Wanafunzi wa Masjid Badawy ukubwani

Wanafunzi wa Masjid Badawy ukubwani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WANAFUNZI WA MASJID BADAWY UKUBWANI

Tukisema tuandike historia za waliosoma Masjid Badawy kama wanafunzi itabidi tuandike kitabu kizima.

Muhimu ni kuwa wengi wa wanafunzi hawa walikuja kutoa mchango mkubwa katika jamii.

Kuna baadhi nilijuananao kwa karibu sana na wengine kwa mbali lakini tunafahamiana kwani Dar es Salaam ile sote watoto tukijuana.
Allah alijaalia kuwa kila walichokitia mkono hawa wanafunzi wa Masjid Badawy kilifanikiwa.

Naweka hapo chini picha za wanafunzi hawa na maelezo kwa mukhtasari.

1. Ramadhani Madabida ameshika picha ya Kalima alikuwa MC katika chakula cha jioni kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Kiislam Tabora. Mgeni wa heshima katika hafla hii alikuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Shughuli hii ilikuwa New Africa Hotel mwaka wa 1997.

2. Jaji Mkuu Mohamed Chande katikati akiwa na Mussa Kwikima Jaji wa Mahakama Kuu.

3. Ismail Bahdour picha hii tumepiga Muscat mwaka wa 1999 nilikuwa natoka msikitini na yeye anaingia. Ismail kwa jina la utani ''Gigi'' alikuwa na kipaji kikubwa cha kucheza mpira na kufundisha pia. Hili jina la Gigi lilikuwa jina la mchezaji wa Brazil. Ismail alikuwa mtu mcheshi na wa maskhara sana. Siku ile tulipokutana hapo msikitini akawa anamwambia mwenyeji wangu, ''Huyu shemeji yangu rafiki yake yule mkubwa wa mkonge Tanzania nzima (Salum Shamte) amemuoa dada yangu (Maryam).''

4. Maryam Shamte Mtangazaji wa BBC London akimfanyia mahojiano Prof. Lipumba White Rose Hotel, Tanga wakati wa Uchaguzi Mkuu wa vyama vingi mwaka wa 1995.

5. Babu Mwita akikaribisha wageni katika khitma ya kila mwaka ya kuwarehemu masheikh na wanachama wa Saigon Cub waliotangulia mbele ya haki. Mgeni wa heshima likuwa Dr. Ghalib Bilal Makamu wa Rais Zanzibar. Hii ilikuwa khitma ya mwaka wa 2010.

6. Kulia ni Yusuf Zialor na kushoto ni Mohamed Chande wakiwa na Mama Mary Mackeja aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Red Cross, Tanzania. Mohamed Chande na Yusuf Zialor waliitumikia Red Cross katika nafasi za juu. Yusuf Zialor alihusika sana katika kuujenga upya msikti wa Mwinyikheri Akida katika miaka ya 1980. Huu ni msikiti wa zamani kupita yote Kariakoo.

7. Jamil Hizam (Denis Law) wa tatu waliochutama. Jamil alichukua jina la mchezaji mpira wa Manchester United katika miaka ya 1960 wakati huo kijana mdogo akichezea club ya mtaani Young Kenya. Jamil katika picha hiyo ni timu ya East African Cargo Handling Services ikijulikana kama Hydra ambayo ilikuwa na wachezaji wa kiwango cha juu takriban wote wakicheza Yanga, Sunderland na Timu ya Taifa, Picha hiyo ni ya mwanzoni miaka ya 1970. Jamil alichezea pia timu ya Taifa ya Vijana.

Allah warehemu ndugu zetu wote waliotangulia mbele ya haki.
Amin.

Screenshot_20220416-171731_Facebook.jpg
 
Nimekuwa Interested kuifahamu hiyo SAIGON CLUB na member wake, mwenye taarifa zaidi atujuze
 
Nimekuwa Interested kuifahamu hiyo SAIGON CLUB na member wake, mwenye taarifa zaidi atujuze
Ipo kariakoo.
Kijiwe cha watoto wa zamani waliokulia kariakoo.
Baadae the state wakamiliki jina ni sehemu ambayo maamuzi yote ya serikali ikiwemo kupanga viongozi uanzia huko
 
Ipo kariakoo.
Kijiwe cha watoto wa zamani waliokulia kariakoo.
Baadae the state wakamiliki jina ni sehemu ambayo maamuzi yote ya serikali ikiwemo kupanga viongozi uanzia huko

 
Ipo kariakoo.
Kijiwe cha watoto wa zamani waliokulia kariakoo.
Baadae the state wakamiliki jina ni sehemu ambayo maamuzi yote ya serikali ikiwemo kupanga viongozi uanzia huko
Hakika mahala ambapo watoto wote wa mjini kindakindaki wanakijua Mzizima na viunga vyake wanapatikana hapo..
 
Back
Top Bottom