Wanajeshi wa Kenya waingia Tz

Wanajeshi wa Kenya waingia Tz

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2008
Posts
1,518
Reaction score
24
Nimepata habari kuwa kundi kubwa la wanajeshi wa Kenya walionekana wakiingia Tanzania kwa msururu wa magari kupitia mpaka wa Namanga.

Naomba mwenye taarifa yoyote ya lengo la wanajeshi hao kuingia TZ kwa msururu wa magari atujulishe.
 
..wanakuja kwa ajili ya mazoezi ya kijeshi ya nchi za Afrika Mashariki.

..hakuna matatizo yoyote kati yetu na Kenya.

..kama sijakosea Waziri Mkuu Mizengo Pinda yuko ktk state visit Kenya kwa mwaliko wa Waziri Mkuu Raila Odinga.
 
Wanajeshi hao walianza kuingia toka juzi, na wanakuja mahsusi kwaajili ya mazoezi ya kijeshi kwa nchi tano za jumuiya ya Afrika mashariki. Mazoezi hayo yatafanyikia mikoa ya kilimanjaro na Tanga na yatadumu hadi septemba 26.operasheni hii ya aina yake inaitwa kilmanjaro, kazi kwenu!
 
Ni kweli hakuna tatizo kati yetu na kenya ni mazoezi tu kwaajili ya hawa jamaa kujinoa zaidi na mbinu mpya za kupambana na ugaidi na mambo kama hayo.
Amani iwe nawe!
 
Ni kweli hakuna tatizo kati yetu na kenya ni mazoezi tu kwaajili ya hawa jamaa kujinoa zaidi na mbinu mpya za kupambana na ugaidi na mambo kama hayo.
Amani iwe nawe!

Asante mkuu kwa kunitoa hofu.
 
Wanajeshi hao walianza kuingia toka juzi, na wanakuja mahsusi kwaajili ya mazoezi ya kijeshi kwa nchi tano za jumuiya ya Afrika mashariki. Mazoezi hayo yatafanyikia mikoa ya kilimanjaro na Tanga na yatadumu hadi septemba 26.operasheni hii ya aina yake inaitwa kilmanjaro, kazi kwenu!

Sawa mkuu.

Kumbe TZ tuko juu kijeshi hapa afrika mashariki?
 
Ni kweli Exaudi wameingia jana,niliona msafara mrefu sana wa magari ya jeshi pamoja na gari za kampuni ya Akamba (six buses) zilikuwa zimebeba wanajeshi wakielekea Monduli.
 
Naona watu wana hasira na nchi yao!, hizi habari muhimu.

Acha GESH LIJIENDELEZE!!!
B.
 
Ni kweli hakuna tatizo kati yetu na kenya ni mazoezi tu kwaajili ya hawa jamaa kujinoa zaidi na mbinu mpya za kupambana na ugaidi na mambo kama hayo.
Amani iwe nawe!
Usisahau kuna uchaguzi unakuja mwakani! Hisije kuwa ni moja ya mazoezi ya kujinoa na haya mambo ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom