Wanahabari wetu ni dhaifu sana

Wanahabari wetu ni dhaifu sana

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Inawezekana mitaala yetu nchi nzima ni mibovu hivyo inatoa wanafunzi, walimu na wahitimu wabovu pia kwenye kila fani, lakini wahitimu kwenye journalism ni wabovu zaidi,

Zamani waandishi habari walikuwa mahiri sana kiasi Cha kuunda mhimili 4 baada ya serikali, bunge na mahakama.

Mwisho wa wanahabari kuwa mhimili wa 4 ilikuwa wakati wa akina Jenelali ulimwwngu, Bagenda, hamza kasongo, tido mhando, na wengine.

Leo hii kila mwandishi wa habari anatetemeka wakati anaamdika au kusoma habari. Wamejawa na woga, wanajiposition ili kupata uteuzi, hii ni hatari sana kwa taifa na dunia. Watu hawataujua ukweli wote kwa namna hii. Utajua kila mwanasiasa anachotaka ukifahamu. Wanasiasa Sasa wanatulazimisha blue tuseme ni nyeusi tunataka au hatutaki. Wanahabari wetu are cowards terribly to say and write what they want to write, real cowards. They can not write about what they believe it is true them, nation and to the world, instead they have decided to join the politicians. They can not fight them now they join them squarely.
 
Alisema JPM kila kitu hewa.

Yawezekana kila kitu ni dhaifu.

Wapi panabakia?

Shikamoo Prof. Assad.
 
Pole sana kwa Kuchelewa kujua Mapungufu yao ambayo kwa Sisi wengine tulishaanza Kuyaona miaka 20 iliyopita na kama ni Kuwakosoa na Kuwaelekeza tena kwa Kuwafundisha pia tumeshafanya mno ila wamebakia ( wameamua ) kuwa Vichwa Maji na kutotaka Kubadilika. Binafsi nilishawadharau Kitambo Mkuu.
 
Inawezekana mitaala yetu nchi nzima ni mibovu hivyo inatoa wanafunzi, walimu na wahitimu wabovu pia kwenye kila fani, lakini wahitimu kwenye journalism ni wabovu zaidi...
Bro usiwalaumu waandishi kwani hawana vyombo vyao wanafanya kazi kwenye vyombo vya wayu na inabidi wafate sera za hao watu waliowaajiri

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Sijabaini bado hoja yako, ila naendelea kupitia tena
 
Pole sana kwa Kuchelewa kujua Mapungufu yao ambayo kwa Sisi wengine tulishaanza Kuyaona miaka 20 iliyopita na kama ni Kuwakosoa na Kuwaelekeza tena kwa Kuwafundisha pia tumeshafanya mno ila wamebakia ( wameamua ) kuwa Vichwa Maji na kutotaka Kubadilika. Binafsi nilishawadharau Kitambo Mkuu.
Wanasiasa wako huru siku hizi kufanya na kusema chochote baada ya mhimili huu wa habari kufa nchini. Waandishi wa nchi nyingine ndio chanzo Cha utawala Bora kwenye mataifa yao.

Wanaibua hata nyaraka za Siri ili kuiponya nchi na dunia. Sisi hawa wa kwetu wote wamegeuka wachambuzi wa michezo (comfort zone yao).
 
Bro usiwalaumu waandishi kwani hawana vyombo vyao wanafanya kazi kwenye vyombo vya wayu na inabidi wafate sera za hao watu waliowaajiri

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Kama unaona chombo kinaenda kinyume na unachokiamini ni heri utoke TU. Mimi niliwahi kuachakazi chuo kikuu kimoja baada ya kuona chuo hicho hakifuati maadili na taratibu. Kuna shida gani watu kuacha kazi na kujitegemea? Elimu yetu ni mbovu bhana, hata Prof. anaogopa kusema ukweli ili asipoteze ajira.
 
Inawezekana mitaala yetu nchi nzima ni mibovu hivyo inatoa wanafunzi, walimu na wahitimu wabovu pia kwenye kila fani, lakini wahitimu kwenye journalism ni wabovu zaidi...
Mkitekwa mnaanza sema tunaenza Zimbabwe
 
Ikatokea bahati mbaya ukafungilia hizi radio hasa za FM utashangaa sana ndugu yangu hutaamini!!! Mimi ndio maana niliachana na local chanels radio na TV!!!
 
Hata mimi napata kichefuchefu kusikiliza hizi Radio na TV. Utafikiri wako kwenye payroll ya serikali. Ukiwauliza utawasikia wakisema hakuna habari inavyozidi uhai wako . Jamani uhai wako utakuwa mashakani kama wewe peke yako TU ndiye unaeandika ukweli peke yako. Haiwezekani uhai wa waandishi woote upotee kwa kuandika habari za kweli na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kufuata taratibu zote za kiandishi zenye maslahi kwa nchi na dunia wakapotezewa uhai wao. Kila kazi inazo occupational risks zake ambazo ni sehemu ya kazi husika. Mfano, hatushangai mtu wa umeme kupigwa shoti na umeme, mpishi kuunguzwa na mafuta jikoni, askari kujeruhiwa, daktari kuambukizwa TB, corona au HIV na mgonjwa.
 
Wanawaza teuzi !!! Ukuu wa mkoa au wilaya na vyeo vya namna hiyo
 
Wanasiasa wanazifahamu hatari zao, ndio maana wanaingiza waandishi na askari kwenye siasa ili kujihakikishia usalama wao. Wanahabari wa Sasa ni mateka wa wanasiasa.
 
Ikatokea bahati mbaya ukafungilia hizi radio hasa za FM utashangaa sana ndugu yangu hutaamini!!! Mimi ndio maana niliachana na local chanels radio na TV!!!
Wewe Ni km Mimi ht hamu ya kununua redio Sina na ht nikikuta wanangu kwny taarifa ya habari nawafokea
 
Wanawaza teuzi !!! Ukuu wa mkoa au wilaya na vyeo vya namna hiyo
Waliye waloga sijui nani?tuseme no mawindo ya teuzi tuu ama yapo ya ziada, wenyekujua msaada tafadhali.
 
Back
Top Bottom