Wanafunzi wachoma bweni la shule kisa mechi ya Man United Vs Liverpool

Wanafunzi wachoma bweni la shule kisa mechi ya Man United Vs Liverpool

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wavulana wanne wa shule nchini Kenya wanashikiliwa katika mahabusu ya polisi kwa kulichoma moto bweni la shule yao, baada ya kuripotiwa kunyimwa ruhusu ya kutazama mechi kati ya Liverpool na Manchester United, umeripoti wavuti wa Daily Nation nchini humo.

Lilimnukuu mkuu wa polisi wa eneo akisema kuwa wanafunzi hao walikuwa miongoni mwa wengine 14 wanohojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Wanafunzi hao wanne wanaosoma katika shule ya sekondari ya Dr Krapf iliyopo katika eneo la pwani ya Kenya la Kilifi watashitakiwa kwa kosa la kuchoma moto kwa makusudi bweni siku ya Jumatano.

Wanafunzi shuleni wanaruhusiwa tu kutazama televisheni Jumamosi, alisema kamanda wa polisi wa Rabai Fredrick Abuga katika mazungumzo na wavuti wa Daily Nation.

Shule yao kwa sasa imefungwa kufuatia tukio hilo.
 
1635333574665.png
 
Back
Top Bottom