kwanza napenda nitoe historia ya MTC kidogo MTC ni chuo kilichokuwa kinaundwa na kozi zifuatacho: Mechanical, Electrical, Civil, na Architecture engineering japo ilikuwa ni elimu ya Fundi mchundo lakini ilikuwa nielimu ya Chuo kikuu kwa 75%. kwanini nasema hivyo? kwa sababu wanafunzi walikuwa huru sana hatukuwa na uniform za kuvaa tulikuwa tunaishi maisha ya raha mastarehe kama kufikwa (kuleta mwamke/msichana) ilikuwa ni ruksa na ilikuwa ni fahari kwa mkuu wetu wa chuo kipindikile Mzee Zuberi. Masomo yalikuwa magumu sana na tulikuwa tunaandaliwa sikuendelea na shule bali kwenda kufanya kazi. Maana kipindikile kwenda Chuo Kikuu bila na kuwa na B ya mathematics na at least masomo yako wastani wake lazima uwe C huwezi pata. Nje ya hapo kuapata hata cheti ilikuwa ngumu umesoma miaka yako 3 kwa kuruka viunzi kila term na mitihani yake ukifail nyumbani na mwishoni sasa unakusanya material yote ya mwaka wa kwanza unafanyia mtihani wa kwa masaa 3. Si hivyo tu ukipata "A" 5 kati ya masomo 6 ukafail moja hupati cheti na ukirudia mtihani ukafail mara 2 basi cheti hupati milele, ilikuwa ni bora kupata "D" zote iliuweze kuchukua cheti. Lakini istoshe kuipata hata 'D" haikuwa rahisi maana range yake D=(50-69), C=(70-79) B=(80-89) A=( 90-100)haikuwa rahisi sana wadau kuweza kuendelea na chuo kikuu au hata elimu ya juu