G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Ukweli wanaJamiiForums kwa gwiji wetu Pascal Mayalla tumeonyesha chuki ya wazi ikiwemo mimi, namuomba radhi.
Ingawa Pascal ni CCM ila alikuwa hana ule u CCM kama makada wengine. Pasco ni mhanga wa mambo mengi yaliyotokea kwenye utawala huu ikiwemo kusitishiwa tenda zake muhimu zilizokuwa zikimpa ugali na watoto kwenda chooni. Pamoja na wengi wetu kujua kuwa Pasco alitia nia, tulijitenga naye na kwa hapa hatukuwaza vizuri.
Ingekuwa vizuri sana kwa Pasco kuweo bungeni kuliko mwana CCM yeyote yule na jukwaa letu hili pendwa lingepata sauti kubwa bungeni. Ndiye mwanajamii forum pekee aliyejitokeza hadharani na kuitaja Jamii forum tena kwa herufi kubwa. Hakuna mpinzani wala mwana CCM yeyote aliyewahi na hadi sasa hakuna.
Kumkosa Pasco bungeni ni huku tukijua kuwa alikuwa akiipa Jf kipaumbele cha kwanza kabisa, pia huku sisi tukijibaragaza humu tulishindwa kabisa kumfanya asikike walau hata kwa kumuanzishia vi thread vya kumpamba, tumecheza vibaya. Pia Pasco ni mwana CCM ambaye anaiheshimu sana katiba, hapa jukwaa letu kama ikitokea likaguswa huyu angesimama kidete.
Sauti ya mwanaccm mmoja inasikika pale anapopinga kitu kuliko sauti ya wapinzani 1000. Tumemkosa mwanaccm nyutro na huenda tukaja kuona madhara yake baadaye! Huyu asingeegemea chama! Huyu kati ya chama na JF angesimama na JF!
So sory bro, tumekukosea na nikiri kuwa hakuna tena mwanaccm wa aina yako ambaye tungempata ndani ya bunge lijalo.