KERO Wanafunzi wa Diploma, Chuo cha Muhimbili-COHAS, Dar es Salaam kuzuiwa kufanya mitihani yao kisa bima za afya

KERO Wanafunzi wa Diploma, Chuo cha Muhimbili-COHAS, Dar es Salaam kuzuiwa kufanya mitihani yao kisa bima za afya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,139
Reaction score
2,223
Wanafunzi wa Diploma, chuo cha Muhimbili-COHAS kilichopo Dar es Salaam kuzuiwa kufanya mitihani yao kisa bima za afya.

Kumekuwepo na malalamiko ya wanafunzi kulalamika kwa kile kinachoendelea katika chuo hicho ambacho kinatoa Elimu kwa ngazi ya diploma (MUCOHAS) huku walimu wakisema maelekezo wamepewa na mkuu wa chuo kama taarifa kutoka NACTE-VET

Maagizo hayo ni pamoja na kuwazuia wanafunzi kutofanya mitihani yao yoyote ile ya ndani na nje.

Naomba kuuliza kwa wadau wa Elimu tamko hili la kuzuia wanafunzi kutokufanya mitihani kisa Bima ya Afya limeanza tangu lini? Ni sheria? Je bunge limepitisha ?

Je, barua ipo wapi yenye maelezo hayo au ni chuo cha mucohas peke yake? Wanafunzi walikuwa wanalalamika walilipia tangu wakiwa mwaka wa kwanza bima zao hawakuwahi kuzipata mpaka wamemaliza wakifatilia wanapewa kalenda.

Changamoto ni nyingi sana kama wazazi tunashangazwa na swala la kuongezwa ADA ghafla katikati ya semista na ilihali ni chuo cha Serikali pia kuna wanafunzi waliopo under TCU wanalazimishwa kuja na rim papers kila semista wakati vitu hivyo havikuapo hata wanafunzi waliopo under TCU upande wa degree hawaleti rim papers.

Serikali tunaomba ufafanuzi wa suala hilo. Bima ya afya ni muhimu lakini si kwa mambo kama ya kuzuia watoto wasifanye mitihani licha ya viongozi wa Serikali kukipa uangalizi maalumu lakini bado mambo ya ajabu yanaendelea.

Watendaji Chuo Cha Muhimbili watakiwa kujitathimini wapewa miezi mitatu ya uangalizi
 
Vyuo vyote huo ndio utaratibu lipa bima acha Janja Janja chalii angu utafeli
 
Mlishaonywa mapema fuata sheria epuka usumbufu bima ni hela ndogo tu..
Ni hela ndogo kwani bima lazima Tena Bima zenyewe, ukiumwa hawakupi dawa za maana unaishia kupewa Panadol tu

Nadhani wasilazimishe mtu kulipa Bima maana sio lazima zaidi ya upigaji.
 
Ni hela ndogo kwani bima lazima Tena Bima zenyewe, ukiumwa hawakupi dawa za maana unaishia kupewa Panadol tu

Nadhani wasilazimishe mtu kulipa Bima maana sio lazima zaidi ya upigaji.
Lipa Bima ndugu
 
Bima ya afya kwa wote itaumiza watu, ni mchongo wa upigaji unaolazimishiwa kwa raia.
 
Serikali lazima uilipie
Yah ni lazima
Ni hela ndogo kwani bima lazima Tena Bima zenyewe, ukiumwa hawakupi dawa za maana unaishia kupewa Panadol tu

Nadhani wasilazimishe mtu kulipa Bima maana sio lazima zaidi ya upigaji.
Mimi ninapinga bima asilimia 100% kwani ni upigaji wa dhahiri na dhuluma iliyo wazi.Sasa kwa mwanafunzi wa chuo hakuna namna inabidi ifuate sheria zinavyosema maana athari zake ni kubwa na itakuwa uzembe kuchelewa au kupuuzwa wakati unajua fika kuwa wakati nasoma joining instructions niliridhia masharti yote pamoja na kujua athari zake kwa kutolipia..
 
Yah ni lazimaMimi ninapinga bima asilimia 100% kwani ni upigaji wa dhahiri na dhuluma iliyo wazi.Sasa kwa mwanafunzi wa chuo hakuna namna inabidi ifuate sheria zinavyosema maana athari zake ni kubwa na itakuwa uzembe kuchelewa au kupuuzwa wakati unajua fika kuwa wakati nasoma joining instructions niliridhia masharti yote pamoja na kujua athari zake kwa kutolipia..
Mkuu Maisha Ni Magumu watu hata hiyo 50k ni mtihani kuipata . Nadhani sio sahihi
 
Yah ni lazimaMimi ninapinga bima asilimia 100% kwani ni upigaji wa dhahiri na dhuluma iliyo wazi.Sasa kwa mwanafunzi wa chuo hakuna namna inabidi ifuate sheria zinavyosema maana athari zake ni kubwa na itakuwa uzembe kuchelewa au kupuuzwa wakati unajua fika kuwa wakati nasoma joining instructions niliridhia masharti yote pamoja na kujua athari zake kwa kutolipia..
Nakubaliana na wewe
 
Nadhani serikali iliqngalie hili kwa ukaribu.. iweke mazingira rafiki kwa wanafunzi hasa wanapoenda kutibiwa mara nyingi wenye bima hawapewi kipaumbele hasa wanafunzi inawalazimu waende hospital ya private.

Kwa tuliopitia maisha ya shule au kusoma mzazi akilipa pesa ya bima anajua kabisa kila kitu amemaliza kazi inabaki kwa mtoto kuhangaika pale anapochelewa kupata huduma.

Suala la kuzuiwa kufanya mtihani hapo kidogo kuna utata kama tumefikia huko basi serikali itoe taarifa rasmi .

Bima ni muhumu kwa wote utaratibu mathubuti uandaliwe..
 
Bima yenyewe si ni 54k, unatumua mwaka mzima.

Walipe tuu.
 
Tatizo hizi Bima wanazozungumzia hazimsaidii kabisa Mwanafunzi.

Mtu anaumwa labda Typhoid au Malaria akienda na kadi yake wanaishia kumoa Paracetamol

Wajinga sana hao watu wa Bima ya Afya
 
Back
Top Bottom