Wanaharakati uchwara wamepoteza ushawishi na kupata kifo kibaya cha aibu

Wanaharakati uchwara wamepoteza ushawishi na kupata kifo kibaya cha aibu

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
👉 Zama za ushawishi wa hila, propaganda za mifukoni na harakati uchwara kwenye mitandao ya kijamii zimefikia kikomo chake rasmi.

👉Wazi kuwa wanaharakati uchwara waliokuwa wanatumia mitandao kumwaga sumu na kuichafua nchi sasa wamepoteza mwelekeo na mashiko.

👉 Kila chuki waliyopanda, kila kejeli waliyoelekeza kwa Taifa lao na kila propaganda waliyosambaza sasa imewarudia wenyewe.

👉 Mbinu zao za zamani za kutengeneza taharuki na migogoro ili kupata "kiki" hazifanyi kazi tena mbele ya jamii iliyoshtuka.

👉 Wananchi wametambua kuwa harakati zao hazikuwa na nia njema ya kujenga Taifa, bali zilikuwa biashara binafsi za kusaka umaarufu na fursa.

👉 Kuweka makazi ughaibuni na kugeuza masuala ya nchi kuwa mtaji wa kujinufaisha kulikuwa usaliti mkubwa Kwa Taifa Lao,

👉 Ukweli mchungu unaowatesa kwa sasa ni kwamba Watanzania wamewachoka, wamewapuuza na kuwatupa kwenye jalala chafu la historia.

👉 Nyumba yao ya kadi waliyoijenga kwa msingi wa matusi na kejeli sasa inaporomoka kwa kishindo mbele ya macho yao wenyewe.

👉 Sauti zao zilizokuwa zikitia hofu na taharuki mtandaoni sasa zimegeuka kuwa kelele zisizo na msikilizaji.

👉 Kipindi cha kuabudiwa kwa sababu ya kutukana na kuidhalilisha nchi kimataifa kimezikiwa kwenye kaburi la aibu.

👉 Jamii imechoka kulishwa migogoro ya kutengenezwa na sasa inahitaji sauti zenye busara, matumaini na mchango halisi wa maendeleo.

👉 Ndio maana upepo wa ushawishi umehama kwa kishindo na kuelekea kwingine kabisa.

👉 Wakati enzi zao zikizama kwa aibu, sauti mpya na zenye staha kama ya Niffer zinazidi kuteka hisia za wengi na kupokelewa kwa heshima.

👉 Mabadiliko haya ya ushawishi kote nchini ni ishara ya wazi kuwa wananchi wanataka sauti zenye uzalendo na staha.

👉 Msaliti yeyote anayeichafua nyumba yake mwenyewe hawezi kupewa heshima ya kuendelea kuwa kiongozi wa fikra wa jamii hiyo.

👉 Anguko hili halikutokana na kufanyiwa mchezo mchafu, bali ni matunda ya mbegu mbovu walizopanda wenyewe kwa miaka mingi.

👉Somo zito kwa kila anayedhani kuwa anaweza kuendelea kudumu kwa kutegemea chuki, uongo na ubomoaji.

👉 Muda wa kuwapuuza na kuwaacha wajikute peke yao kwenye ulingo wao wa matusi umefika rasmi.

👉 Zama zao za kutawala fikra za watu zimekwisha na ukurasa mpya wa heshima na uzalendo ufunguliwa.

👉 Ulingo sasa umewatema waliokuwa wakichafua nchi na waliotulia kwa staha na uzalendo ndio wanaoshikilia hatamu za sasa✍️🇹🇿
HUXULkrXEAAeKIW.jpg
 
Huyo hapo pichani ndio kashika hatamu?
Ni kwa muda gani ?
 
Back
Top Bottom