SI KWELI Wanahabari waliovujisha video ya Rais wa Sudan Kusini akijikojolea wauawa

SI KWELI Wanahabari waliovujisha video ya Rais wa Sudan Kusini akijikojolea wauawa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit alitokwa na mkojo iliyolowesha suruali yake wakati wa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuzindua mradi mpya wa barabara, Jumanne Desemba 13, 2022.

Video ya tukio hilo ilisambaa na kukawa na uvumi kuwa waandishi waliokuwa na rais Kiir siku hiyo wameuawa na wengine wamekimbilia Kenya.

1671354338999.png
 
Tunachokijua
Mbali na Sudan Kusini kuwa na mazingira magumu ya wanahabari, waandishi waliokuwa na Rais hawajathibitishwa na mamlaka za nchi hiyo kuwa wamepotea.

Umoja wa Wanahabari wa Sudan Kusini walitoa waraka ukionesha kuwa hakuna muandishi aliyewekwa jela au kuuawa au kupotea baada ya tukio hilo kutokea.

Uchunguzi wa JamiiForums umebaini kuwa picha ya mtu aliyejinyonga ambayo inamtaja mtu huyo kuwa ni mwandishi aliyerekodi video ya Rais si sahihi. Mtu huyo alijinyonga mwezi Agosti 2022 hivyo hahusiki na taarifa inayonasibishwa naye na wala hakuwa mwandishi wa habari.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit alitokwa na mkojo iliyolowesha suruali yake wakati wa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuzindua mradi mpya wa barabara, Jumanne Desemba 13, 2022.

Video ya tukio hilo ilisambaa na kukawa na uvumi kuwa waandishi waliokuwa na rais Kiir siku hiyo wameuawa na wengine wamekimbilia Kenya.

Kumbuka kuwa hata kule kuna vitengo kama uvccm kwahiyo kama serikali imewaua kweli na kuwapoteza lazima vitokee vikundi vya kupinga hilo.
 
Asante sana JFCheki kwa kufuatilia hii taarifa na kutuletea ukweli. Waandishi wengi tulikuwa tumeanza kuogopa kuripoti matukio.
 
Makosa mawili kwenye post hii:-

1. Zimetajwa nchi mbili tofauti za Sudan na baadaye Sudan Kusini (South Sudan).

2. Muandishi badala ya Mwandishi.

Edit before you post any stuff.
Nina mambo sita juu yako Mkuu moja ni hapa ni ''Common errors'' amefanya ni somo kamili linalo jitegemea!!......weye ndo una makosa ya uelewa rudi drsani bila kipingamizi ukasome what is commn errors!...hiyo moja! pili....hujui Rais wa sudan ni nini! ...na nani.. wapi...... lini....

tatu umeandika makosa tena kwa kujiamini! bila kujiuliza unachokifanya!.......

Nne bado upo unaishi na wanao/majirani wanona. ulivyo kibua......Tano sisemi sana utaja jiua bureee,,,,,sita....endelea mwenyewe!
 
Ameandika Julius Bukyana, Mhariri wa NBS TV ya nchini Uganda.
_________
"Baadhi ya waandishi walioripoti habari ya Rais Salva Kiir kujikojolea hadharani wakati akiimba wimbo wa taifa, wameanza kupotea na wengine miili yao kuokotwa wakiwa wamefariki. Mwili wa mwandishi mmoja wa gazeti la New Nation umeokotwa wikiendi iliyopita na mwandishi wa Juba Monitor hajulikani alipo. Jumuiya ya Afrika mashariki inapaswa kupaza sauti kwa majirani zetu hawa. Uandishi wa habari ni taaluma sio jinai"
Walichokosea waandishi walipaswa kukwepesha kamera kwa kwa kuwa shughuli ile ilikuwa live. Hata hivyo kama ni kweli waandishi wameuawa ni kitendo cha kikatili na kilaaniwe. Mungu haruhusu ukatili wa kutoa roho ya mwanadamu mwenzako kwa vyovyote vile. Soma kitabu cha Kutoka 20:13. Kutoa uhai wa mwanadamu mwenzako ni laana kwa aliyetekeleza na aliyeagiza. Laana hiyo haiishii kwa mkosaji bali kwa kizazi chake chote.
 
Ameandika Julius Bukyana, Mhariri wa NBS TV ya nchini Uganda.
_________
"Baadhi ya waandishi walioripoti habari ya Rais Salva Kiir kujikojolea hadharani wakati akiimba wimbo wa taifa, wameanza kupotea na wengine miili yao kuokotwa wakiwa wamefariki. Mwili wa mwandishi mmoja wa gazeti la New Nation umeokotwa wikiendi iliyopita na mwandishi wa Juba Monitor hajulikani alipo. Jumuiya ya Afrika mashariki inapaswa kupaza sauti kwa majirani zetu hawa. Uandishi wa habari ni taaluma sio jinai"
Habari nyingine zinachefua.
 
ni uonevu, kwani si alijikojolea kweli au
 
Rais wa nchi za waliostarabika toka karne ya 16, kama Rais wao angejinyea au kujikojoelea yule mwandishi angepewa tuzo, Africa ananyongwa

tofauti kubwa mno, tupo mbali saana.
 
Back
Top Bottom