Wanajeshi 20,000 wa Urusi wadaiwa kuuawa au kujeruhiwa huko Bakhmut, Ukraine

Wanajeshi 20,000 wa Urusi wadaiwa kuuawa au kujeruhiwa huko Bakhmut, Ukraine

Na BBC Swahili

View attachment 2564673
Vita vya Bakhmut, mji wa Ukraine ambao Urusi imetumia miezi kadhaa kujaribu kuuteka, "inaendela kwa utulivu", anasema kamanda mkuu wa Ukraine. Mapema mwezi huu, maafisa wa Magharibi walikadiria kati ya wanajeshi 20,000 na 30,000 wa Urusi waliuawa au kujeruhiwa huko Bakhmut tangu msimu uliopita wa joto.

Lakini pamoja na hayo, Valerii Zaluzhnyi alisema "juhudi kubwa" za wanajeshi wa Ukraine zinairudisha nyuma Urusi.

Moscow ina hamu ya ushindi baada ya kushindwa kupata mafanikio makubwa katika siku za hivi karibuni.

Licha ya hayo, wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanaamini kuwa Bakhmut ina thamani ndogo ya kimkakati, na umuhimu wa jiji hilo sasa ni wa kiishara.

Katika mtandao wa Facebook, Luteni Jenerali Zaluzhnyi alisema kwamba wakati hali kwenye mstari wa mbele wa Ukraine "ni ngumu zaidi katika mwelekeo wa Bakhmut...kutokana na juhudi kubwa za vikosi vya ulinzi, tunafanikiwa kuleta utulivu."

Luteni Jenerali Zaluzhnyi alichapisha ujumbe huo baada ya kuzungumza na Mkuu wa Majeshi wa Uingereza, Admirali Sir Tony Radakin, kuhusu hali ya Ukraine.

Maoni yake ni ishara chanya ya hivi punde kutoka kwa maafisa wa Ukraine kuhusu vita virefu vya Bakhmut.

Siku ya Alhamisi, Oleksandr Syrsky, kamanda wa vikosi vya ardhini vya nchi hiyo, alisema kuwa wanajeshi wa Urusi "wamechoka" huko Bakhmut.

Bwana Syrsky aliongeza kuwa wakati Urusi "haijakata tamaa ya kuchukua Bakhmut kwa gharama yoyote licha ya hasara ya wanajeshi wake na vifaa... wanapoteza nguvu kubwa".

Mji huo ulikuwa na wakzi 70,000 kabla ya kuanza kwa vita lakini sasa umesalia na watu wachache tuwengi wakikimbia usalama wao.
Slava Ukraine...💪💪
 
Unategemea BBC wataleta habari gani ambazo siyo biased -mbona hawasemi kwamba wanajeshi wa Ukraine wamejificha kwenye reinforced concrete bunkers zilizo jengwa wakati wa utawala wa kisoviet kujikinga dhidi ya nuclear missiles za Kimerikani, mahandaki hayo yalijengwa madhubuti mtu unaweza kuishi humo hata mwaka mzima bila ya kutoka nje/juu ya aridhi kuna mpaka barabara - Waukraine wameficha silaha nyingi humo na wanajeshi ndio maana kwenye vyombo vya habari wanasema kamji hako ni insignificant,sasa kama hakana maana kwa nini mnakag'ang'ania na kupoteza wanajeshi lukuki kuna nini pale??

Naona kilicho baki sasa kama Zelensky na washauri wake wa kijeshi wakigangania mji huo Urusi italazimika kitumia mabom/missiles bunker busters na kuwamaliza wote walio jificha humo pamoja na silaha zao.
 
JWTZ hii hii mkuu? Embu acha kuvunjia heshima Jeshi letu. Ukiweka silaha za Nuclear chini, mchukue Mrusi, Mchina, Iran n.k wote waweke pamoja kisha walete, hawachomoki hao wehu.

Tena tukipewa vifaa ndo kabisaaa.
Naliheshimu JWTZ nimelelewa nalo lakini ulichokisema hapana kwakweli.
 
Russia tuliyokuwa tunasimuliwa ni imara,kumbe ni mdebwedo sijaona.Hata jeshi letu imara la JWTZ likizipiga na Russia linamshinda mapema sana.
.
Screenshot_20230313-143119.jpg
 
JWTZ hii hii mkuu? Embu acha kuvunjia heshima Jeshi letu. Ukiweka silaha za Nuclear chini, mchukue Mrusi, Mchina, Iran n.k wote waweke pamoja kisha walete, hawachomoki hao wehu.

Tena tukipewa vifaa ndo kabisaaa.
Ila kwa kigezo hiki utasema Marekani anaweza.
 
Mhh! Kijana hao warusi wanapigana vita dhidi ya ulaya nzima na Marekani mpaka sasa. Wana uwezo mkubwa sana wa kijeshi acha maneno ya ajabu.
Sio maneno ya ajabu bro, bali ndo ukweli wenyewe.Anachojivunia Mrusi ni kule kuwa na idadi kubwa ya askari(Askari wengi). Kwa Mrusi kuuawa kwa askari sio hoja kwake -Ataleta wengine, wakiuawa ataleta wengine tena mpaka mtachoka kuwaua. Unaweza kulionja hilo katika mpambano uliotokea huko mji wa Bakhmut Ukraine ambapo watoa habari walisema ilikuwa Rusia analeta askari ni wimbi baada ya wimbi na mji huo ulitapakaa maiti/mizoga ya askari. Hapa nazungumzia Infantry kwani hao ndo wanaoteka maeneo.
 
Katika hiyo 'mizoga' kama ya Urusi ni 20,000, ya Ukraine ni mingapi?

Hizo ni propaganda za kivita za kimagharibi na sii zaidi ya hapo.
Inaweza kuwa kweli ni propaganda tena za kimagharibi lakini ukweli utaendelea kubaki kwamba walikufa askari wengi pamoja na raia walionaswa katika mapigano hayo.
 
Wazee wakutoa takwimu za wenzao kuliko zao mngekuwa mmeurejesha uwoo mji ata nusu tu ingekuwa jambo la maana ila mnatoa takwimu kuficha hasara mliyoipata
 
Zelensky aliwaambia Westerners kuwa Bakhmut ikianguka ndio utakuwa mwisho wa mchezo. Kwahiyo NATO wameweka nguvu zotee hapo Bakhmut na hiyo ndio imepelekea kufanya progress ya WAGNER kwenda mdogomdogo. Lakini mwisho wa yote Bakhmut itakwenda tu mtake msitake

kherson na kharkiv ziliondoka ndan ya miez mitatu ya counteroffencv. bakhmut ndio sehem pekee ya russia kufutia aibu. lakin wap. mwaka unakatika soon
 
Back
Top Bottom