Wanaharakati mnapochukua video muwe makini. Unachukua paa au dirisha huoni utakamatwa?

Wanaharakati mnapochukua video muwe makini. Unachukua paa au dirisha huoni utakamatwa?

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo wote!

Kwa wale waliosoma Jiografia hasa kwenye masuala ya Spatial and settlements distribution mtakubaliana na mimi kuhusu jambo hili.

Kila sehemu, Mahali Ina style yake ya ujenzi, kuanzia madirisha, uezekaji wa bati, ndani kwenye silingboard,
Pia kila Zama Zina styles zake za ujenzi na magazine.

Style ya nyumba za Iringa, Malinga, njombe, haiwezi kufanana na style ya Dodoma, Tabora Singida.
Styles za miaka ya 90 huko haziwezi kuwa sawa na styles za miaka ya elfu 2.

Ni muhimu sana wanaharakati kulijua jambo hili. Hasa wale mnaofanya harakati zile za Moto.

Bora ujirekodi nyuma uwepo ukuta au background ya kitambaa. Mtu unajirekodi unasema uko nje ya nchi wakati ndani ya chumba ulichopo kina styles zote za maeneo ya Iringa, mafinga, Makambako na Iringa
Kweli?

Unaji record nje, Miti na mimea, na udongo unaonyesha kabisa huyu yupo Geita, au maeneo ya aina hiyo. Kweli?

Kwenye mapambano ni hatari sana kufikiri umejificha zako Kumbe kuna watu wanakuangalia. Hatari sana.

Jumatatu njema.

Kwa sasa Dar es salaam
 
Ndiyo maana kwenye uchunguzi wa kisasa kuna kitu kinaitwa Open Source Intelligence (OSINT), kazi yake ni kushughulika na taarifa za kawaida kama hizo ambazo watu wengi huwa Wanazi chukulia kawaida.
 
Wanaharakati wa tanzania wengi viazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom