombo. Mtihani huo ni muhimu unaweza kuwakumbusha wazazi wajibu wao katika elimu ya watoto wao. Mtoto anafika darasa la nne hajui kusoma na kuandika kwani darasa la nne wanajifunza kusoma na kuandika? Pia unakuta mzazi mwingine hajui mwanae yupo darasa la ngapi. Kwa mtihani huo wazazi na walimu watashirikiana bega kwa bega kuhakikisha mtoto anajifunza anayotakiwa kujifunza, chekechea, darasa la kwanza na la pili na kuyazingatia.
Siyo mtoto anatoka shule anaenda kushinda kwenye vibanda vya video na internet cafe wanacheza games.

Eeeeh! hayaaa kila la heri basi!
 
Hope1 umeeleza vizuri sana,lakin hivi unajua kuwa kuna shule wanafunz wa madarasa mawili tofauti wanakaa chumba kimoja,mfano la 1 na la 2 wanasomea darasa moja,mwalim akija kwa ajili ya la 1 la 2 wanafunga madaftari kufatilia cha la 1 ingawa hakiwahusu,kitabu kimoja watoto 10.,
na kama hii mitihan haitatungwa na kusahihishwa na NECTA basi ujue tunajidanganya,huwa naona rafu za form II
 
Last edited by a moderator:
huu ni mfumo mwingine wa kuongeza ulaji tu!!!

hamna kitu kabisa!!

baadae watakuja na mtihani wa sita!!

we ngoja tu!
 
makubwaaa!! sasa mbona wengi watarudia! kwani wa lanne hautoshi? mi naona wangeufanyia kazi vizuri mtihani wa darasa la nne! sasa na lapili nao wanafanya necta jamani si majanga haya! haya kila laheri!

Mkuu NECTA inaandaa na kusimamia mchakato mzima wa Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), Mtihani wa Maarifa (QT), Mitihani ya kidato cha Nne (CSEE), Mitihani ya kidato cha Sita (ACSEE), Mitihani ya Vyuo vya Elimu (DSEE, GATCE, GATSCCE) tu.
 
Mulugo anzisha mtihani wa taifa kila darasa, kidato na semester. Hapo necta, nacte na tcu watakuwa bize na mitihani zaidi. Ubora wa elimu tanzania utakuwa juu. Juu zaidi ya dunia.
 
Hope1 umeeleza vizuri sana,lakin hivi unajua kuwa kuna shule wanafunz wa madarasa mawili tofauti wanakaa chumba kimoja,mfano la 1 na la 2 wanasomea darasa moja,mwalim akija kwa ajili ya la 1 la 2 wanafunga madaftari kufatilia cha la 1 ingawa hakiwahusu,kitabu kimoja watoto 10.,
na kama hii mitihan haitatungwa na kusahihishwa na NECTA basi ujue tunajidanganya,huwa naona rafu za form II
Tena mkuu rafu hizo tumegundua huwa zinachezwa sana na wazazi kwa ushirikiano na wakuu wa shule. Wakati ule kabla ya Dk. Ndalichako kufuta matumizi ya matokeo ya FII kama sifa ya watahiniwa binafsi kujisajili Mitihani ya CSEE, wengi wa watoto ambao walishindwa kufika F4 kwa sababu moja au nyingine walikuwa wanajisomea kwenye vitwisheni uchwara mitaani halafu mwisho wa mwaka wanajisajili kufanya kama PC kwa kutumia matokeo ya FII ambayo nayo walifeli kwa alama F.

Lakini kwa kutumia uzoefu wake Dr. Ndalichako na kwa kushirikiana na Ofisi za Ukaguzi wa Shule ambazo ndiyo mmiliki wa mitihani ya FII aliwakamata wengi. Na ndiyo ukawa mwisho wa NECTA kutambua matokeo ya FII kama kigezo cha PC kujisajili kwa mitihani ya CSEE.
 
Kama wizara imeshindwa kuusimamia mtihani wa Darasa la Nne hadi maelfu ya wanafunzi yanafika sekondari yakiwa hayajui kusoma wala kuandika, ni muujiza gani utafanyika ili huo mtihani wa darasa la 2 uwe na ufanisi?
 
Back
Top Bottom