Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.......

Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani

Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria

  1. Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
  2. Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
  3. Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?

Je mnawashauri nini wanajamvi?

Ndo maana huwa ninasema wasabato wana matatizo ya akili. How comes ugome kufanya UE kwa sababu eti unatunza sabato. Kwanza mna uhakika gani kama hiyo Jumamosi ndio siku ya saba kama ilivyo fuatwa na wayahudi wa enzi za Mussa? YESU Mwenyewe alifanya kazi siku ya sabato na yeye ndie Bwana wa SABATO. Mungu hafungwi na siku wala miandamo ya miezi. Mungu haabudiwi katika siku ya sabato, Mungu ana abudiwa katika roho na kweli. Sheria zifuate mkondo wake, hao wanafunzi wafukuzwe chuo kwa ku reject kufanya mitihani.
 
Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.......

Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani

Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria

  1. Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
  2. Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
  3. Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?

Je mnawashauri nini wanajamvi?

Watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa (HOSEA 2: 28 )...Yesu alisema Iweni wapole kama huwa na werevu kama nyoka na Ya Mungu mpeni Mungu na ya kaisari mpeni kaisari.
 
Msabato haruhusiwi kutoka jasho na asitembee umbali zaidi ya jiwe litakapododoka baada ya kulitupa toka mlangoni kwake. Ukiwa Dar kuna joto na mtu anatokwa na jasho bila hata ya kutoka nje, hivyo ni dhambi. Kama mtu anatoka nyumbani kwake hadi kanisani ambapo ni mbali na kwake, anatenda zambi. Hivyo kama kuna mazambi hayo mengi itakuwa ni upuuzi kutofanya mtihani ati utatenda dhambi
Okay, nimekupata mkuu, kwamba kwa maoni yako, kufanya mtihani jmosi si tatizo kwa wana sabatos.
 
Nadhani wanafunzi waache ujinga, mtihani siku ya J1 wala J2 au siku zingine haina shida. Mbona waislam wanafanya kazi Ijumaa? Mbona shuguli za chaguzi hufanyika J2?

Sabato ya kweli ni pumziko moyoni, lipatikanalo ndani ya Yesu pekee ambaye ni Bwana wa sabato. Siku zote ni za Mungu, hakuna hata moja ambayo ni ya shetani, na siku zote inabidi tumwabudu Muumba.

Kakika nchi za kiarabu, wakristo hukusanyika siku ya Ijumaa (J1 na J2) ni siku za kazi.

Alafu wakati leo hapa ni J1 kwingine ni Ijuma au J2. So kasome maandiko vizuri, wahsauri wanafunzi wenu wakafanye mitihani siku yoyote itakapotolewa.

Pia Yesu alisema msingi wa sabato ni kufanya mema, kama vile "kumokoa punda shimoni", mtijani wako na wa thamani sana kuliko thamani ya Punda!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

mkuu umesomeka na kueleweka.
 
Naona wapinga kristo mmejipanga hapa mnachekelea kuona watumishi wa Mungu wakisimamishwa masomo kwa sababu ya kutaka kuwalazimisha kufanya/kutenda kinyume na maagizo/amri za Mungu.

Kabla hamjaendelea kuropoka ni vizuri mkajisomea maandiko matakatifu na kuyaelewa. Wengi wenu mnaonekana hamuijui Sabato wala hamzijui amri kumi za Mungu kwakuwa mnatumia amri zilizochakachuliwa na mwanadamu.

Kutoka 20:8-11 unasema hivi:
"8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu".

Hiyo ndiyo amri ya Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu, sasa ikitokea kuna mtu mmoja ama wawili wamekwenda kinyume na amri hiyo ama amekwenda kinyume na amri nyengine ya Mungu kati ya zile kumi hiyo haihalalishi uvunjifu wa amri nyengine ama kuwafanya wengine wawe wakosaji ama kushurutishwa kukiuka maagizo ya Mungu kwakuwa wengine walikiuka.

Najua yapo baadhi ya madhehebu ya kikristo yanachuki kubwa sana na Kanisa la Waadventista Wasabato kwa sababu wanazozijua wao wenyewe lakini hilo halijawahi kuwa tatizo kwa Wasabato hata mara moja kwakuwa hiyo sio kazi yao ya kuwahukumu watu.

Kwa wananfunzi Wasabato walioko katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, mimi napenda kutumia fursa hii kuwatia moyo kwamba muendelee kuwa na imani thabiti kwakuwa hayo mnayokutana nayo ni majaribu ya shetani ili kujaribu kupima imani yenu, na kamwe Mungu hatawatupa mkono na hatimaye mtafanikiwa kuhitmu masomo yenu na kupata shahada zenu, aidha hapo mlipo kwa sasa ama mahali pengine.

Napenda niwakumbushe kisa cha Pastor Dkt. Herry Mhando ambaye alifukuzwa shule ya sekondari akisoma masomo ya A Level kwa kukataa kufanya mitihani siku ya Sabato takatifu lakini Mungu alisimama nae na akafanikiwa kusoma hadi kiwango cha kupata shahada zake kadhaa kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambulika na kuheshimika sana duniani.

Pia niwashuhudie kuw mimi binafsi pamnoja na wanafunzi wenzangu tuliwahi kukumbana na mazingira hayo ya kulazimishwa kufanya mitihani siku za jumamosi wakati tukihangaika kujitafutia elimu katika ngazi za elimu ya juu lakini tulisimama imara na hatimaye Mungu akatushindia. Kwahiyo hili linalowatokea sio mara ya kwanza na haitokuwa mara ya mwisho kutokea kuwa shetani anafanya kazi kwa njia mbalimbali na mbinu mbalimbali. Jambo la msingi na la muhimu sana kwenu ni kuendelea kumtegemea Mungu na kufanya mambo yenye kumpendeza Mungu kwani kwa hakika mtashinda tu!
Kwa ufahamu wangu mdogo ni kwamba siku ya sabato ilikua hairuhusiwi kufanya kazi za nguvu, kama vile, kulima, kuwinda wanyama, kuvua samaki, kujenga majumba na kazi za biashara. sasa mimi sijaona kama test au mtihani unahusika na hayo niliyoyataja hapo juu. Jee inaruhusiwa msabato kujiunga na jeshi? kama ndivyo, ikitokea mashambulizi siku ya Jumamosi atachukua hatua gani..??
Naheshimu sana imani za watu, lakini pia nawashauri waumini wawe na tafsiri sahihi ya wanachokisoma, ikitokea kwamba mitihani imekatazwa thats fine, stick on it..
 
Siku sita fanya kazi na siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako........Kutoka 20:8-11

Mathayo 27:57 Kufa siku ya maandalio
Mathayo 28:1 siku ya kwanza ya juma Alifufuka.
Yesu alikufa siku ya maandakio( Ijumaa) ambayo ni Good Friday kwa RC
Alifufuka siku ya kwanza (Jumapili) ambayo ndio siku Iitwayo Pasaka kwa RC.....hadi hapo Jumamosi ndio siku ya Saba ambayo ni Sabato ya Bwana.
Ewe Mfarisayo lini utabadilika...? Ninyi Wasabato(mafarisayo) Yesu alipata tabu sana na nyinyi....Ila hakuna shida maaana hao mafarisayo wenzako wako mtaani wana kula jeuri yao..
 
Poleni nyie mnaadhibiwa kwa kushika amri ya Mungu..... ila njia rahisi ni kuachana na hawa Warumi na washirika wao a.k.a Maant Christ waliobariki ndoa za jinsia moja cha kufanya ni kujiunga na vyuo vya kisabato kama ni wanafunzi wa education,na bba watapokelewa University of Arusha.. vyuo vingine vya SDA kwa hao wanafunzi wsliofukuzwa ni Bugema University na Univ of EA Baraton

SDA=Mormon=Jehova Witness=Mafarisayo
 
Ufunuo wa Yohana 13:1-18
Inaongelea Mnyama........Papa

Ha ha ha....Umajaribu kupotezea mada ehhh....masikini Helen G White amepotosha kizazi cha Mafarisayo(Wasabato)....Any way hiyo ni tungo ya zamani sana njoo na tungo mpya...
halafu eti nasikia pia hamruhusiwi kuoga siku ya Sabato...? Hebu nipe jibu fasta ewe Mfarisayo..

Wasabato=Jehova Witness=mormon=Cult religion...
 
Acha upotoshaji, Muogope Mungu.Tazama Ufunuo 22: 18, 19. "Na mtu yeyote akiongeza au akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima..."

Upotoshaji upi wewe Mfarisayo...Kwasasa kanisa la SDA linahaha kufanya reformation ya baadhi ya mambo waliyokuwa wanaamini...Maana hayana maana ....Kama kuto kuoga siku ya Sabato....
 
Dini inapokuwa mzigo na upofu wa kiimani ni janga! Unakataa kufanya mitihani ili kuilinda sabato wakati una dhambi nyingine kibao unazifanya ni upumbavu

Hili ndiyo lile dhehebu ambalo waumini wake walimaliza mwezi pale JKIA wakitaka kwenda Iraq bila passport wala VISA?
 
Okay, nimekupata mkuu, kwamba kwa maoni yako, kufanya mtihani jmosi si tatizo kwa wana sabatos.
Sawa kabisa na hata nabii Issa alisema huwezi acha ndama katumbukia kisimani ukaenda kusali siku ya sabato. Ndo maana sie unaambiwa ukaswali na uendelee na kazi siku kama ya leo
 
Sawa kabisa na hata nabii Issa alisema huwezi acha ndama katumbukia kisimani ukaenda kusali siku ya sabato. Ndo maana sie unaambiwa ukaswali na uendelee na kazi siku kama ya leo
I get you precisely.....
 
Mmmh!!
Mambo ya Imani yana changamoto sana katika jamii yenye watu mchanganyiko wa kiimani.

Katika maisha yangu nimekutana na watu ambao wana siku maalum ya kufanya Ibada kuu(Ni muhimu na lazima wao waabudu siku hiyo na wasipofanya hivyo kwao ni dhambi kubwa sana!!!). Kwa mfano Alhamisi(Hindu, Budha?), Ijumaa(Waislam), Jumamosi(Wasabato), Jumapili(Wakristo wengi), Jumatatu(Mansonia? Free......!?).
Hao wote wangependa wasifanye kitu chochote siku yao ya kuabudu zaidi ya kujiandaa kwenda Ibada, kusali na kupumzika tu. Sasa kila mmoJa akitaka iwe anavyotaka sijui kama Shule, vyuo, Ofisi, biashara, siasa, michezo nk. kama vinaweza kufanyika?

Hapa inahitajika Hekima na Busara tu na wala sio misimamo mizito mizito.
Na kwa vyovyote vile lazima watakuwepo watu watakao athirika ni maamuzi ya kijumuiya.
 
Hiyo ni tafsiri yako juu ya maandiko, sio lazima kila mtu akubaliane nayo, mambo ya imani should be handled with care.

Back
Top Bottom