msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Zaidi ya wanafunzi 600 katika shule za msingi mbili za Kayenze na Chasubi zilizopo kata ya Kayenze halmashauri ya Ilemela wanasoma wakiwa chini kutokana na ukosefu wa madawati.
Aidha, changamoto nyingine inayotajwa katika shule zote mbili ni upungufu wa walimu ambapo jumla ya wanafunzi ni 3100 lakini walimu waliopo ni 25 pekee, hali inayopelekea ufundishaji kuwa mgumu na wanafunzi kukosa baadhi ya masomo kutokana na upungufu wa walimu uliopo katika shule zote mbili.
Wakati hayo yakijiri, huko Muleba nako hali si shwari. Ambapo shule ya msingi Burungura yenye wanafunzi 868 na walimu watano, inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na uhaba wa walimu hususani wa kike hali inayosababisha utoro kwa wanafunzi wa kike kwa kushindwa kuhudhuria masomo yao wakati wa hedhi.
Credit to ITV-Tanzania