π Zama za ushawishi wa hila, propaganda za mifukoni na harakati uchwara kwenye mitandao ya kijamii zimefikia kikomo chake rasmi.
πWazi kuwa wanaharakati uchwara waliokuwa wanatumia mitandao kumwaga sumu na kuichafua nchi sasa wamepoteza mwelekeo na mashiko.
π Kila chuki waliyopanda, kila kejeli waliyoelekeza kwa Taifa lao na kila propaganda waliyosambaza sasa imewarudia wenyewe.
π Mbinu zao za zamani za kutengeneza taharuki na migogoro ili kupata "kiki" hazifanyi kazi tena mbele ya jamii iliyoshtuka.
π Wananchi wametambua kuwa harakati zao hazikuwa na nia njema ya kujenga Taifa, bali zilikuwa biashara binafsi za kusaka umaarufu na fursa.
π Kuweka makazi ughaibuni na kugeuza masuala ya nchi kuwa mtaji wa kujinufaisha kulikuwa usaliti mkubwa Kwa Taifa Lao,
π Ukweli mchungu unaowatesa kwa sasa ni kwamba Watanzania wamewachoka, wamewapuuza na kuwatupa kwenye jalala chafu la historia.
π Nyumba yao ya kadi waliyoijenga kwa msingi wa matusi na kejeli sasa inaporomoka kwa kishindo mbele ya macho yao wenyewe.
π Sauti zao zilizokuwa zikitia hofu na taharuki mtandaoni sasa zimegeuka kuwa kelele zisizo na msikilizaji.
π Kipindi cha kuabudiwa kwa sababu ya kutukana na kuidhalilisha nchi kimataifa kimezikiwa kwenye kaburi la aibu.
π Jamii imechoka kulishwa migogoro ya kutengenezwa na sasa inahitaji sauti zenye busara, matumaini na mchango halisi wa maendeleo.
π Ndio maana upepo wa ushawishi umehama kwa kishindo na kuelekea kwingine kabisa.
π Wakati enzi zao zikizama kwa aibu, sauti mpya na zenye staha kama ya Niffer zinazidi kuteka hisia za wengi na kupokelewa kwa heshima.
π Mabadiliko haya ya ushawishi kote nchini ni ishara ya wazi kuwa wananchi wanataka sauti zenye uzalendo na staha.
π Msaliti yeyote anayeichafua nyumba yake mwenyewe hawezi kupewa heshima ya kuendelea kuwa kiongozi wa fikra wa jamii hiyo.
π Anguko hili halikutokana na kufanyiwa mchezo mchafu, bali ni matunda ya mbegu mbovu walizopanda wenyewe kwa miaka mingi.
πSomo zito kwa kila anayedhani kuwa anaweza kuendelea kudumu kwa kutegemea chuki, uongo na ubomoaji.
π Muda wa kuwapuuza na kuwaacha wajikute peke yao kwenye ulingo wao wa matusi umefika rasmi.
π Zama zao za kutawala fikra za watu zimekwisha na ukurasa mpya wa heshima na uzalendo ufunguliwa.
π Ulingo sasa umewatema waliokuwa wakichafua nchi na waliotulia kwa staha na uzalendo ndio wanaoshikilia hatamu za sasaβοΈπΉπΏ