Lukwangule,
Jina hili Lukwangile huliona ktk fani ya waandishi wa habari ( unaweza kuwa muandishi,mtangazaji, blogger au photo journalist), na kama ni kweli ni hivyo, mchango wako hapo juu unazidisha hoja kuwa waandishi wa Tanzania sio makini ktk kazi zao.
Mchango wako Lukwangule unaufanya utetezi wako ktk hoja hii ya Mkapa kuwaponda ionekane ina uzito na haipaswi kushambuliwa tu kwa vile Mzee wa Uwazi ametoa maoni yake, Mkapa aliwahi kuwa mhariri Daily News na gazeti hilo lilijijengea jina ndani ya Tanzania, Afrika, Ulaya na Marekani na kutoa waandishi kama kina Tom Sithole, Ulimwengu Godfrey Mwakikagile n.k.
Mimi bado namuunga mkono Mkapa kwa kauli yake, maana mwandishi wa sasa wa Tanzania kazi yao kwenda ukumbi wa maelezo na kuandika kile wanachoambiwa na walioitisha mkutano. Hakuna maswali ya kutaka ufafanuzi wala kufuatilia ktk intaneti,JF n.k kuona kama yale walioelezwa yana mantiki.
Mfano mpaka leo hii sijasoma gazeti lolote lililotoa wasifu wa viongozi wa CCJ wametokea wapi, wameishaifanyia nini jamii kabla ya kuingia ktk siasa n.k, huu ni mfano hai kwa kipindi hiki kuwa waandishi kazi yao ni kutafuniwa habari na sio kutafuta habari zenye kutuliza kiu ya wasomaji.
Hii ni changamoto kubwa kwa waandishi wa habari. Bw.Rioba ktk makala yake ktk gazeti la Raiamwema wiki hii 24/03/2010 anasema Mkapa amefanya kazi kubwa ktk kipindi chake kuhakikisha kwa vitendo vyuo vikuu mbalimbali Tanzania vimeanzisha kozi za ngazi ya shahada na stashahada ya uandishi wa habari na mawasiliano.
Pia hata ktk webusaiti ya
www.bbcswahili.com kuna sehemu ya kozi ya uandishi wa habari chini ya kichwa cha habari Chuo Cha Habari BBCSWAHILI London ambapo mtangazaji wa BBC London idhaa ya kiswahili anaelezea vipi unaweza kuwa muandishi/mtangazaji mzuri.
Hivyo tunategemea kuona kiwango cha uandishi wa habari kikizidi kwenda juu na sio kurudi nyuma kama sasa.