Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Nimeona video inayomuonesha mkufunzi mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akizungumza mwaka 2024, ambapo anasikika akikipongeza chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kile alichokiita “kazi nzuri,” na hata kumpongeza kiongozi wa chama hicho.
Kauli kama hii mara chache sana hukemewa au kuchukuliwa hatua, pengine kwa sababu mhusika ni mwanajeshi anayekitaja chama tawala. Hata hivyo, ingekuwa ni mwanajeshi anayetoa kauli ya kuunga mkono chama cha upinzani hususan CHADEMA ni wazi tungeona matamko, ukemeaji na huenda hatua za kinidhamu zingeanza kuchukuliwa mara moja.
Hali hii inaleta sintofahamu kubwa kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa jeshi lolote duniani linatakiwa kuwa huru na lisilojihusisha na siasa. Jeshi ni chombo cha taifa, si cha chama chochote cha siasa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Sura ya 192 (The Tanzania People’s Defence Forces Act), msimamo huu uko wazi kabisa.
Kifungu cha 48(1)(a) kinaeleza kwamba:
“Mwanajeshi hatakiwi kushiriki katika shughuli yoyote ya kisiasa bila ruhusa ya mamlaka ya juu ya kijeshi.”
Hii inajumuisha:
Kwa mantiki hiyo, ikiwa mwanajeshi huyo hatochukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu licha ya kauli yake ya kuunga mkono Chama cha Mapinduzi, basi hatua hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa kuwadharau wananchi na kuvunja misingi ya usawa na uadilifu ndani ya taasisi za umma.

- Kuonesha hadharani uungaji mkono kwa chama cha siasa,
- Kuhudhuria mikutano ya kisiasa,
- Au kutumia sare au nyenzo za kijeshi katika shughuli za kisiasa.