Wanafunzi walioandika barua kuacha shule kisa ugumu wa maisha wapata ufadhili

Wanafunzi walioandika barua kuacha shule kisa ugumu wa maisha wapata ufadhili

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza, ambao kila mmoja aliacha shule ili kufanya shughuli za kujiingizia kipato kusaidia wazazi wao, wamepata ufadhili wa kuendelea na masomo yao katika Shule ya Sekondari ya Ocean iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mtwara.

Mmoja kati yao ni Taufiq Hamis (15), mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Msimbati ambaye hivi karibuni alizua gumzo katika mitandao ya kijamii, baada ya kuandika barua kwa mkuu wake wa shule, akimweleza azma yake ya kuacha shule ili akafanye shughuli za uvuvi akilenga kusaidia majukumu ya nyumbani.

Taufiq aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona wazazi wake wameshindwa kumtimizia mahitaji yake ya shule na hali mbaya ya kiuchumi nyumbani kwao iliyosababisha awe anakosa chakula mara kadhaa.

Mwanafunzi mwingine, Issa Abdallah (15), yeye alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Mbekenyela, lakini aliacha masomo na kwenda kufanya shughuli za uchimbaji wa madini.

Meneja wa Shule ya Ocean, Juma Nchia alieleza kuwa taasisi mbili za Kalamu Education Foundation (KEF) pamoja na Mar'wa Education Centre inayomiliki Shule ya Ocean kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali, wameamua kuwachukua wanafunzi hao na kuwahamishia katika Shule ya Sekondari ya Ocean ya Mtwara.

Nchia alisema kuwa Taasisi ya KEF ambayo ina mpango wake ujulikanao kama Hakuna Kufeli' ambayo inasaidia elimu kwa watoto kutoka sehemu mbalimbali katika mikoa ya Kusini na Pwani, imeamua kuchukua wanafunzi hao ili wakue katika mazingira ya shuleni na kuwaondolea adha za kifamilia.

Taasisi ya elimu ya Kalamu itakuwa ikiwasiliana na wadau mbalimbali wa elimu na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi hao kisha kutoa ripoti".

Taasisi ya elimu ya Kalamu itakuwa ikiwasiliana Sekondari Ocean na wadau mbalimbali wa elimu na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi hao kisha kutoa ripoti," alisema na kuongeza kuwa taasisi ya Marwa Islamic Institute inayomiliki shule hiyo, itakua ikichangia ada za wanafunzi hao.

"Tunaomba wafadhili wajitokeze kwa wingi kusaidia watoto, elimu ni bure lakini bado watoto wanahitaji vifaa, sare na mahitaji mengine muhimu pia," alisema Nchia.

Issa alisema kuwa alifanya shughuli za uchimbaji madini kwa muda wa wiki mbili na kufanikiwa kupata Sh40,000 ambazo aliwapatia wazazi wake kwa ajili ya mahitaji muhimu ya nyumbani.

Hata hivyo, alitoka kwenye shughuli hizo baada ya mmoja wa walimu kumuona na kumshauri kurudi shuleni na hatimaye kupata wafadhili waliompeleka katika shule ya Ocean.


Source: Mwananchi
 
Wasome sasa, hakuna kisingizio hapo tena 😅
 
Back
Top Bottom