Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Nilibahatika kuwapa lift Askari wawili wa JWTZ waliokuwa wanatoka kazini huko Monduli. Kwa kuwa kuna joto la Uchaguzi Wajeshi hao walikuwa na interest sana kujua tutampigia kura nani kwa Urais hapo 31 Oktoba. Rafiki yangu aliwajibu kuwa wao (Wanajeshi) ndiyo wenye hatma ya kuamua na sio wapiga kura maana hata tukimpigia kura mpinzani kama wao Wajeshi hawataki haitasaidia kitu.
Mjeshi mmoja wao akasema hakuna kitu kama hicho na kwao hakiwezekani. Ndipo yule rafiki yangu akajibu kuwa 'tutampa Dk Slaa'! Yule mwanajeshi akafurahi sana akasema ndiye anayefaa kuwa Rais maana Dk Slaa ndiye Rais wa Wanajeshi wa vyeo vya chini na Kikwete ni Rais wa wa Askari wanaoanzia na nyota moja! Alisema wao kama Askari wa chini wana malalamiko kuhusu maduka ya Free Duty ya Jeshi maana yanawafaidisha baadhi ya maofisa wa vyeo vya juu na hayana nafuu yoyote kwa Askari.
Mwenzake alitutahadharisha kuwa tusishangae kutowaoana Wanajeshi wa JWTZ ifikapo tarehe 28 Oktoba uraiani maana huenda wote wakamwa makambini; hata wanaoishi uraiani wataweka kambi Jeshini hadi baada ya Uchaguzi.
Hivyo Wadau, msishangae mtakapoona kuwa Askari wa JWTZ hawaonekani kuanzia tarehe hizo.