"Ikitokea bei ya bidhaa imeshuka sana, uchumi wa nchi utakuwa umepanda au umeshuka? Na kwa nini?" Kwa mfano ikitokea soda imeshuka bei kutoka Tsh 700/- had Tsh 150/-.
Uchumi wa nchi haupimwi kwa bei, unapimwa kwa uzalishaji ulio na ufanisi. Kwa mfano, unaweza kuwa na bei kubwa sana za mahindi, kitu ambacho kinaweza kukufanya ufikiri kitasaidia kukuza uchumi kwa sababu wakulima wa mahindi watapata bei nzuri kwa mazao yao, lakini kama wakulima hawajazalisha na bei kubwa hiyo inatokana na ukame wa mahindi, bei kubwa haisaidii..
Na vile vile, unaweza kuwa na mahindi yenye bei ndogo sana, kwa sababu mvua nyingi na uzalishaji umepita mahitaji ya soko. Hapo pia una tatizo kwa sababu wakulima wametumia resources nyingi sana (muda, pembejeo, nguvu etc) lakini hawapati a good return on investment kutokana na deflation. deflation ambayo inaweza hata kuwa dis-incentivize kulima tena.
Swali linaulizwa kwa msingi wa makosa wa kufikiri kwamba uchumi wa nchi unashuka au kupanda kwa sababu ya bei, bila ya kuangalia uzalishaji.
Kama unataka kwenda na ceteris paribus, itabidi uangalie bidhaa inatengenezwa wapi? Nje au ndani ya nchi? Consumption yake ikoje nje na ndani ya nchi?
Kuongelea bei bila demand ni kama kumuhesabu window shopper kama mnunuzi. Kwa anayejua uchumi hakuna demand kama hakuna purchasing power. Kuna mengi sana ambayo muulizaji wa swali inabidi ayazingatie.
Kwenye macro economics kuna sentiments kwamba inflation is bad and the opposite (deflation) is good for the economy.This is not always true, the devil is in the details.
Uchumi wa Japan sasa hivi na kwa miaka kadhaa tatizo lake si inflation, ni deflation. Mpaka Shinzo Abe anaonekana messiah kwa ku adopt Keynessian rescues.
To the extent that producers wanakuwa discouraged to produce.
Kwa nini tu produce wakati tunajua bei zinashuka tu?