Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Miaka minne ilopita nilitoa maoni kuwa, endapo wale jamaa wa UKUTA wangenywea na kutokufanya maandamano yao waliyokuwa wameyapania, basi huo ungekuwa ni ushindi mkubwa kwa Rais Magufuli. Si tu ushindi uonekanao kwa macho, bali ushindi wa kisaikolojia pia.
Niliandika hapa:
www.jamiiforums.com
Maandamano hayo hayakufanyika. Rais Magufuli aliwaambia hao walokuwa wamepanga hayo maandamano kuwa yeye ‘hajaribiwi’.
Nadhani walimwelewa alichokisema.
Miaka 2 baadaye kukapangwa tena kuwe na maandamano makubwa ambayo yangefanyika siku ya muungano. Haya hayakuitishwa na chama chochote cha kisiasa. Yaliitishwa na dada’ake na Salary Slip 🤣.
Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani.
Mwaka huu tena vyama vya ACT-Wazalendo na CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi mkuu na kudai kuwa vimefanyiwa hujuma, viongozi wake wakaitisha maandamano ya amani nchi nzima, yasiyo na kikomo, ya kupinga matokeo.
Hakuna hata mtu mmoja aliyeingia barabarani na kuthubutu kuandamana.
Huwa naona sana humu wale akina dada wa Twitter, wale wanaharakati wa Jamhuri ya Twitter, Shangazi na yule mwezake Binti Maria wakisifiwa sana wanapo longalonga huko kwenye hiyo jamhuri yao. Halafu kuna huyu raia mpya aitwaye Amsterdam. Naye naona anapenda sana kulonga huko kwenye hiyo jamhuri.
Kwamba eti ni majasiri sana. Hawamwogopi mtu, blah blah blah.
Sasa, kama kweli hawamwogopi mtu na hawaogopi kitu, kwa nini sasa huwa wanaishia kupiga mayowe kwenye hiyo jamhuri yao? Kwa nini wasitende kwa vitendo hayo maneno yao kwa kuingia barabarani na mabango yao na vipaza sauti kumpinga huyo wasiyempenda?
Jibu ni moja tu: na wao wanajua kuwa huyo Ngosha hajaribiwi. Akisema kitu akiwa amekasirika huwa anamaanisha. Aliposema hajaribiwi, naamini wote walioisikia hiyo kauli, waliielewa.
Kelele zipigwazo jamhuri ya Twitter haziwezi kubadili chochote kilichopo huku uraiani.
Kauli ya Ngosha na virungu vya kamanda Mambosasa, vimewapa watu uhamisho toka Tanzania kwenda Jamhuri ya watu wa Twitter.
Niliandika hapa:
Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana. Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale...