Tetesi: Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Thaqaafa Mwanza wanusurika Kubakwa

Tetesi: Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Thaqaafa Mwanza wanusurika Kubakwa

Edsger wybe Dijkstra

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2019
Posts
244
Reaction score
491
Wanafunzi wakike shule ya Sekondari Thaqaafa iliyoko mkoa wa Mwanza , wilaya ya Nyamagana wamenusurika kubakwa baada ya vibaka watatu kuingia ndani ya bweni saa nane usiku.

Wakiwa katika harakati za kumziba mdomo mmoja wa wanafunzi ili asipige kelele waanze kumbaka, ghafla mwanafunzi mwenzake alishtuka na kupiga mayowe yaliyofanya vibaka hao kutoka mbio na kutokomea kusikojulikana.

Baadhi ya wanafunzi waliohojiwa kisiri siri wanadai matron wa shule aliwambia hatoshughulika na kitu chochote kwa sababu hajalipwa mshahara wake kwa miezi takriban 3 na kitu.Hivyo hakujali kuhakikisha anafunga milango ya bweni.

Pia wanafunzi wameonywa kutotoa taarifa zozote, inaonekana uongozi unataka jambo hili liishie chini ya kapeti.

Update: Taarifa za uhakika zinasema sio vibaka kutoka nje shule bali ni wanafunzi wa kiume wa hapo hapo Thaqaafa ndio walifanya kitendo hicho.

Nimeshtushwa sana kwa sababu shule hii nilishamuonya sana jamaa yangu mmoja asipeleke mtot tangu ilipofungiwa kituo kwa kuibia mitihani lakini hakuniskia,

Soma Pia: Mwanza: Wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Thaqaafa waandamana kudai matokeo ya watoto wao

Hii shule wanaoifahamu wanadai ina changamoto lukuki kila sector na uongozi wake ni wa kiswahili swahilina hivi.Pia naskia ina mgogoro mkubwa wa umiliki.

My take: SERIKALI ITAZAME SHULE KAMA HIZI NA HATUA ZICHUKULIWE DHIDI YA WAHUSIKA.INASEMEKANA MPKA SASA VIONGOZI WA SHULE HII HAWAJACHUKUA HATUA YOYOTE DHIDI YA MATRON KWA KILE KINACHODAIWA KUWA NI KUOGOPA KUDAIWA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA .
 
Thaqaafa enzi zake ilikuwa dhule kubwa sana mwanza sijui ni nini kimeitokea
 
Wanafunzi wakike shule ya Sekondari Thaqaafa iliyoko mkoa wa Mwanza , wilaya ya Nyamagana wamenusurika kubakwa baada ya vibaka watatu kuingia ndani ya bweni saa nane usiku.Wakiwa katika harakati za kumziba mdomo mmoja wa wanafunzi ili asipige kelele waanze kumbaka, ghafla mwenzake aliyefahamika kwa jina moja la Sunaiya alishtuka na kupiga mayowe yaliyofanya vibaka hao kutoka mbio na kutokomea kusikojulikana.
Miongoni mwa vichocheo vya kubaka ni👇
 
Update : Taarifa za uhakika zinasema sio vibaka kutoka nje bali ni wanafunzi wa kiume wapatao wanne walitoroka bwenini kwao na kwenda kuingia bwenini kwa wasichana kutaka kubaka.
 
Wazee wa makobasi katika ubora wao
..mnaendeshaje shule kama madrasa ?
 
Vibaka ndo wanusurika kubakwa mkuu na wala sio wanafunzi
 
Inatakiwa wa Improve security system, Ili wazazi wawe na amani na watoto wao...!

Matukio kama hayo yatampunguzia wateja kwenye shule yake....!
 
We ni muongo sana…nimesoma thaqaafa na nimekulia hyo mitaa …Hakuna kibaka wala haijawah tokea kibaka kutaka kuruka ukuta kwenda kuiba au kubaka wanafunzi humo!! Ni Uongo.
 
Thaqaafa kinachowaponza ni tamaa ya pesa kila mwanafunzi wanamchukua bila kufanya background check, tukio hili ni kweli limetukia lakni sio vibaka, ni wanafunzi wa kiume wa hapo hapo thaqaafa ndio waliingia bwenini usiku wa manane kujarbu kubaka.
Pia wamepokea wanafunzi wengi waliofukuzwa kwenye shule nyingine kwa sababu za utovu wa nidhamu.Unaambiwa sasa ivi thaqaafa sio ile tuliyosoma sisi, bweni la wavulana ushoga umetamalaki kweli kweli
 
We ni muongo sana…nimesoma thaqaafa na nimekulia hyo mitaa …Hakuna kibaka wala haijawah tokea kibaka kutaka kuruka ukuta kwenda kuiba au kubaka wanafunzi humo!! Ni Uongo.
Mkuu ata mimi nimesoma hapo napajua, tukio ni kweli limetukia lakini sio vibaka kutoka nje , ni wanafunzi wa kiume walitoroka bwenini kwao usiku wa manane
 
Hii ni vita ya kibiashara. Na mleta mada amehamisha magoli kutoka kuwa ni vibaka hadi kuwa wanafunzi wanne wa shule hiyo hiyo. Ukiwa muongo ni lazima uwe na kumbukumbu.Someni between the lines mtamuelewa mleta mada anachokusudia.
 
Back
Top Bottom