Wanajeshi Wanne wa Nepal na komando wao wakamatwa Dar es salaam, Tanzania

Wanajeshi Wanne wa Nepal na komando wao wakamatwa Dar es salaam, Tanzania

Vunja ukimya..tujitolee kuwafichua watu kama hawa...!maana wengi wao wanakua na mission maalum nchini mwetu..si ajabu wanawasaidia hawa walipua mabom...na tindikalii
 
kaka au ndugu unataka niweke wazi ili umfiche au wamfiche nimeeleza for more information ni pm

mkuu hata mimi ninayemmoja anajifanya mtanzania ila nimkenya na ni muhindi tena wa maeneo ya Mombasa, kamefoji vyeti vya mpigakura na akahonga police akapewa driving licence ya TZ!!! Pia wahusika mje PM pia niwape details!
 
Mtwara wamejaa tele wahamiaji haramu. Mwingine raia wa Uingereza Mama anaitwa Samantha anaishi mitaa ya Mnarani anamiliki Lorge ipo mitaa ya Shangani karibu na Pride FM. Vibali vya kuishi nchini na vya kuendesha lorge ni magumashi matupu. Wahamiaji haramu wamejaa hapa Mtwara na wanasaidiwa na jamaa mmoja wa uhamiaji na sehemu ya kuchukulia mshiko anachukulia pale Posta Mkoa ndani ya gari. Hao wachina ndo usiseme kiwanda cha Cement kinachojengwa nje ya mji wa mtwara kumejaa wachina wengi wao ni magumashi... kama Hongkong yani.
Hilo jina Samantha mbona kengele zinalia isije kuwa mnaishi na yule white widow aliyezungumziwa Nakumatt ilipopigwa Kenya!Na hao pichani kutoka Nepal-what if ni mercenaries wamekuja kwa kazi maalum tubaki kusema wamekimbia maisha magumu!komandoo akimbie nchi?labda kaasi.
 
Kweli kabisa ndugu. Natumaini wahusika wa idara ya uamiaji watachukulia suala hili kwa umakini zaidi.

Tukicheza na waamiaji tumekwisha.
 
Safiiii sana kwa waliofanikisha mpango wa kuwatia mbaroni watu kama hawa huwa hatari sana baadae
 
hao ndio magaidi wenyewe, unaweza kuta ndio ISIS wamekuja kusaidia wenzao kina Farid!
 
Kwa habari zaidi

angalia itv saa mbili
 
Nimeiona hiyo mkuu, mmmh labda sina akili yaani !!!!???? Najiuliza wameacha kazi kwao ya kuajiriwa na kuja TZ ati kufanya kazi ya ulinzi haijaniingia akilini, wafunge geti na kufungua, kulinda ktk maofisi na majumba sijaelewa, jamani wahusika tunahitaji kulindwa kwa hali na mali, Idara husika mgeni akiingia muwe mnahakikisha ameondoka muda unaotakiwa, huu ni udhaifu mkubwa imenisononesha sana. Na sisi wananchi tusaidiane katika kulinda nchi yetu ktk kuwafichua wote tulio na wasiwasi nao, hii ni nchi yetu hakuna jirani atakayekuja kutulindia mkuu makomando wamejazaje yaani wako full.
 
Ni matumaini yetu kuwa Idara ya Uhamiaji itafanyia kazi dondoo hizi zilizotolewa na wapenda nchi kuhusiana na uzi huu na tungependa watoe hata feedbak kidogo kuhusu hizi taarifa na pia namna walivyozifanyia kazi. Hii inaitwa transparency na ni kipimo ha UWAJIBIKAJI!
 
Hao ni wahamiaji haramu wanajitafutia maisha bora kama ilivyo kwa Watanzania wengi waliozamia nchi zingine.

Watanzania wengi sana utawakuta nchi za nje wakiishi bila uhalali kwa kutafuta maisha bora, sidhani kama hii ni big issue, ikumbukwe kuwa mila za Nepal ni sifa kwa kijana yoyote kuingia jeshini kama ndio kitu cha kwanza cha maisha yake na kama hakuwa jeshini basi thamani yake hushuka.

Sioni tatizo la hao kuwa hao waliwahi kuwa wanajeshi huko kwao. Ni wazamiaji kama wazamiaji wengine wowote.
 
hao ndio magaidi wenyewe, unaweza kuta ndio ISIS wamekuja kusaidia wenzao kina Farid!
div 5,hujui kama nchi hii ya Nepal wanafuata dini ya Hindu na ni Buddhists,wamechanganya dini mbili hizo kwa wakati mmoja.
 
Hii nchi ishakuwa kama ya mfalme Juha...

Uongozi nao upo kama Pazia la Sufi, kila aina ya upepo unaweza kuupuliza!

Mpaka makomandoo nao wanaingia na kuishi?

Mi nadhani Jukumu la usalama wa Taifa wangepewa JWTZ, yaani wahusika woote wa migration wawe staff wa JWTZ na wapewe mbinu zoote za upelelezi..
 
Migration na Usalama wa Taifa kwa ujumla wanatakiwa kutoa namba za simu maalum ambazo raia wangekuwa wanatolea taarifa juu ya mambo yenye wasiwasi kama haya na mengineyo yote ya kutilia shaka!

Mambo ya kujipeleka polisi! hm! unaweza kuuzwa wewe instead.
 
div 5,hujui kama nchi hii ya Nepal wanafuata dini ya Hindu na ni Buddhists,wamechanganya dini mbili hizo kwa wakati mmoja.

ebo! kwa hiyo nchi hiyo hakuna waislamu? uislamu ni uraia au ni dini? nadhani umeathirika na utaratibu wenu wa kuanza "chuo" kabla ya darasa la kwanza!
 
Hao ni wahamiaji haramu wanajitafutia maisha bora kama ilivyo kwa Watanzania wengi waliozamia nchi zingine.

Watanzania wengi sana utawakuta nchi za nje wakiishi bila uhalali kwa kutafuta maisha bora, sidhani kama hii ni big issue, ikumbukwe kuwa mila za Nepal ni sifa kwa kijana yoyote kuingia jeshini kama ndio kitu cha kwanza cha maisha yake na kama hakuwa jeshini basi thamani yake hushuka.

Sioni tatizo la hao kuwa hao waliwahi kuwa wanajeshi huko kwao. Ni wazamiaji kama wazamiaji wengine wowote.

nakuunga mkono hawa wamekuja kutafuta maisha alafu kama ulivyosema wabongo wangapi wamezamia ktk nchi za nje huko wanaishi hawana right papers za huko wamejilipua, mimi pia sioni kama big issue pia
 
Migration na Usalama wa Taifa kwa ujumla wanatakiwa kutoa namba za simu maalum ambazo raia wangekuwa wanatolea taarifa juu ya mambo yenye wasiwasi kama haya na mengineyo yote ya kutilia shaka!

Mambo ya kujipeleka polisi! hm! unaweza kuuzwa wewe instead.

Kwa nchi kama Tz unaweza kugeuziwa kibao kwa kutoa taarifa yoyote kumhusu mtu mwingine, labda tu mtoa taarifa awe mmoja wa watumishi wa idara mojawapo zinazohusika na ulinzi na usalama.
 
Wanepal wamejaa kibao Mgodini Tanzanite One,kwa kigezo eti ni ma expert wa ulinzi kuliko raia wa nchi nyingine.
 
Hao wanajeshi nadhani watakuwa ni wawindaji ,maskini tembo wetu!
 
Back
Top Bottom