Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
Wakati Tanzania ilipomfukuza Boniface Mwangi mwezi Mei 2025, watu wengi walikimbilia kuikosoa, wakiita hatua hiyo ya kidikteta. Lakini sasa, Serikali ya Kenya kupitia taarifa za raia wema imemkamata kwa tuhuma nzito za kusaidia vitendo vya kigaidi wakati wa maandamano ya Juni 25 na ushahidi kamili.
Hii inathibitisha kile ambacho Mamlaka za Tanzania ziliona mapema, umakini wa vyombo vya ulinzi na usalama ulibaini haraka kuwa Mwangi hakuwa mtetezi wa amani, bali alikuwa tishio kwa usalama wa umma.
Mwezi Aprili, inaripotiwa kuwa Mwangi alijaribu kuingia nchini Tanzania kwa malengo ya kuwachochea wanachama wa CHADEMA kufanya vurugu. Kwa umakini na weledi Tanzania ilichukua hatua za haraka na za kisheria kwa kumzuia kuingia nchini.
Tangu wakati huo, amekuwa akiharibu taswira ya Tanzania akiwa Kenya, akiipaka matope nchi kwa madai ya udikteta. Lakini sasa, baada ya Idara ya uchunguzi Kenya (@DCIKenya) kukuta mabomu ya machozi, risasi za mazoezi, na ushahidi wa kidijitali nyumbani na ofisini kwake, ajenda yake ya kweli imefichuliwa.
Sasa ni zamu yao wanaharakati wa CHADEMA kwenda Kenya kusikiliza kesi dhidi ya Boniface Mwangi