Wanahabari, Kikwete aliwaambia wanakula rushwa, kimya; Mkapa kasema.., kelele!!!

Viongozi wa Tanzania nao hawapo wazi katika uongozi na kuwasilisha takwimu na mambo yanavyokwenda kwenye idara za serikali, waandishi nao wengi wao ni vilaza. Utakuta mtu huyo huyo mmoja anaripoti michezo, huyo huyo mambo ya uchumi, huyo huyo mambo ya udaku... huyo huyo siasa yaani professional hakuna kwa kweli.
 
Wakati yeye anaona tatizo kwa waandishi, waandishi wanaona tatizo kwenye uongozi! Na kati ya hao wawili mzigo mkubwa wa mabadiliko ya nchi yako kwa viongozi!

Tatizo la Mkapa na media lilikuja pale tuu mwandishi mmoja alipomuuliza kama ni kweli naye alihusika na yale mabilioni yaliyosemwa na Mrema. Tangu siku hiyo , hakuita tena press conference.
 
Waandshi wetu wa habari wamenishangaza kweli kwa hatua yao ya kukaa kimya dhidi ya tuhuma kuwa wanakula rushwa kwa ujumla wao tuhuma zilizotolewa na raisi wa Tanzania ndugu Kikwete. Yaani huwezi amini zaidi ya mzee Ndimara Tegambwage kunung'unika kidogo, wengine woote wamekaa kimya kama vile hawakusika kilichosemwa juu yao!
Sasa cha ajabu, Mzee Mkapa nae karudia hayo hayo akiwa nchi jirani ya Kenya ila yeye katumia lugha ya kiungwana kidogo kwa kusema waandishi wa Tanzania hwana uzalendo na hawana uelewa wa mambo kabisa, yaani kwa mambo ambayo hata wanayauliza?!..........Lolo! waandishi wamechachamaa, sasa wanampelekea mashambulizi makali Mkapa...
Hii inakuwaje?... waandishi wa Tanzania wanamuogapa JK? au wanasubiri nae astaafu?, au ni kweli kawapa rushwa ili wasimuandame?
Mzizi wa mbuyu,

"Waandishi wa Tanzania hawana Uzalendo na hawana Uwelewa wa mambo kabisa........."(Mkapa)
Katika setesi hiyo ya Mkapa kuna maneno mawili hakupaswa kuyatumia; "UZALENDO" kwa sababu yeye mwenyewe umemshinda!! alipewa nafasi na Fursa ya kuonyesha uzalendo wake, alichofanya wote tunakijua. mtu wa matendo na tabia kama yake hastahili kumvua mwengine uzalendo. "UELEWA" Mkapa angekuwa mwelewa wala asingetamka hayo dhidi ya Wanafani wenzie alikuwa na fursa ya kuwajenga na kutujengea Media nzuri akiw Rais atokanae na fani hiyo ya habari. Nadhani wanahabari wana haki ya kumsakama kwa kuwatia shutuma kwa sifa mbaya juu ya Uzalendo na Uelewa vitu ambavyo yeye Mkapa alivipoteza zamani. Ingefaa huyu Bw. apumzike kuzungumza hadharani, bila shaka ule "Uvivu wa kufikiri na Wivu wa Kike" vinamrudia mwenyewe.
 
Mkapa anapenda sana kutukana watanzania, lakini kitu nilichokiona katika ile clip ni kwamba ameexpose uwezo wake jinsi ulivyo mdogo. Na ndio maana Chissano alikuwa akimwangalia kwa mshangao. Anasema alikuwa afanyi press conference kwa sababu alikuwa anataka waandishi ambao wanajua ishu inayozungumziwa-well versed on the issue to paraphrase him. Sasa swali ninalojiuliza utajuaje kama waandishi wanajua ishu bila ya kuwapa nafasi ya kuzungumza.
 
There is NEITHER permanent enemy NOR permanent FRIEND. hata enzi zile awamu ya TATUzaangesema Mwinyi angekiona cha mtema kuni na Angesema Mkapa wangecheka aahaaa ahaaa Mheshimiwa bwana AACHI UTANI siku zote mcheshi anatuthamini na anapenda kututania sisi wana habari SIJUI KWA VILE NA YEYE ALIKUWA MWANAHABARI????
 
c mnakumbuka ile katuni ya kenya ya waandishi wakilamba miguu ya kikwete ndio haya kwa sasa waandishi wa habari walipofikia ni kama kosa la jinai kumuandama kikwete na taaluma yako ni kama itaisha so wanaimba kama kasuku tu! waandishi nchi ii ni wanafiki cjapat ona, habari inaandikwa sio kwa uhalisia wake bali kwa kua muandukwa ni nani, habari yoyote inayomuhusu mkapa wanaiandika kwa matusi na kejeli chungu mzima lakini kwa uyu wa sasa ni mapambio kama kasuku vile
 
Wakati fulani unawaangalia watu unabaki unajiuliza hivi kweli wanajua wanachokisema? Halafu unaanza kufanya udadavuzi wa kawaida kabisa nani anasema na anajua nini mwisho unagundua anayesema kwanza hajui anachosema hajakifanyia utafiti an mwishoni anazungumza pumba zaidi kuliko ilivyo.

Kikwete alikuwa na haki ya kuzungumza kwa kuwa incident za waandishi kudakwa na watu wa pccb inaongezeka na huyu wa juzi juzi si wa kwanza. Pili kama rais ana haki ya kusema kwamba lipo tatizo na lazima watu waliangalie.

Huwezi kujiita forth estate kama wewe mwenyewe unanuka uchafu unaotakiwa kuuangalia. Ni vyema ukatambua daima dumu kwamba samaki hajitambui kama amelowa mpaka umtoe nje ya maji na ashindwe kupumua. Naam sisemi kwasababu watu wanasema unajitetea na ukiliza wako. la hasha kuna shida kubwa ya wewe kukwepa waandishi na ndio maana waandishi si tu wanapinga sheria zilizopo ambazo zimetiliwa mkazo na Mkapa bali wanataka uwazi katika masuala ya umma masuala ambayo watu wengine hawapo tayari kusema. Kuna uhuru mkubwa wa kuandika mambo ya serikali ukweli uwongo na udadisi lakini hali hii imewezeshwa na hali ya kuvumilia inayoendeshwa na awamu ya nne Mkapa alikuwa anafungia magazeti na alipobanwa zaidi akamtangaza mtu fulani si raia wa nchi hii. Huwezi kabisa kumlinganiosha kikwete na Mkapa.Kikwete anabanwa anajitetea na anawaita watu kujieleza na yeye kufafanua. Hotuba gani zenye uadilifu aliziotaja anayejidai ni muadilifu. hakuna anayemshambulia mkapa, lakini unaweza kuona ni namga kwa namna tofauti kama ilivyo katika nchi zinazokomaa demokrasia vyombo vya habari vinavyotumikia umma.

Unaweza kuingia kwa JF na kutandaza mcharazo wako uwe mzuri au mbaya kwa kuwa serikali haina mpango wa kujam mawasiliano China kama hawakutaki wanajua namna ya kukufanyia na hutaonekana kwa wachina na nchi nyingi zenye ubabazazi kama aliokuwa anaufanya Mkapa wa kukataa kuzungumza na vyombo vya habari habari zao hazipo nje tazama nchi mbili tajiri za Asia zinavyofanya.Kitu ambacho waandishi wanataka mtu huyu akubali ukweli ni kwamba yeye mwenyewe si muadilifu hivyo nma kujua kwake kiingereza kunaonyesha pia kasoro yake ya ubinafsi.

Hii si mara ya kwanza kusema kwamba watanzania haaandishi hawana chochote na mara zote amejibiwa kwamba anachosema si sahihi waandishi wa kimataifa wanamuuzliza wale wanayodhani yanafaa kuelezwa kimataifa na sisi tunauliza ubora wa utawala wake kwani maepa yote yalianzia kwake kama anabisha tuianze kudadavua rekodi juu ya utawala wa Kikwete umetengeneza dhambi ngapi zakwake na yeye ametengeneza dhambi ngapi ambazo leo ndio tunapam,bana nazo na kelele kibao.

Waandishi kama wengine na hata wewe unayesema wapo kilaza ni watu wenye taaluma zao, Mkapa hakuwa mwandishi wa habari alichukuliwa kwenye wadhifa na huo wadhifa ndio unamfanya kuwa na kibri. sasa suala la kuspecialize ni kukua si kwa taaluma bali kwa sekta zote za huduma. Huwezi kuspecialize katika mazingira ya sasa ambapo wataalamu wa mawasiliano bado , kuna level ya kufikia, ikifika kutoka katika sekta husika watatoka watu ambaow atahitaji kuepewa mweleko kidogo nao wataweza kutumiwa kuhabarisha watu.

Nisemeje sasa je mtu ana haki ya kumtukana mtu ambaye alitakiwa kumsaidia kufikia level fulani hao wa nje wamemsaidiaje? Labda tuseme ukweli kuwa hawajamsaidia kitu zaidi ya kmujenga image yake kama mtu bomba lakini ni yeye aliyelianzisha la rada, ndege ya rais ambayo haina maana na Kiwira na yeye ndiye aliyeyaanzisha ya EPA, na watu wanahaki ya kuzungumza kwamba hakufanya vyema kuwakimbia waandishi wa nyumbani. Sawa kutokana na kutengeneza image yake amekuwa ndani ya bill gate it is okay lakini ukweli unabaki yeye ni mbinafsi na kibri chake ndicho hicho kinamfanya kudharau kila mtu labda huko Lushoto ndiko ambako hajaanza kudharau.
 
Mzizi wa mbuyu,

"Waandishi wa Tanzania hawana Uzalendo na hawana Uwelewa wa mambo kabisa........."(Mkapa)
Katika setesi hiyo ya Mkapa kuna maneno mawili hakupaswa kuyatumia; "UZALENDO" kwa sababu yeye mwenyewe umemshinda!! alipewa nafasi na Fursa ya kuonyesha uzalendo wake, alichofanya wote tunakijua. mtu wa matendo na tabia kama yake hastahili kumvua mwengine uzalendo. "UELEWA" Mkapa angekuwa mwelewa wala asingetamka hayo dhidi ya Wanafani wenzie alikuwa na fursa ya kuwajenga na kutujengea Media nzuri akiw Rais atokanae na fani hiyo ya habari. Nadhani wanahabari wana haki ya kumsakama kwa kuwatia shutuma kwa sifa mbaya juu ya Uzalendo na Uelewa vitu ambavyo yeye Mkapa alivipoteza zamani. Ingefaa huyu Bw. apumzike kuzungumza hadharani, bila shaka ule "Uvivu wa kufikiri na Wivu wa Kike" vinamrudia mwenyewe.

Na Kikwete kusema waandishi wa Tanzania wanakula rushwa, katumia maneno mazuri?
 
Mkapa anapenda sana kutukana watanzania, lakini kitu nilichokiona katika ile clip ni kwamba ameexpose uwezo wake jinsi ulivyo mdogo. Na ndio maana Chissano alikuwa akimwangalia kwa mshangao. Anasema alikuwa afanyi press conference kwa sababu alikuwa anataka waandishi ambao wanajua ishu inayozungumziwa-well versed on the issue to paraphrase him. Sasa swali ninalojiuliza utajuaje kama waandishi wanajua ishu bila ya kuwapa nafasi ya kuzungumza.

Mkuu ungerudia kusoma nilichoandika, inawezekana unachosema ni kweli.
Lakini je, Kikwete pia kasema waandishi Tanzania wanakula rushwa yeye yuko sahihi? mbona hasakamwi? anasakamwa Mkapa tuuuuu??!!
 
Wakati fulani unawaangalia watu unabaki unajiuliza hivi kweli wanajua wanachokisema? Halafu unaanza kufanya udadavuzi wa kawaida kabisa nani anasema na anajua nini mwisho unagundua anayesema kwanza hajui anachosema hajakifanyia utafiti an mwishoni anazungumza pumba zaidi kuliko ilivyo.

Kikwete alikuwa na haki ya kuzungumza kwa kuwa incident za waandishi kudakwa na watu wa pccb inaongezeka na huyu wa juzi juzi si wa kwanza. Pili kama rais ana haki ya kusema kwamba lipo tatizo na lazima watu waliangalie.

Huwezi kujiita forth estate kama wewe mwenyewe unanuka uchafu unaotakiwa kuuangalia. Ni vyema ukatambua daima dumu kwamba samaki hajitambui kama amelowa mpaka umtoe nje ya maji na ashindwe kupumua. Naam sisemi kwasababu watu wanasema unajitetea na ukiliza wako. la hasha kuna shida kubwa ya wewe kukwepa waandishi na ndio maana waandishi si tu wanapinga sheria zilizopo ambazo zimetiliwa mkazo na Mkapa bali wanataka uwazi katika masuala ya umma masuala ambayo watu wengine hawapo tayari kusema. Kuna uhuru mkubwa wa kuandika mambo ya serikali ukweli uwongo na udadisi lakini hali hii imewezeshwa na hali ya kuvumilia inayoendeshwa na awamu ya nne Mkapa alikuwa anafungia magazeti na alipobanwa zaidi akamtangaza mtu fulani si raia wa nchi hii. Huwezi kabisa kumlinganiosha kikwete na Mkapa.Kikwete anabanwa anajitetea na anawaita watu kujieleza na yeye kufafanua. Hotuba gani zenye uadilifu aliziotaja anayejidai ni muadilifu. hakuna anayemshambulia mkapa, lakini unaweza kuona ni namga kwa namna tofauti kama ilivyo katika nchi zinazokomaa demokrasia vyombo vya habari vinavyotumikia umma.

Unaweza kuingia kwa JF na kutandaza mcharazo wako uwe mzuri au mbaya kwa kuwa serikali haina mpango wa kujam mawasiliano China kama hawakutaki wanajua namna ya kukufanyia na hutaonekana kwa wachina na nchi nyingi zenye ubabazazi kama aliokuwa anaufanya Mkapa wa kukataa kuzungumza na vyombo vya habari habari zao hazipo nje tazama nchi mbili tajiri za Asia zinavyofanya.Kitu ambacho waandishi wanataka mtu huyu akubali ukweli ni kwamba yeye mwenyewe si muadilifu hivyo nma kujua kwake kiingereza kunaonyesha pia kasoro yake ya ubinafsi.

Hii si mara ya kwanza kusema kwamba watanzania haaandishi hawana chochote na mara zote amejibiwa kwamba anachosema si sahihi waandishi wa kimataifa wanamuuzliza wale wanayodhani yanafaa kuelezwa kimataifa na sisi tunauliza ubora wa utawala wake kwani maepa yote yalianzia kwake kama anabisha tuianze kudadavua rekodi juu ya utawala wa Kikwete umetengeneza dhambi ngapi zakwake na yeye ametengeneza dhambi ngapi ambazo leo ndio tunapam,bana nazo na kelele kibao.

Waandishi kama wengine na hata wewe unayesema wapo kilaza ni watu wenye taaluma zao, Mkapa hakuwa mwandishi wa habari alichukuliwa kwenye wadhifa na huo wadhifa ndio unamfanya kuwa na kibri. sasa suala la kuspecialize ni kukua si kwa taaluma bali kwa sekta zote za huduma. Huwezi kuspecialize katika mazingira ya sasa ambapo wataalamu wa mawasiliano bado , kuna level ya kufikia, ikifika kutoka katika sekta husika watatoka watu ambaow atahitaji kuepewa mweleko kidogo nao wataweza kutumiwa kuhabarisha watu.

Nisemeje sasa je mtu ana haki ya kumtukana mtu ambaye alitakiwa kumsaidia kufikia level fulani hao wa nje wamemsaidiaje? Labda tuseme ukweli kuwa hawajamsaidia kitu zaidi ya kmujenga image yake kama mtu bomba lakini ni yeye aliyelianzisha la rada, ndege ya rais ambayo haina maana na Kiwira na yeye ndiye aliyeyaanzisha ya EPA, na watu wanahaki ya kuzungumza kwamba hakufanya vyema kuwakimbia waandishi wa nyumbani. Sawa kutokana na kutengeneza image yake amekuwa ndani ya bill gate it is okay lakini ukweli unabaki yeye ni mbinafsi na kibri chake ndicho hicho kinamfanya kudharau kila mtu labda huko Lushoto ndiko ambako hajaanza kudharau.

Pole sana, lakini kama wakubwa wanasema waandishi wameoza siyo bure jiangalieni....wale hawakurupuki huenda kuna mtu amewapa mafaili yenu..hivyo badala ya kutunisha vifua vyenu jisafisheni hamjachelewa sana..
 
Lukwangule,

Jina hili Lukwangile huliona ktk fani ya waandishi wa habari ( unaweza kuwa muandishi,mtangazaji, blogger au photo journalist), na kama ni kweli ni hivyo, mchango wako hapo juu unazidisha hoja kuwa waandishi wa Tanzania sio makini ktk kazi zao.

Mchango wako Lukwangule unaufanya utetezi wako ktk hoja hii ya Mkapa kuwaponda ionekane ina uzito na haipaswi kushambuliwa tu kwa vile Mzee wa Uwazi ametoa maoni yake, Mkapa aliwahi kuwa mhariri Daily News na gazeti hilo lilijijengea jina ndani ya Tanzania, Afrika, Ulaya na Marekani na kutoa waandishi kama kina Tom Sithole, Ulimwengu Godfrey Mwakikagile n.k.

Mimi bado namuunga mkono Mkapa kwa kauli yake, maana mwandishi wa sasa wa Tanzania kazi yao kwenda ukumbi wa maelezo na kuandika kile wanachoambiwa na walioitisha mkutano. Hakuna maswali ya kutaka ufafanuzi wala kufuatilia ktk intaneti,JF n.k kuona kama yale walioelezwa yana mantiki.

Mfano mpaka leo hii sijasoma gazeti lolote lililotoa wasifu wa viongozi wa CCJ wametokea wapi, wameishaifanyia nini jamii kabla ya kuingia ktk siasa n.k, huu ni mfano hai kwa kipindi hiki kuwa waandishi kazi yao ni kutafuniwa habari na sio kutafuta habari zenye kutuliza kiu ya wasomaji.

Hii ni changamoto kubwa kwa waandishi wa habari. Bw.Rioba ktk makala yake ktk gazeti la Raiamwema wiki hii 24/03/2010 anasema Mkapa amefanya kazi kubwa ktk kipindi chake kuhakikisha kwa vitendo vyuo vikuu mbalimbali Tanzania vimeanzisha kozi za ngazi ya shahada na stashahada ya uandishi wa habari na mawasiliano.

Pia hata ktk webusaiti ya www.bbcswahili.com kuna sehemu ya kozi ya uandishi wa habari chini ya kichwa cha habari Chuo Cha Habari BBCSWAHILI London ambapo mtangazaji wa BBC London idhaa ya kiswahili anaelezea vipi unaweza kuwa muandishi/mtangazaji mzuri.

Hivyo tunategemea kuona kiwango cha uandishi wa habari kikizidi kwenda juu na sio kurudi nyuma kama sasa.
 
Kama kuna watu wanaandika unprofessionally basi ni hawa waandishi wa Tz, wengi wao ni makanjanja tu wanatetea mialiko yao ya Ikulu ndo maana walipoambiwa ukweli na K'wete hawakuja juu na Mzee mkapa kasema kidogo tu wakaja juu. Kama mnakumbuka hawa waandishi wanafiki ndo wakati Mkapa anakaribia kumaliza muda wake walipiga kelele ili katiba ibadilishwe na Mkapa aendelee. Unafiki tu!
 
Mkuu ungerudia kusoma nilichoandika, inawezekana unachosema ni kweli.
Lakini je, Kikwete pia kasema waandishi Tanzania wanakula rushwa yeye yuko sahihi? mbona hasakamwi? anasakamwa Mkapa tuuuuu??!!

Aliyoyasema Kikwete yapo na aliyiyasema Mkapa yapo. kila mmoja amezungumza kivyake na kwa wakati huu kila mtu ana influence tofauti, huwezi kutegemea waandishi wa habari wamsakame RAIS wao nyie VIPI???

Waandishi wa Habari hawana tofauti na Madreva wa mabasi makubwa wahudumu wa Hotel n.k. vitu hivi kwa TAnzania ni mataokeo ya kutojiandaa na UTANDAWAZI, ongezeko la mabasi na Vyombo vya habari havikwenda sambamba na ongezeko la vyou bora vya wajournalist na madrivers, zamani tulizoea kuwaona madreva wa malori na mabasi wakiwa ni wazee mambo hayo yamebadirishwa na kasi ya maisha.

Vyuo vya waandishi wa habari tulizoea kuona vyuo vya certificates na diploma sasa hivi madegree ndio yanaanza kuchangamkiwa, kifupi nadhani ni fani muhimu liyikuwa imesahauliwa it is a matter of time things will change wajameni hasa baada ya wao kunyooshewa vidole.

Na nyie watanzania acheni kusoma soma UDAKU mnawafanya wamiliki wa vyombo vya habari waajiri waandashi uchwara wenye kuwa na uwezo wa kuandika udaku tu ili magazeti yauzwe, wakiandika mada za maendeleo hamuoni kama ni magazeti, yakiletwa magomeni, temeke, ilala hakuna wa kuyanunua mpaka masaki, mikocheni na labda mwenge kwakuwa mimi naishi huko
 
Back
Top Bottom