Mwaka jana, chuo kilitangaza kuwa hakukuwa na grace period, hivyo muda wa masomo unapomalizika, mwanafunzi alitakiwa kulipia extension ili kuendelea na masomo.
Hata hivyo, mwaka huu chuo kimetangaza kuwa grace period ipo kwa muda wa miezi mitatu. Changamoto ni kwamba sisi tuliolipia extension kwa kipindi hicho cha miezi mitatu hatujarudishiwa fedha zetu.
Tunapokwenda kuulizia suala hili, tunaambiwa kuwa utaratibu wa kurejesha fedha hizo haupo.
Tunaomba suala hili lifanyiwe kazi na sauti yetu isikike, kwani tunaamini tunastahili kupata ufafanuzi na haki zetu kuhusu malipo tuliyofanya.