Wanajanvi tumsaidie Mzee MUHIDINI GURUMO.

Wanajanvi tumsaidie Mzee MUHIDINI GURUMO.

Saitot

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2013
Posts
613
Reaction score
152
Nikiwa kama mpenzi wa burudani , hasa muziki wa dansi nimejisikia vibaya baaada ya kumuona huyu mzee leo chanel Ten, akiomba msaada wa watanzania kumchangia chochote kwa tamasha ambalo litafanyika dar es salaam.Amediriki kusema katika miaka yote ya kimuziki hajafanikiwa kumiliki hata baiskeli,. Kwa hali hii naamini kabisa ndo maana wengi wa wasanii hujiingiza katika biashara haramu ili waendane na majina yao.
 
Mwaka huu nlimwona akitumbuiza kwenye sherehe ya maccm huku akiyasifia sana kwa mafanikio, hivi yalishindwa msaidia hadi aombe kwetu
 
Kuna watu wanadharau humu??? Maisha yanabadilika ndgu zangu, leo kwa mwenzio kesho kwako
 
Hivi huyu Mzee anaumwa nini hasa?
 
Kwanini wanamuziki,wasanii,wanamichezo wanapenda sana wasaidiwe,kwani nini kipi wamekifanya tofauti na watu wengine kama waalimu,waganga,askari,wakulima?wote tunalitumikia hili taifa na kila mtu anafanya kazi pia kwa ajili ya aisha yake,wao wamewachangia nani,nakumbuka Mzee Msuya aliwahi sema kila mtu atabeba msalaba wake,watu wakamjia juu,hapana kila mtu kwa hivi sasa ana msalaba wake,sidhani kama kuchangia kuna saidia kitu,naamini Gurumo ana familia yake ambayo ndio inatakiwa ibebe msalaba wake,kila mtu anashida ,maisha ni kujipanga,tena Gurumo yeye aliwahi ana nyumba nzuri na maisha mazuri tu na hata hela ameishika sana.na kila mtu aubebe msalaba wake mwenyewe,ukiwa na nguvu jitengenezee maisha ya mbeleni,somesha watoto wako ambao watakuja kukusaidia baadaye,kama kutumikia au kutangaza nchi kila mmoja wetu kwa njia moja au nyingine wote tumeshiriki,sio lazima tuwe wanasanaa au wanamichezo ndio tujulikane kama tumeitangaza nchi,hiyo ni dhana potofu.
 
Back
Top Bottom