University of Dodoma (UDOM)
Public Institution
- Feb 24, 2024
- 50
- 55
Arusha, 28 Machi, 2026
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeibuka mshindi wa Kwanza katika mashindano ya Girls in ICT Hackathon 2026 baada ya wanafunzi wake kushiriki kubuni mfumo wa kuhakiki taarifa kwa kutumia Akili Unde (AI) unaoitwa “Hakiki Scanner.”
Timu hiyo iliwahusisha wanafunzi wawili wa UDOM kwa kushirikiana na wenzao kutoka UDSM na MUST, na kufanikiwa kushinda makundi mengine kutoka vyuo mbalimbali nchini.
Mashindano hayo yalihusisha vyuo mbalimbali ikiwemo UDOM, UDSM, Chuo cha Takwimu, IFM, DIT, NIT, ARDHI, IAA (Arusha), Arusha Technical College, SUZA (Zanzibar), IITM (Zanzibar), MUST pamoja na RUCU.
Mashindano yalitanguliwa na mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na TCRA, UCSAF na ICTC, yakilenga kuwajengea wasichana uwezo wa kutumia AI kutatua changamoto za kijamii.
Pongezi kwa wanafunzi wetu Bi. Mercy Mwasakilali na Bi. Tausi Amiri, kwa kuiwakilisha vyema UDOM.
Kaulimbiu ya mwaka 2026 ni:
“Akili Unde kwa Maendeleo: Wasichana Wakibadilisha Mustakabali wa Kidijitali.”