Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Hapo kuna mmoja kashika mpini mwingine kwenye makali...nani mshindi?
 
Hii imenikumbusha SAUT-MWANZA, masalia walifukuzwa. Wakaambiwa hata wakienda mahakamani hawatawapokea. Kwamba chuo kinaongozwa kwa mila na desturi za canon law. Hizi shule/vyuo vya kanisa ni vya kuogopa. Wanaweza kufukuza chuo kizima wakaanza upya!. Tena usije chezea warumi. Kwa mfano nimeshuhudia kosa la mwanafunzi kumpiga refa uwanjani anafukuzwa chuo, msichana kuvaa suruali unafukuzwa, kuandamana unafukuzwa. Na hii imesababisha nidhamu kuwepo.
 
Siku sita fanya kazi na siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako........Kutoka 20:8-11

Mathayo 27:57 Kufa siku ya maandalio
Mathayo 28:1 siku ya kwanza ya juma Alifufuka.
Yesu alikufa siku ya maandakio( Ijumaa) ambayo ni Good Friday kwa RC
Alifufuka siku ya kwanza (Jumapili) ambayo ndio siku Iitwayo Pasaka kwa RC.....hadi hapo Jumamosi ndio siku ya Saba ambayo ni Sabato ya Bwana.
 
Naona wapinga kristo mmejipanga hapa mnachekelea kuona watumishi wa Mungu wakisimamishwa masomo kwa sababu ya kutaka kuwalazimisha kufanya/kutenda kinyume na maagizo/amri za Mungu.

Kabla hamjaendelea kuropoka ni vizuri mkajisomea maandiko matakatifu na kuyaelewa. Wengi wenu mnaonekana hamuijui Sabato wala hamzijui amri kumi za Mungu kwakuwa mnatumia amri zilizochakachuliwa na mwanadamu.

Kutoka 20:8-11 unasema hivi:
"8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu".

Kwanza kabla ya mjadala kuendelea, ningependa kujua ni vitu gani ambavyo si ruhusa kwa SABATOS kuvifanya siku ya jumamosi, tukisha jua hilo then, tutaweza kuuweka mtihani katika kundi gani, baadae kutoa maamuzi, karibu..

Ya kaisari apewe kaisari na ya Mungu apewe Mungu, waache kuchanganya dini na taaluma, vyuoni si mahala pa kudumu ni sehemu za kupita tu na kila sehemu kuna taratibu zake, kila mtu kila sehemu akisema afanye kwa jinsi anavyoamini unadhani kuna la maana litaendelea kweli?

Nadhani wanafunzi waache ujinga, mtihani siku ya J1 wala J2 au siku zingine haina shida. Mbona waislam wanafanya kazi Ijumaa? Mbona shuguli za chaguzi hufanyika J2?

Sabato ya kweli ni pumziko moyoni, lipatikanalo ndani ya Yesu pekee ambaye ni Bwana wa sabato. Siku zote ni za Mungu, hakuna hata moja ambayo ni ya shetani, na siku zote inabidi tumwabudu Muumba.

Kakika nchi za kiarabu, wakristo hukusanyika siku ya Ijumaa (J1 na J2) ni siku za kazi.

Alafu wakati leo hapa ni J1 kwingine ni Ijuma au J2. So kasome maandiko vizuri, wahsauri wanafunzi wenu wakafanye mitihani siku yoyote itakapotolewa.

Pia Yesu alisema msingi wa sabato ni kufanya mema, kama vile "kumokoa punda shimoni", mtijani wako na wa thamani sana kuliko thamani ya Punda!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mbona kuna vyuo kama IFM na Mzumbe wanafanya mitihani siku za jumamosi na hatujasikia wasabato kufukuzwa? Au wa TEKU ni masalia?

Kuna jamaa yangu ni msabato na anaishi na demu wake geto moja.linapofika swala la kufanya mitihani au presentation jumamosi alikua anagombana sana na ma doctor.siku moja nikamwambia mbona unaishi na mwanamke na mnazini huoni hiyo ni dhambi au dhambi ni kufanya kazi jumamosi?amenichukia mpaka leo.wakati mwingine haya mambo ya imani tunajichanganya sana.

sabato ni siku ya kwanza ya juma, na wala sio jumamosi, someni maandiko

Hao waache ujinga wa kuleta dini vyuoni mbona waislamu wanafanya mitihani ijumaa,wasituletee visilani basi waende vyuo vya kisabato.

Walisoma By Laws za chuo wakati wa kujiunga au kurudisha form za kujoin na chuo? Wao kwa nini hawakuchagua vyuo vya kisababto kama wanapenda usabato? Chezea warumi weweee utageuka kuwa six leaver hata mahakama ifikie wapi!!

SAUT Mwanza walileta hizo nyodo, wakafukuzwa bila kurudishiwa chao. Wachache wakaomba msamaha wakasamehewa.

Afu wengi wa wanafunzi (Wasabato ) walio goma walikuwa wanaishi kama mke na mme bila ndoa, hivyo kukutanisha vikojoleo kwao ilikuwa kama kawa licha ya amri za Mungu kukataza. Tena kipindi hicho jmosi haikuwa siku ya masomo ila mwl aliweza kuomba wanafunzi kusoma siku hiyo. Tangia wasabato walete kimbelembele hadi leo jmosi ikawekwa kwenye time table kama siku ya j3 hadi Ijumamosi mapindi kama dawa na paper kama kawa J3 hadi Jmosi.

Bwana Yesu Asiwe.

Hiyo ndiyo amri ya Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu, sasa ikitokea kuna mtu mmoja ama wawili wamekwenda kinyume na amri hiyo ama amekwenda kinyume na amri nyengine ya Mungu kati ya zile kumi hiyo haihalalishi uvunjifu wa amri nyengine ama kuwafanya wengine wawe wakosaji ama kushurutishwa kukiuka maagizo ya Mungu kwakuwa wengine walikiuka.

Najua yapo baadhi ya madhehebu ya kikristo yanachuki kubwa sana na Kanisa la Waadventista Wasabato kwa sababu wanazozijua wao wenyewe lakini hilo halijawahi kuwa tatizo kwa Wasabato hata mara moja kwakuwa hiyo sio kazi yao ya kuwahukumu watu.

Kwa wananfunzi Wasabato walioko katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, mimi napenda kutumia fursa hii kuwatia moyo kwamba muendelee kuwa na imani thabiti kwakuwa hayo mnayokutana nayo ni majaribu ya shetani ili kujaribu kupima imani yenu, na kamwe Mungu hatawatupa mkono na hatimaye mtafanikiwa kuhitmu masomo yenu na kupata shahada zenu, aidha hapo mlipo kwa sasa ama mahali pengine.

Napenda niwakumbushe kisa cha Pastor Dkt. Herry Mhando ambaye alifukuzwa shule ya sekondari akisoma masomo ya A Level kwa kukataa kufanya mitihani siku ya Sabato takatifu lakini Mungu alisimama nae na akafanikiwa kusoma hadi kiwango cha kupata shahada zake kadhaa kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambulika na kuheshimika sana duniani.

Pia niwashuhudie kuw mimi binafsi pamnoja na wanafunzi wenzangu tuliwahi kukumbana na mazingira hayo ya kulazimishwa kufanya mitihani siku za jumamosi wakati tukihangaika kujitafutia elimu katika ngazi za elimu ya juu lakini tulisimama imara na hatimaye Mungu akatushindia. Kwahiyo hili linalowatokea sio mara ya kwanza na haitokuwa mara ya mwisho kutokea kuwa shetani anafanya kazi kwa njia mbalimbali na mbinu mbalimbali. Jambo la msingi na la muhimu sana kwenu ni kuendelea kumtegemea Mungu na kufanya mambo yenye kumpendeza Mungu kwani kwa hakika mtashinda tu!
 
Sabato iliumbwa kwa ajili ya Binadamu na sio binadamu kwa ajili ya sabato.....
MUNGU aliIumba Mbingu na Nchi kwa Siku sita na siku ya saba akapumzika.
Mathayo 5:17-18
Msidhani yakuwa nalikuja kulitangua torati au manabii ; la sikuja kulitangua bali kulitimiliza, kwa maana nawambia mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja haitaondoka hata yote yatimie............
Warumi 7:12
Nehemia 9:13
 
Kila kitu kinawezekana chini ya roho mtakatifu.Kama roho mtakatifu aliwaongoza kuona mitihani si sehemu ya kutenda mema basi wako sahihi.Wasi wasi wangu ni je kweli roho mtakatifu amewaongoza hivyo?Wengi wa waadvetista wasabato,wanaongozwa na vitabu vijulikanavyo kama' roho ya unabii'Nilikuja kugundua baadhi ya maandiko humo yanayotia shaka!Nilipojifunza zaidi nikagundua kuwa hata anayedhaniwa kuviandika(Ellen White)atawashangaza pale atakapoyakana baadhi ya maandiko yake!Nimegundua Illuminat walitia mkono wao kwa ustadi mkubwa sana!Nawashauri waitegemee biblia pekee kwani ndicho kitabu ambacho watajaribu kukichakachua lakini Mungu hawezi kuruhusu wafanikiwe hadi nyakati za Bwana zitimie.Biblia ukiisoma kwa unyenyekevu,itatoa majibu kwa mashaka yote.Kwani sisi leo tumepewa siku moja tu 'LEO'ndiyo siku ya kumpa Mungu utukufu.Tuangalie shetani asije akatumia maandiko ku divert attention yetu tukatumia akili za kibinadamu na kusahau jinsi tulivyoahidiwa roho mtakatifu!Kwani yeye anafurahia kutokufanikiwa kwetu kimwili na kiroho.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.......

Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani

Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria


  1. Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
  2. Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
  3. Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?

Je mnawashauri nini wanajamvi?

Hao ni maagent wa shetani. Maana nyakati za mwisho!! Mungu atafanya kitu tuzidi kuwaombea tu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Dhambi zote wangeziogopa kama hii, dunia ingekuwa mahali pazuri pa kuishi.
Anyway . . . .

Na Ijumaa nao wakatae?
 
Hao wanastahili kufukuzwa na naunga mkono uongozi wa chuo kwa 100 asilimia, wangekwenda kusoma vyuo vya kisabato kuepeka usumbufu kuliko kuleta usumbufu kwenye vyuo vya umaa ama vya mathehebu mengine

i dont think so
 
Poleni nyie mnaadhibiwa kwa kushika amri ya Mungu..... ila njia rahisi ni kuachana na hawa Warumi na washirika wao a.k.a Maant Christ waliobariki ndoa za jinsia moja cha kufanya ni kujiunga na vyuo vya kisabato kama ni wanafunzi wa education,na bba watapokelewa University of Arusha.. vyuo vingine vya SDA kwa hao wanafunzi wsliofukuzwa ni Bugema University na Univ of EA Baraton
 
Back
Top Bottom