SoC02 Wanafunzi wa mchepuo wa sanaa (Arts) kidato cha tatu na nne wapunguziwe idadi ya mada (topics) katika masomo kama "Biology" na Hisabati (Mathematics)

SoC02 Wanafunzi wa mchepuo wa sanaa (Arts) kidato cha tatu na nne wapunguziwe idadi ya mada (topics) katika masomo kama "Biology" na Hisabati (Mathematics)

Stories of Change - 2022 Competition

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za wakati huu ndugu zangu wa jamiiforums. Mimi Infantry Soldier nipo mzima wa afya.

UTANGULIZI: MUUNDO WA MFUMO WA ELIMU NCHINI TANZANIA KWA UFUPI.

Mfumo wa elimu wa kitaifa kwa hapa Tanzania una ngazi kuu nne. Kwanza miaka saba ya elimu ya msingi ya lazima (kuanzia umri wa miaka sita), pili ni miaka minne katika ngazi ya sekondari, tatu ni miaka miwili ya elimu ya "A Level" na nne ni miaka mitatu mpaka mitano ya elimu ya juu kulingana na taaluma inayosomewa.

images (1).jpeg

(Picha kwa hisani ya tovuti ya Wizara Ya Elimu)

Kuanzia mwaka huu wa 2022, Serikali imeanza kutoa elimu bure kwa ngazi ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote nchi nzima.

Kuingia katika shule ya sekondari kunategemea na mwanafunzi kupata Cheti cha Elimu ya Msingi cha Tanzania kwa kufaulu mtihani wa kitaifa. Kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi yanayoendelea hapa nchini kwa sasa wanafunzi wengi hawajaweza kuendelea na elimu zaidi ya ngazi ya msingi.

images (4).jpeg

(Picha kwa hisani ya tovuti ya Wilaya Ya Kilosa)

Elimu ya sekondari bila malipo ilianzishwa ili kusaidia kushughulikia suala hili. Kwa sasa kiwango cha kujua kusoma na kuandika cha Tanzania, ni cha juu kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

PENDEKEZO LANGU JUU YA KUPUNGUZWA KWA IDADI YA MADA (TOPICS)

Ndugu zangu Watanzania, ninapendekeza wanafunzi wa mchepuo wa sanaa (Arts) kidato cha tatu na nne wapunguziwe idadi ya mada (topics) katika masomo kama "Biology" na Hisabati (Mathematics) yasiyowasaidia kuunda "combination" kidato cha tano.

images (5).jpeg

(Picha kwa hisani ya mtandao wa kituo cha habari cha East African Television)

Mwanafunzi wa mchepuo wa sanaa akipunguziwa mzigo wa topics/mada katika masomo tajwa hapo juu, inampa fursa kubwa sana ya yeye kuelekeza nguvu zake nyingi katika masomo kama Historia, Kiswahili, Geography pamoja na English ambayo ana nafasi kubwa ya kuyatumia katika kuunda "combinations" kama HKL (History, Kiswahili, Language), HGL (History, Geography, Language), HGK (History, Geography, Kiswahili) pamoja na HGE (History, Geography, Economics) pindi afikapo kidato cha tano.

Mwanafunzi wa mchepuo wa sanaa unamfundisha mada za Hisabati kama "Circles and Spheres" pamoja na "Trigonometric Ratios" ili zije zimsaidie wapi na katika nini siku za usoni? Wanasheria maarufu walioko hapa Tanzania kama mzee Mabere Marando au Nimrod Mkono, mada ya somo la biology ya kidato cha tatu kama "Classification of living things" imemsaidia vipi katika kufikia malengo yake ya kitaaluma kwa kiwango cha juu?

mwalimu akiwa darasani.jpg

(Picha kwa hisani ya mtandao)

Ndugu zangu watanzania, sasa umefika wakati wa kufanya mabadiliko ya jumla na makubwa sana katika mitaala pamoja na mifumo yetu ya elimu kama kweli tunataka kuwa na Tanzania imara kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae. Viongozi wetu ni lazima watambue ya kwamba Tanzania ya sasa si sawa na ile ya miaka 20 nyuma.

Tanzania ya mwaka 2002 ambayo mimi Infantry nilihitimu kidato cha nne sio sawa na hii ya mwaka 2022 aliyohitimu mtoto wa dada yangu na wala haitakuwa kama ile ya mwaka 2052 atakapokuwa anahitimu mjukuu wake. Katu hazitakaa zifanane. Jamani tunahitaji kubadilika. "We, seriously, need to change."

Moja kati ya hotuba zake, Rais mstaafu wa Marekani ndugu Barack Hussein Obama aliwahi kusema kwa lugha ya Kiingereza, "as time changes, and so must we" akiwa na maana kwamba, "kadri muda unavyobadilika, ni lazima na sisi tubadilike"

61e798e9d64d3677774663.jpg

(Picha kwa hisani ya tovuti ya Wilaya Ya Kilosa)

Jenga picha mwaka jana ulikuwa una watoto wawili wa kike nyumbani kwako ambao walikuwa wakisoma shule mbili tofauti. Mmoja ni mtoto wa dada yako anayeitwa Zakia na mwingine binti yako wa kuzaa anayejulikana kwa jina la Irene. Katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana wa 2021, Zakia, aliyekuwa akisoma mchepuo wa sanaa alifanikiwa kufaulu masomo ya Biology na Hisabati kwa Alama "A" yote mawili, na kisha kupata alama "B" kwa yale mengine saba (7).

Binti yako Irene ambaye alikuwa anachukua mchepuo wa sayansi, alifanikiwa kupata alama hizo hizo akiwa katika shule tofauti za ndugu yake Zakia.

Unafikiri ni nani atakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kutumia ufaulu wa alama "A" mbili katika masomo ya Biology na Hisabati katika kuunda combination kidato cha tano? Kiuhalisia ni Zakia ndiye atakayetumia Bilogy na Hisabati katika kuunda combinations kama PCB (Physics, Chemistry, Biology), PCM (Physics, Chemistry, Mathematics), PGM (Physics, Geography, Mathematics), CBA (Chemistry, Biology, Agriculture), pamoja na CBN (Chemistry, Biology, Nutrition).

bukimaf1.jpg

(Picha kwa hisani ya mtandao)

Ninajua fika ya kwamba kuna baadhi ya wadau muda sio mrefu watakuja na hoja zao mufilisi na kuanza kuuliza, kwanini kwa masomo ya Biology na Hisabati pekee na sio somo la civics ambalo nalo pia halisaidii katika kuunda combination kidato cha tano?

Kitu ambacho ninapenda kuwakumbusha wadau hao (kama watajitokeza) ni kwamba somo la civics kwa sasa halisaidii katika kuunda combinations kwa wanafunzi wa O Level kwa michepuo yote hata kama akipata alama "A".

Pendekezo la kuunganisha somo la Civics na Historia kuwa moja huu ni mjadala wa siku nyingine utakaohitaji muda na umakini sana katika kuudadavua. Kwa leo ninapenda kuishi hapa. Asanteni sana kwa kusoma.

AMBATANISHO: Mada za Masomo husika kwa kidato cha tatu na nne.

Mada za somo la Hisabati kidato cha tatu

TOPIC 1: Relations
TOPIC 2: Functions
TOPIC 3: Statistics
TOPIC 4: Rates And Variations
TOPIC 5: Sequence And Series
TOPIC 6: Circles
TOPIC 7: The Earth As A Sphere
TOPIC 8: Accounts

Mada za somo la Biology kidato cha tatu.

TOPIC 1: Classification Of Living Things
TOPIC 2: Movement
TOPIC 3: Coordination
TOPIC 4: Excretion
TOPIC 5: Regulation
TOPIC 6: Reproduction

Mada za somo la Hisabati kidato cha nne.

TOPIC 1: COORDINATE GEOMETRY
TOPIC 2: AREA AND PERIMETER
TOPIC 3: THREE DIMENSIONAL FIGURES
TOPIC 4: PROBABILITY
TOPIC 5: TRIGONOMETRY
TOPIC 6: VECTORS
TOPIC 7: MATRICES AND TRANSFORMATION
TOPIC 8: LINEAR PROGRAMMING

Mada za somo la Biology kidato cha nne.

TOPIC 1:GROWTH
TOPIC 2: GENETICS
TOPIC 3: CLASSIFICATION OF LIVING THINGS
TOPIC 4: EVOLUTION
TOPIC 5: HUMAN IMMUNO DEFICIENCY (HIV) ACQUIRED IMMUNO DEFICIENCY SYNDROME (AIDS), AND SEXUAL TRANSMITTED INFECTIONS (STI’s)

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Upvote 29
Tatu Hesabu huchangansha kichwa kwa hawa Ngwini.
Mkuu, kwa hiyo future engineers wanaosoma kidato cha nne wanaisoma hisabati kwa lengo la kuchangamsha akili na sio kuja kuweza kujenga structures bora?
 
Hapa tunazungumzia wake wa Arts kama nada inavyosema, au umesahau?
Mkuu, kama lengo ni kuchangamsha akili kupitia somo la hisabati sasa hayo madaraja ya As na Bs ni ya kazi gani?

Brother, hoja yako bado ni dhaifu sana ndio maana unashindwa kuitetea
 
Kwa kifupi masomo hayo ni muhimu kwa watoto. Mengine achana nayo.
Hakika masomo haya ni muhimu lakini kamwe siwezi kuacha kuwapigania wadogo zangu haki yao ya kupunguziwa mzigo wa mada zisizo na tija katika mustakabali wa maisha yao ya kielimu.
 
Asante sana Askari wa nchi kavu. Mada nzuri na nimeshakupigia kura.

Hata hivyo nina angalizo kidogo.

Kuna sababu wanafunzi wote wanalazimishwa kusoma masomo haya.

1. Hesabu ni somo la muhimu sana na kuna uwezekano mkubwa kuwa huko mbele ya safari watakutana nalo kwa namna moja au nyingine. Kuna wengine watasoma HGE au EGM kidato cha 6. Bila msingi mzuri wa hesabu wanaweza wakatetereka. Hata kwenye Isimu kuna Mathematical na Computational Linguistics. Bila msingi mzuri wa hesabu ni majanga. Kwa maoni yangu somo la Hisabati halikwepeki!

2. Biology ni somo linalohusu viumbe na maingiliano yao na mazingira. Ni somo la muhimu linalomfanya binadamu ajitambue yeye mwenyewe alivyo pamoja na mahusiano yake na viumbe hai wengine na mazingira yao.

Hata hivyo mada yako inachokonoa swali la msingi zaidi na la muhimu pengine kuliko yote. Lengo hasa la hii elimu yetu ni nini? Ni ajira kwa waipatayo? Ni kuwatajirisha? Ni kuwakaramsha waipatayo na kuwafanya kuwa na uelewa wa kiwango fulani wa jinsi mifumo inayoendesha maisha yao inavyofanya kazi kimwingiliano katika mazingira waliyomo?

Ati; lengo hasa la hii elimu yetu ni nini?

Kila la heri katika shindano hili mkuu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Ulimakafu
 
Back
Top Bottom