KERO Wanafunzi wa Uandishi tunalazimika kulika Ithibati mara mbili kwa JAB. Tunaomba utaratibu huu uangaliwe

KERO Wanafunzi wa Uandishi tunalazimika kulika Ithibati mara mbili kwa JAB. Tunaomba utaratibu huu uangaliwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Naomba kuwasilisha kero yangu kuhusu utaratibu wa utoaji wa ithibati kwa wanafunzi wanaohitimu shahada ya Mass Communication mwaka huu.

Kwa sasa, hatuwezi kufanya kazi bila kuwa na ithibati kutoka JAB. Hata hivyo, ithibati ya awali inayotolewa ina muda wa miezi mitatu pekee, ikilenga wanafunzi wanaokwenda kufanya mafunzo kwa vitendo (field).

Baada ya kumaliza mafunzo hayo, tunalazimika kujisajili tena ili kupata ithibati nyingine kwa gharama ya shilingi 50,000, ilhali ithibati ya kwanza hugharimu shilingi 20,000. Hii ina maana kwamba mwanafunzi analazimika kulipia ithibati mara mbili ndani ya kipindi kifupi.

Tunaomba mamlaka husika ziangalie upya utaratibu huu kwa kuzingatia hali halisi ya kiuchumi ya wahitimu wengi. Si rahisi kumudu gharama hizi mara mbili, ilhali hatuwezi kufanya kazi bila kuwa na ithibati hiyo. Tunaiomba JAB na wadau husika kutafuta suluhisho litakalopunguza mzigo huu kwa wahitimu wapya.
 
Soko la ajira lenyewe ni la mchongo, halafu mnaletewa tena tozo za mchongo!
 
Back
Top Bottom