Watu wafundishwe na kueleweshwa Katiba ya sasa. Wakaishakuielewa ndipo masuala yA katiba mpya ama la ndiyo yafuatwe.
Ukimuuliza, Sukununu, katiba ya sasa ina mapungufu gani, anaangalia pua, hana chakujibu. Hakuna hata kifungu kimoja anaweza kukifafanua!!!
Bila kuelimisha wananchi wote kuelewa katiba ya sasa, mchakato wa kubadilisha katiba utatekwa na mamluki wenye ajenda zao za siri!
Kwa hiyo, wanasiasa ningawaelewa sana kama kweli wana nia ya dhati ya wananchi wakishiriki mchakato wa katiba iwapo wangeanza kampeni ya miaka mitatu kuwafundisha na kuwaelewesha wananchi katiba ya sasa.