Wanafunzi wa Kimarekani Wakiendesha Mdahalo wa Urais wa Tanzania kwa Kiswahili

Soma historia wacha uzembe bro, vitabu vipo.
Mimi nazungumza kuhusu kabila la Wangozi lililokuwepo tangu, hata kabla mwarabu hajaja kubuni hiyo dola.
Nimesoma historia ya kiswahili form 3&4 kiongozi...... Lakini sidhani kama nilishakutana na jina la kabila unalosemea....
 
Mi navyojua kiswahili kimeanzia pwani ya Mombasa na ni cha ufasaha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma historia ya kiswahili form 3&4 kiongozi...... Lakini sidhani kama nilishakutana na jina la kabila unalosemea....

Kwa utandawazi uliopo kwenye karne ya leo inashangaza kwa wewe kushikilia bango la elimu ya sekondari.
Jiongeze kaka, tafiti kote kote, nimesema vitabu vipo, taarifa zipo, wazee wapo yaani sijui unakwama wapi.
 
Basi sawa.... Ila unapoanza kujifunza kitu utaanza kwanza kujifunza chimbuko lake..... Ndo maana cha kwanza kujifunza kwenye historia ya kiswahili ni chimbuko tena mapema sana sekondari...... Ukiletewa swali la origin ya kiswahili kwenye mtihani huku bongo (tuseme CSEE) halafu useme chimbuko ni hilo kabila ulilotaja,aisee utalia na mtihani matokeo yakija...
 
Historia ya shule huwa imepindishwa pindishwa kiaina, haijakamilika, ila yote tisa, kila lugha dunia hii ina kabila ilikochimbukia, hata Kingereza ukifuata chimbuko chake utashangaa sana.
 
Historia ya shule huwa imepindishwa pindishwa kiaina, haijakamilika, ila yote tisa, kila lugha dunia hii ina kabila ilikochimbukia, hata Kingereza ukifuata chimbuko chake utashangaa sana.
Hilo kabila ndo lile lililopo maeneo ya Turkana
 
Hilo kabila ndo lile lililopo maeneo ya Turkana

Nahisi kuna sababu kwanini historia ilikupiga chenga shuleni, haupo makini kwenye kufuata taarifa.
Kabila la Pwani litapatikanaje mikoani, ni kama kwenda Njombe ukatafute kabila la Wazaramo.
 
Nahisi kuna sababu kwanini historia ilikupiga chenga shuleni, haupo makini kwenye kufuata taarifa.
Kabila la Pwani litapatikanaje mikoani, ni kama kwenda Njombe ukatafute kabila la Wazaramo.
Duh! Kumbe ni la pwani samahani mkuu.... Mm nakumbuka nimesoma kuhusu kikundi fulani cha wabantu huko maeneo ya turkana kinachosadikika ndo chimbuko la kiswahili...... Nakumbuka nilisoma kikundi hicho kilivamiwa na kabila fulani linaloitwa wazimba(siko sure na hilo jina ndo ikawafanya wenyeji kukimbilia maeneo ya pwani...
Ndo maana nilikuwa nafikir hilo kabila ndo hicho kikundi unachokisemea.... Lakini kama ni kabila la pwani haina shaka itakuwa ni theory nyingine tu hiyo....
 
Q Poa ila pia Turkana sio Bantu, wapo kwenye kundi la Nilotes ambalo limesheheni Wamaasai pia.
 
Kabisaa !!!! Na baadhi ya watu wakiiona mgeni/mzungu anaongea kiswahili hujikuta wakifunguka balaa bila kujielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…