Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Nimeona mtandaoni watu wengi wakiwamo wanasheria na wanaharakati wakitetea makahaba waliokamatwa na mkuu wa wilaya ya Ubungo
Ukahaba ni kinyume na maadili yetu watanzani na umekatazwa kwenye vitabu vyote vya dini
Sasa unapokuta mtetezi wa hao watu wanaofanya vitendo viovu unajiuliza dunia inakwenda wapi?
Wanadai kuwakamata ni kuingilia faragha za watu, sasa hata mashoga basi tusiwakamate kwa sababu ni kuingilia faragha zao pia?
Wengine utawasikia wakisema kuwa wanaojiuza wana maisha magumu, huu ni upumbavu, kwani wamama wanaouza magenge, wanaofanya usafi, wanaolima, kuosha vyombo n.k hawana maisha magumu kuliko hao makahaba?
Tumekataza ushoga na tunaupinga kwa nguvu zote kwa sababu ni kinyume na maadili yetu, kwa nini ukahaba tunashindwa kuukemea?
PIA SOMA
- Vita ya DC Ubungo na Makahaba: Mgongano wa sheria, haki na maadili
- Kuna kesi ya udhalilishaji kama wale walioonekana kwenye video ya kukamata makahaba watapata mwanasheria mzuri
- Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?