Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Wanajeshi watano wa Uganda wanaofanya kazi na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia wamekutwa na hatia ya kuwaua raia saba nchini humo.
Wawili kati ya wanajeshi hao wamehukumiwa kifo, huku wengine watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 39 gerezani kila mmoja.
Wanajeshi hao watatu watarudishwa Uganda ili kutumikia vifungo vyao. Raia hao waliuawa kinyume cha sheria wakati wa mapigano ya risasi huko Golweyn kati ya wanajeshi wake na wanamgambo wa al-Shabab, AU inasema.
Jeshi la Amisom la Umoja wa Afrika limekuwepo Somalia kwa miaka 14. Limekuwa likipambana na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab ambao wanashikilia sehemu ya nchi hiyo.
Karibu theluthi ya jeshi la Amisom lenye maafisa 20,000 wanatoka Uganda- likiwa ni sehemu kubwa ya jeshi kuliko wanaotoka nchi nyingine.
Uamuzi wa mahakama ya kijeshi wa Jumamosi wa Uganda unakuja mwezi mmoja baada ya AU kutangaza kutaka kupanua operesheni yake ya kijeshi nchini Somalia, ikisubiri kibali kutoka kwa Umoja wa Mataifa na serikali ya Somalia.
BBC