5523
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,275
- 2,410
Na BBC Swahili
Vita vya Bakhmut, mji wa Ukraine ambao Urusi imetumia miezi kadhaa kujaribu kuuteka, "inaendela kwa utulivu", anasema kamanda mkuu wa Ukraine. Mapema mwezi huu, maafisa wa Magharibi walikadiria kati ya wanajeshi 20,000 na 30,000 wa Urusi waliuawa au kujeruhiwa huko Bakhmut tangu msimu uliopita wa joto.
Lakini pamoja na hayo, Valerii Zaluzhnyi alisema "juhudi kubwa" za wanajeshi wa Ukraine zinairudisha nyuma Urusi.
Moscow ina hamu ya ushindi baada ya kushindwa kupata mafanikio makubwa katika siku za hivi karibuni.
Licha ya hayo, wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanaamini kuwa Bakhmut ina thamani ndogo ya kimkakati, na umuhimu wa jiji hilo sasa ni wa kiishara.
Katika mtandao wa Facebook, Luteni Jenerali Zaluzhnyi alisema kwamba wakati hali kwenye mstari wa mbele wa Ukraine "ni ngumu zaidi katika mwelekeo wa Bakhmut...kutokana na juhudi kubwa za vikosi vya ulinzi, tunafanikiwa kuleta utulivu."
Luteni Jenerali Zaluzhnyi alichapisha ujumbe huo baada ya kuzungumza na Mkuu wa Majeshi wa Uingereza, Admirali Sir Tony Radakin, kuhusu hali ya Ukraine.
Maoni yake ni ishara chanya ya hivi punde kutoka kwa maafisa wa Ukraine kuhusu vita virefu vya Bakhmut.
Siku ya Alhamisi, Oleksandr Syrsky, kamanda wa vikosi vya ardhini vya nchi hiyo, alisema kuwa wanajeshi wa Urusi "wamechoka" huko Bakhmut.
Bwana Syrsky aliongeza kuwa wakati Urusi "haijakata tamaa ya kuchukua Bakhmut kwa gharama yoyote licha ya hasara ya wanajeshi wake na vifaa... wanapoteza nguvu kubwa".
Mji huo ulikuwa na wakzi 70,000 kabla ya kuanza kwa vita lakini sasa umesalia na watu wachache tuwengi wakikimbia usalama wao.