Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

umeenda deep lakn kabla ya mahakama huenda wa ex host local remedies, kuna chama chao cha ma[pro walikianzisha, hakiwezi kuwasaidia?
Nawashauri waende mahakamani.Pia wakumbuke kuwa watachukiwa na wengi na hata wakuu wa chuo watafanya namna ili kuwatimua kwa njia yoyote ile.Mfuata ukweli siku zote hupondwa na huchukiwa na watu na ndo maana watu wengi humu jf wanacomment kwa matusi na kashfa.Cha msingi wazidi kumuomba Mungu naye atawasaidia tu.
 
umeanza vizuri sana ila umalizoaji mbovu
Hujui kitu wewe kaa kimya ,maandiko yanasema Yesu alitesa msalabani siku ya maandalio ya sabato .jiulize ni lini kisha pigia mstari.Ila waache ujinga kama wanataka hivyo na waislam nao ?DIMAYO nao? Bahai? Acha wakae mtaani wajifunze

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Wanayepaswa kumfuata alisema, "..ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu, mpeni Mungu"

Hawa jamaa wanalazimisha ya Mungu wampe Kaisari na vice versa!!

Kimsingi binafsi naona ni mwanafunzi ambaye hajajiandaa tu ndio anayeweza kugomea mtihani kwa sababu ya aina hii!

Nguvu mtu anayotumia kujiandaa na mtihani ni kubwa sana kiasi kwamba sababu za kipuuzi hazina nafasi kuahirisha mtihani!
nadhani nguvu ya kumtafuta Mungu ni kubwa zaidi.....................
 
nadhani nguvu ya kumtafuta Mungu ni kubwa zaidi.....................

Mfano ule wa Yesu juu ya kumpa Kaisari yaliyo yake, na Mungu yaliyo yake, kama ukiutafsiri kwa ulichoandika wewe, basi angepaswa kusema kinyume chake!
Na ule mfano kuhusu punda aliyetumbukia shimoni, kama ungekuwa wewe ungesema abaki shimoni hadi sabato iishe!

Binafsi nadhani kuna wakati sheria za dini kwa mwenye akili timamu unapaswa kuchanganya na logic yako, kwa sababu kimsingi sheria ya dini sio lazima iwe sheria ya Mungu, na ndio maana tuna dini tofauti tofauti ila Mungu yuko mmoja tu naye aliweka amri zake!
 
wakienda kulalamika kisheria nadhani watasaidiwa na chuo ndio kinamakosa! kama mwanafunzi amekuwa registered kusoma full tym maana yeke ni jumatatu hadi ijumaa na ni wakati wa mchana tu. hata mtihani au vipindi vikiwa usiku ni makosa. kufundiswa jumamosi au jumapili pamoja na kufanya mitihani hizo siku pia ni makosa. ratiba ya masomo yao ndio inayoonyesha mwanafunzi anasoma kwa mtindo gani. kama ratiba yao walikuwa wanafundishwa jumamosi na walikuwa wanaingia darasani basi huo ni utaratibu wa chuo na ni lazima ufuatwe ndio maana walikubali kujiunga na chuo. kama jumamosi walikua wanafanya local arrangement na walimu wao ili wasome na kufanya mitihani basi hiyo inaonyesha kuwa jumamosi sio siku ya masomo. vijana wameonewa na inabidi walalamike. hili tatizo lipo sana katika vyuo vyetu tanzania na wanafunzi ndio wakulaumiwa kwa kuwa hao ndio wanaoukubali hizi local arrangement za vipindi na mitihani baadae mazoea yanakuwa sheria.
 
umenikuna sana

acha kupotosha....
wakatoliki kutokana na sensa yetu tuliyofanya wenyewe bila Khassim za serikali ituhesabu tupo jumla ya waumini milioni 12 Tanzania nzma.
DSC_0005_717ce.JPG
tutafute jambo leo nadhani kuna data
 
mkuu hta chuo kikuu cha sayansi na technolojia mbeya(MUST),kuna wanafunzi walisimamishwa kufanya chuo kisa hawakufanya mtihani siku ya sabato
 
mkuu hta chuo kikuu cha sayansi na technolojia mbeya(MUST),kuna wanafunzi walisimamishwa kufanya chuo kisa hawakufanya mtihani siku ya sabato

ungetujuza kilichofuata ili hawa nao wapate uzoefu Mkuu
 
Nafasi ya Waislamu na katiba mpya Tanzania. Waislamu wanaihitaji siku ya Ijumaa iwe ni siku ya mapumziko ili waweze kupata wasaa wa kushiriki ibada yao kwa kujinafasi zaidi...
 
nenda shule, piga kama mwendawazimu kisha tambaa zako, kasali. Mungu ni mwenye rehema atakusamehe pale ulipokengeuka
lakini unajua kuna dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu?
 
  • Thanks
Reactions: dtj
wakienda kulalamika kisheria nadhani watasaidiwa na chuo ndio kinamakosa! kama mwanafunzi amekuwa registered kusoma full tym maana yeke ni jumatatu hadi ijumaa na ni wakati wa mchana tu. hata mtihani au vipindi vikiwa usiku ni makosa. kufundiswa jumamosi au jumapili pamoja na kufanya mitihani hizo siku pia ni makosa. ratiba ya masomo yao ndio inayoonyesha mwanafunzi anasoma kwa mtindo gani. kama ratiba yao walikuwa wanafundishwa jumamosi na walikuwa wanaingia darasani basi huo ni utaratibu wa chuo na ni lazima ufuatwe ndio maana walikubali kujiunga na chuo. kama jumamosi walikua wanafanya local arrangement na walimu wao ili wasome na kufanya mitihani basi hiyo inaonyesha kuwa jumamosi sio siku ya masomo. vijana wameonewa na inabidi walalamike. hili tatizo lipo sana katika vyuo vyetu tanzania na wanafunzi ndio wakulaumiwa kwa kuwa hao ndio wanaoukubali hizi local arrangement za vipindi na mitihani baadae mazoea yanakuwa sheria.

Labda hapo teku ndio watashnfa lkn SAUT hilo hamna joining instruction imekombaini vitu vyote ikiwamo kukubali kwa baadhi ya mitihani au program nyinginezo za chuo kufanyika jmosi.

Na kama ukubaliani nao wanakwambia nibora urudi kwenu
 
Hicho ni chuo kidogo sana na ni private ambacho kinajali faida zaidi.Wasabato wasipojiunga na chuo hicho kabisa mapato yao yatapungua hivyo baadaye wataamua kurahisisha masharti.Wanachofanya ni mambo yasiyo na busara uhuru wa kuabudu ni muhimu.
 
heri ya happ japokua si haki pia ukiamua kunyooka nao
Labda hapo teku ndio watashnfa lkn SAUT hilo hamna joining instruction imekombaini vitu vyote ikiwamo kukubali kwa baadhi ya mitihani au program nyinginezo za chuo kufanyika jmosi.

Na kama ukubaliani nao wanakwambia nibora urudi kwenu
 
Hicho ni chuo kidogo sana na ni private ambacho kinajali faida zaidi.Wasabato wasipojiunga na chuo hicho kabisa mapato yao yatapungua hivyo baadaye wataamua kurahisisha masharti.Wanachofanya ni mambo yasiyo na busara uhuru wa kuabudu ni muhimu.

hapo umenena
 
nauliza tu,hivi wasabato wanaosoma nje ya nchi katika nchi zisizo na mifungamano ya dini hizi kuu mbili tulizonazo hapa nchini(mf.china, urusi n.k), huwa nao wanagomea mitihani???duuuh....kuna nchi siku za chrismass na eid ni darasani kama kawaida. kwa upande wa Tz mlimani nimeshashuhudia watu wanafanya test siku za chrismass na eid na mhadhiri anakwambia "huo ndio muda pekee ambao niko free" , kwa hyo una hiari uende kwenye test au ubaki na imani yako ya kusherehekea eid au chrismass.....mhh mambo ya imani kaazi kweli kweli!!!
 
lakini unajua kuna dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu?
nadeclare interest kuwa mimi ni mtu wa Kristo, hicho ulichopost nakijua na najua nilipopost nilipost kitu gani. Inawezekana kabisa ukawa unachojua kuwa ni kumkufuru RohoMt. kikawa sicho kabisa, anyway siko hapa kukuelimisha maaana ya kumkufuru Roho Mt.

Ila hao vijana hawajui kilichowapeleka pale. Ingawa kuna mpuuzi mmoja alipost kuwa eti kanisa liko ktk mateso, Mwambieni eande Iran, Kwa WATALIBAN, Kuwait, huko ataona kanisa linavyoteseka. Asituletee upuuzi eti kanisa liko katika mateso kwa sababu ya yy kutofanya mitihani on Saturday kisa hakujianda kufanya paper, anasingizia mateso kwa kanisa
 
Ingawa mjadala huu ni wa muda mrefu kidogo, ila mwanzoni mwa mwezi huu, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilitoa hukumu ambayo inawapa haki wanafunzi kama hawa kuweza kusoma bila haki zao za kuabudu kuingiliwa na serikali au mamlaka zingine. Haki za Binadamu wananchi wa Tanzania wanazohakikishiwa kwenye katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Haki zingine za kimataifa ambazo Tanzania imeridhia kuzikubali, inakataza kuwepo kwa sheria nyingine zozote ambazo zinakinzana na kuzuia raia wa Tanzania kutokuwa huru na kufurahia haki zao za msingi za binadamu ikiwemo ya kutokuzuiwa kupata elimu kwa sababu ya misingi ya dini zao.

Katika mjadala huu ambao umeendelea kwa muda mrefu hapa jukwaani, wengi wametoa maoni tofauti tofauti wakishuku au kupinga haki ya wanafunzi hawa kuendelea na dini na imani zao hasa katika vyuo hivi binafsi ambavyo vina sheria zao ambazo walikubaliana nazo wakati wanaomba kujiunga. Tafadhali soma nakala ya HUKUMU ya Mahakama ya Rufaa maana inaweza kusaidia kupanua upeo wetu wa kuelewa haki wanazopewa wananchi, hasa inapokuja kwa maswala ya uhuru wa dini.

Wengine wametoa changamoto ya maisha binafsi ya wanafunzi hao ambayo huenda yanakinzana na madai yao ya kidini. Ingawa mimi binafsi nakubaliana asilimia 100 na changamoto hii maana kama unadai kuonewa kidini, angalau elekeza maisha yako kikamilifu kwa kufuata maadili ya dini hiyo. Lakini inaposoma hukumu hii, unagundua kwamba "Dini" au "Imani za Kidini" kisheria inapewa tafsiri pana kabisa na tafsiri binafsi za kidini nazo zina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo mbele ya sheria, kinachotakiwa tu ni kwamba ile haki inayodaiwa inadaiwa kwa dhati, katika kipengele tu cha haki hiyo na kwamba dhamiri ya mhanga wa kunyimwa haki hiyo anaamini kwa dhati kabisa kwamba (kwa tafsiri hii), kufanya mtihani siku ya Jumamosi hakuridhiwi na maadili ya imani yake. Kwa hiyo utaona swala la dhamira binafsi ni muhimu katika sheria, na ingawa ni kinyume kabisa kimaadili, lakini mbele ya sheria, wanafunzi hawa bado wana haki ya kikatiba na kisheria kutokufanya mitihani siku ya Jumamosi na kuruhusiwa kuendelea kusoma (labda kwa kufanya mitihani siku nyingine ya wiki) kama dhamiri yao inawahimiza kufanya hivyo hata kama kwenye maeneo mengine ya kidini (mfano kingono kama ilivyoelezwa awali), wanaweza wasiwe makini sana, lakini kinachohesabiwa ni Dhamiri binafsi ya mhusika.

Niwatakie siku njema na wiki njema.
 
Back
Top Bottom