WanaHabari waliosema AS Vita Club ni hatari wakiwa Ugenini Wameufyata kwa Simba SC

WanaHabari waliosema AS Vita Club ni hatari wakiwa Ugenini Wameufyata kwa Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Baadhi ya wanaHabari na Wachambuzi wa soka kuelekea mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya AS Vita Club, waliosema As Vita Club ni hatari sana wakiwa viwanja vya ugenini, hatimaye sasa wameufyata mkia baada ya kipigo cha mabao 4-1 na kufuzu hatua ya robo fainali kwa kishindo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Walisema baadhi ya nukuu zao "As Vita Club msimu huu ni hatari wakiwa ugenini kuliko wakiwa kwenye dimba lao, katika mechi 4 ambazo wamecheza kwenye hatua ya makundi wamecheza vizuri sana na wamefanikiwa kupata alama 4 ambazo wamezipata kwenye viwanja vya ugenini hivyo wana nafasi ya kuibuka na ushindi". Walisema.

Nyie... Nyie waandishi na Wachambuzi kwanini hamkuipa haki yake Simba SC? Hizo rekodi mbona Simba anazo, amekusanya alama 4 ugenini, Simba SC ni Klabu Kubwa na Bora Afrika, acheni kuichukulia poa, Simba SC ni Next Level, anakufunga na anakupigia mpira mwingi uwanjani (BIRIANI), haya sasa mmeufyata kwa Simba SC.

AS Vita Club amefedheheshwa mno amepingwa nje ndani na kufurushwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
FB_IMG_1617462872323.jpg
 
Back
Top Bottom