Wanajisifu wanaijua Sheria kumbe wameikariri Sheria ila hawailewi wala hawaifuati

Wanajisifu wanaijua Sheria kumbe wameikariri Sheria ila hawailewi wala hawaifuati

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,397
Reaction score
12,415
Wanajisifu wanaijua sheria kumbe wameikariri sheria ila hawailewi wala hawaifuati

Hawana lolote, muda wote wanaonekana kachanganyikiwa kwasababu ya kukariri sheria wasio ielewa wala kuifuata. Wamebaki ni watu wa kulalamika usiku na mchana ili sheria iwafuate wakati wao hawaifuati. Yote ni kwasababu wanajidai ni wasomi wa sheria ya kwenye vyeti tu wakati hata kuongea kwao wanaonyesha kuongea, sheria walio ikariri bila kuielewa.

Hawana sifa za kushika Urais wa taifa hili kwasababu ni viongozi wasio na maadili kabisa sijui walisomea sheria ya wapi ambayo wanashindwa kuitumia ili iwasaidie kuheshimu kanuni na taratibu za taifa letu na viongozi wa taifa letu.

Ni viongozi ambao wanashindwa kuheshimu taasisi za taifa letu. Kama walisomea sheria mimi nadhani walikuwa wanakariri vifungu tu. Hawaielewi sheria ila wameikariri. Hawana uwezo wa kuitafakari sheria ili iwaongoze wao. Wao wanaaamini ukishakariri vifungu vya sheria basi unakuwa umeshapata sifa za kuwa Rais wa taifa hili. Wao ndivyo wanavyoamini.

Wangelikua wanailewa sheria wangeitumia sheria maishani mwao na kuifuata hivyo tungewaona ni viongozi wenye hekima.

Lakini dalili zao zilionyesha tangu mwanzo kwamba ni viongozi wanaopenda mabishano ya sheria walioikariri tena wala hawaifuati wala kuielewa kama mafilisayo. Wanabishana kwa kutumia vifungu vya sheria ili kutuonyesha walivyo kariri vifungu vya sheria bila kuvielewa. Yote ni kwasababu wao ni kama mafalisayo walio wakiriri vifungu vya biblia lakini hawavifuati ili viwaongoze. Wanataja vifungu vya sheria kusudi waogopwe na wajinga wasiojua nini maana ya sheria.

Ni wajinga tu wanao wafuata watu hao ili wawasikilize wakati wanataja vifungu vya sheria walivyo kariri. Bali werevu wa sheria hukaa kimya na kuifuata sheria wala hawaishabikii.

Wamekariri sheria ili wabishane na viongozi na taasisi za serikali. Ni mafalisayo tu, ni sawa na wale walimu wa sheria wa kwenye biblia walio kariri vifungu ili waonekani wanajua vifungu vya biblia lakini wala hawijui sheria walio ikariri wala hawaifuati na kuishemu.

Wanataka kujidai kwamba ndio watu wa maana sana katika taifa letu kumbe ni kwasababu akili zao zimepumbazwa na mabeberu hivyo hawajielewi kwasababu ni watumwa wa mawazo ya kuamini misaada ya kusaidiwa na mabeberu kuliko wao wenyewe kujisaidia.

Wala hawawajui mabeberu wala nia ya mabeberu ila wanawaamini mabeberu.

Ni viongozi gani wakariri vifungu vya sheria wasivyo vielewa? wanavunja sheria za Taifa letu huku vifungu wamevikariri?

Sisi wananchi wa taifa hili hatuwahitaji kwani hawawezi kuwa viongozi wa taifa letu huru. Kwasababu wana shirikiana na mabeberu hawana chochote cha kulifanyia taifa letu zaidi ya kwenda kuwalipa mabeberu wao rasilimali zetu kama fidia.

Sisi wananchi wa Taifa letu huru tunaungana na Rais wetu ili kutengeneza mazingira mazuri ya kiuchumi kwaajili ya vizazi vyetu vya baadaye.

We would like to see our sons, our daughters, grandsons and granddaughters shine in our blessed Tanzania Land.

What we know progress never move in a straight path, sometimes there're ups and downs.

But having a better policy in industriazation and better education and more imphasising math, science and innovation would make our national reach the ecomic goal.

Let's join our President Dkt John Magufuli. Together we are going to make our nation great in the world.

Ni mimi Meneja wa Makampuni
a. k. a Mr. Newton wa Tz.

Sent from HUAWEI MATE40 PRO.
 
Wewe hujielewi kabisa na unayoongea ni upumbavu wa kiwango cha lami,ccm ndo inaleta double standard kwenye sheria,sheria wanaitumia kwa ajili ya wapinzani halafu kwa CCM ni sawa,we ni popoma tu kama hujui nani anajua tafsiri za sheria kati Tundu Lissu na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
 
Mtoa mada leo umeniharibia siku kabisaa maana nilipoona heading ya uzi wako nilikuja mbio sana nikijua nakuja kuongeza vitu kichwani. Daaah nilichokutana nacho aisee yaani maandishi yoote hayo hakuna hata kilichoelezwa hata kimoja ajabu sana? Daaah hivi umeshawahi kuiona tu wachilia mbali kuisoma sheria yeyote hapa duniani? Sasa ushujaa huu wa kuandika maelezo mareefu ukidhani unaongelea taaluma kumbe bila kujua unawakilisha hisia unautoa wapi?
 
Hivi JF kwanini wasiweze kuzuia mipopoma kama hili kuweka uzi humu! Jitu halijasoma shule linatamani kushindana na wasomi.
 
Nimepoteza muda wangu kusoma pumba. swali vp wanaokariri kilomita za barabara?
 
Cc Meneja wa makampuni
Mosi unasaka uteuzi kwa mtu ambaye naye anasaka kurejea ofisini! Nathibitisha Hilo kwa namba zako za chombo Cha mawasiliano unachokitumia yaani simu!
Pili, hii ni rushwa Kama zilivyo rushwa nyingine yaani unampigia na kukipigia ccm kampeni kwa kuwashambulia wanachama wa vyama vingine ili nawe urejeshewe fadhila kwa kupewa uteuzi! It's unfair!
Hili shambulio lako ni la kifedhuli na kipumbavu kwani ni sawa na kusifia taaluma yako ya kutumia grill wakati wa kuchimbia mafuta na gas na kuudharau udaktari!
Nakushauri urudi tu China ukaombe kibarua Cha kuchimba makaa ya mawe kwani siasa za bongo pasua kichwa!
 
Hili ni taifa letu sote, mimi na wewe hatuwezi kuona watu wachache eti wanajidai wao ndio wanaelewa sana kuzidi hata viongozi wanao tuongoza eti wanajifanya wanaelewa sana kuliko sheria na kanuni tulizo jiwekea.

Tena, musiombe nifanikiwe kuingia kwenye bunge la Mwaka huu, tunataka tuhakikishe hili taifa linasonga mbele, wale wanao jidai kwamba wanaijua sana sheria mpaka kufikia kudharau kanuni zetu mimi nakuja kuwaonyesha kazi ya degree yangu ya Theology.
 
Hakika unajisumbua mno na sababu ni uelewa wako mdogo juu ya Mambo ya kidunia! Bunge sio madhabahu mjomba na mbunge siyo kasisi! Baki kwenye madhabahu Ile vya huko!
Itoshe tu kukukumbusha kuwa, mvunja katiba na taratibu pamoja na kuvuruga umoja wa kitaifa unaye huko ccm! Pambana naye kwanza kabla ya kuhangaika na wanasheria wanaojitambua na kujielewa!
 
Wewe ndiye unaulewa mdogo.
Ushabiki wa siasa umekupumbaza ili usielewe.
 
Wewe ndiye unaulewa mdogo ushabiki wa siasa umekupumbaza ili usielewe.
Wewe ni shabiki wa Nini? Hujitambui bado! Au imepotea jukwaa la kuandika hizi limbs zako? Hilo ni jukwaa la siasa na wewe umelitumia, hivyo nawe ni shabiki wa siasa uliyevamia siasa kiduanzi? Hao waumini uliokwenda kuwasomea theolojia watakupiga mawe madhabahuni usipoangalia approach zako vyema! Achana na siasa huzijui na huziwezi pia[
 
Nimekuja kuwafungua akili waliopumbazwa ili waache siasa za kishabiki
 
Back
Top Bottom