A
Anonymous
Guest
Sisi wanafunzi wa VETA Mpanda, kuanzia mwezi wa tano tunasubiri kufanya mtihani wa PSV na HGV. Tuliambiwa mfumo umebadilika na tunapaswa kusubiri kukamilika kwa usajili kwenye mfumo mpya kwa ajili ya mtihani, lakini mpaka sasa tunapewa taarifa ambazo hazina hitimisho.
Tunaomba msaada wa kulifuatilia suala hili kwa sababu VETA ndio watendaji wakuu na wanaweza kulifuatilia na kuwezesha mitihani kufanyika. Kwa upande wa kozi za udereva wa HGV na PSV VETA Mpanda, kuna changamoto katika kushughulikia suala la mitihani na vyeti. Kuna mafunzo yaliratibiwa Sumbawanga tangu mwezi wa nne, lakini mpaka leo suala la vyeti bado ni changamoto.
Tunaambiwa usajili unasumbua kukamilika, hivyo tuendelee kusubiri. Tunajiuliza, kama wao ndio watendaji, kwa nini wasilishughulikie suala hili ili mitihani ifanyike? Toka mwezi wa tano mpaka sasa tunaambiwa ni tatizo la mfumo wa usajili na tunaendelea kusubiri, bila kujua tutasubiri mpaka lini, wakati tumelipa ada.
VETA nyingine zinaendelea kudahili wanafunzi na taratibu zinakamilika kwa wakati, huku wanafunzi wakifanya mitihani na kupata vyeti kama kawaida. Sisi kama wanafunzi wa kozi hizi za udereva tunaomba msaada ili suala hili lifuatiliwe na tupatiwe suluhisho.