Wanaharakati wawili kutoka Kenya, Bob Njagi na Nicholas Oyoo, walidaiwa kutekwa nyara Oktoba 1, 2025 mchana na wanaume wanne wenye silaha wanaoaminika kuwa maafisa wa usalama. Wawili hao walikuwa wameungana na mgombea urais wa National Unity Platform (NUP), Bobi Wine, katika kampeni zake nchini Uganda. Mashuhuda wanasema walilazimishwa kuingia kwenye gari na simu zao kuzimwa mara moja
Kisa hiki kilitokea baada ya wanaharakati hao kuonekana wazi kwenye mikutano ya kampeni ya Bobi Wine katika Wilaya ya Kamuli, mashariki mwa Uganda. Video zilizorekodiwa zinaonyesha Mwenyekiti wa Free Kenya Movement, Bob Njagi, akiwa jukwaani sambamba na kiongozi wa upinzani Bobi Wine. Katika nyakati nyingine Njagi alionekana akimsikiliza kwa makini Bobi Wine na hata kuungana naye kwenye msafara wa kampeni vijijini
Kwa mujibu wa rafiki yao, waliwasili Uganda Septemba 29, 2025 wakiwa na Waganda wawili ambao baadaye walirudi makwao, na kuwaacha Wakenya watatu kuendelea na kampeni za NUP. Septemba 01, 2025, walishiriki kampeni katika maeneo ya Buyende na Kamuli wakiwa pamoja na viongozi wa upinzani. Lakini hali ilibadilika ghafla Jumatano mchana waliposimama kituo cha mafuta kurekebisha gari
Mashuhuda wanasema majira ya saa tisa alasiri, gari la rangi ya kijivu liliwasili na watu wanne wenye silaha wakishuka. Mwanamke mmoja pia alikuwamo ndani ya gari. Walimkamata Bob Njagi na Nicholas Oyoo, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Free Kenya Movement. Rafiki yao aliyenusurika alisema yeye pia alitekwa kwa muda mfupi lakini aliachiliwa baada ya kuwaeleza wahusika kuwa gari lake halikuwa limefungwa
Mara baada ya wanaharakati hao kuchukuliwa, simu zao zilikatika na rafiki yao akabaki peke yake, akiwa na hofu kubwa. Hadi sasa hajathubutu kuripoti kwa mamlaka akihofia usalama wake. Tukio hili linajiri miezi minne tu baada ya mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Agather Atuhaire wa Uganda kukamatwa nchini Tanzania na kudai walipitia vitendo vya ukatili. Kwa upande wa Njagi, hii si mara yake ya kwanza kutekwa kwani mwaka jana alitoweka kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kutekwa kwa tuhuma za kushiriki maandamano ya kupinga serikali