John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Wanajeshi wa Urusi wameukamata mji mmoja muhimu wa bandari wa Ukraine na kuuzingira mwingine kama sehemu ya juhudi za kuitenganisha nchi hiyo na Pwani yake.
Jeshi la Urusi limesema limechukua udhibiti wa Kherson na maafisa wa Ukraine katika eneo hilo wamethibitisha kuwa wanajeshi wamechukua udhibiti wa makao makuu ya serikali ya mitaa katika mji huo wa bandari ya Bahari Nyeusi wenye wakazi 280,000.
Kherson sasa ndiyo mji wa kwanza mkubwa kuanguka tangu kuanza uvamizi wa Urusi wiki moja iliyopita. Kwingineko, Warusi wameendelea na mashambulizi yao katika maeneo kadhaa, ijapokuwa msafara wa vifaru na magari mengine unaripotiwa kukwama kwa siku kadhaa nje ya Mji Mkuu Kyiv.
Mapigano makali yameendelea leo viungani mwa mji mwingine muhimu wa bandari katika Bahari ya Azov, Mariupul na kuutumbukiza gizani. Umeme na mawasiliano ya simu vimekatwa, na makazi na maduka yanakabiliwa na uhaba wa chakula na maji.
Chanzo: DW