Naona wapinga kristo mmejipanga hapa mnachekelea kuona watumishi wa Mungu wakisimamishwa masomo kwa sababu ya kutaka kuwalazimisha kufanya/kutenda kinyume na maagizo/amri za Mungu.
Kabla hamjaendelea kuropoka ni vizuri mkajisomea maandiko matakatifu na kuyaelewa. Wengi wenu mnaonekana hamuijui Sabato wala hamzijui amri kumi za Mungu kwakuwa mnatumia amri zilizochakachuliwa na mwanadamu.
Kutoka 20:8-11 unasema hivi:
"8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu".
Hiyo ndiyo amri ya Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu, sasa ikitokea kuna mtu mmoja ama wawili wamekwenda kinyume na amri hiyo ama amekwenda kinyume na amri nyengine ya Mungu kati ya zile kumi hiyo haihalalishi uvunjifu wa amri nyengine ama kuwafanya wengine wawe wakosaji ama kushurutishwa kukiuka maagizo ya Mungu kwakuwa wengine walikiuka.
Najua yapo baadhi ya madhehebu ya kikristo yanachuki kubwa sana na Kanisa la Waadventista Wasabato kwa sababu wanazozijua wao wenyewe lakini hilo halijawahi kuwa tatizo kwa Wasabato hata mara moja kwakuwa hiyo sio kazi yao ya kuwahukumu watu.
Kwa wananfunzi Wasabato walioko katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, mimi napenda kutumia fursa hii kuwatia moyo kwamba muendelee kuwa na imani thabiti kwakuwa hayo mnayokutana nayo ni majaribu ya shetani ili kujaribu kupima imani yenu, na kamwe Mungu hatawatupa mkono na hatimaye mtafanikiwa kuhitmu masomo yenu na kupata shahada zenu, aidha hapo mlipo kwa sasa ama mahali pengine.
Napenda niwakumbushe kisa cha Pastor Dkt. Herry Mhando ambaye alifukuzwa shule ya sekondari akisoma masomo ya A Level kwa kukataa kufanya mitihani siku ya Sabato takatifu lakini Mungu alisimama nae na akafanikiwa kusoma hadi kiwango cha kupata shahada zake kadhaa kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambulika na kuheshimika sana duniani.
Pia niwashuhudie kuw mimi binafsi pamnoja na wanafunzi wenzangu tuliwahi kukumbana na mazingira hayo ya kulazimishwa kufanya mitihani siku za jumamosi wakati tukihangaika kujitafutia elimu katika ngazi za elimu ya juu lakini tulisimama imara na hatimaye Mungu akatushindia. Kwahiyo hili linalowatokea sio mara ya kwanza na haitokuwa mara ya mwisho kutokea kuwa shetani anafanya kazi kwa njia mbalimbali na mbinu mbalimbali. Jambo la msingi na la muhimu sana kwenu ni kuendelea kumtegemea Mungu na kufanya mambo yenye kumpendeza Mungu kwani kwa hakika mtashinda tu!