duh..
huwa sichanganyikiwi kirahisi lakini leo mmefanikiwa kunichanganya;
Nini kimekuchanganya Mzee?
mwenyewe nimedandia treni kwa mbele nadhhani tunazungumzia zile kazi ambazo wanakijiji tunasifika kuzifanya yaani kulima udongo na kupanda mazao. Kwamba wanawake wanafanya kazi hizi sana ni ukweli wa muda mrefu, wanaume nao wanafanya kazi lakini in relation to overall work ya mwanammke ni wazi kuwa mwanammke anajikuta anafanya zaidi kwani.
.
Huoni mgawanyo wa kazi usio wa kuridhisha hupelekea Kilimo kwanza kutokufanikiwa?
Anajikalisha na chakula kinaletwa, anakula kama ana wazimu. Mama anakuja kutoa vyombo kwenda kussafisha.. Wanaenda chumbani mzee anataka "kula kile chakula kingine". Mama pamoja na kuchoka inabidi akubali kumpa mtu chakula kile roho inatamani. Kesho yake mzunguko mwingine unaanza labda ukiwa na mabadiliko machache.
Kwanini mama anamlisha mara mbilimbili?? Baba haoni mama kachoka?
Mara kuna kikao cha "kilimo kwanza" baba peke yake anaenda kutoa maoni! Of course mama yuko nyumbani "anaanglaia watoto"
.
Kwani kabla ya kwenda kikao cha kilimo kwanza, huyu baba asingeweza kufanya kikao kidogo na mkewe kwanza kujua hali halisi? Huoni ingeepusha kuonekana wa ajabu kujadili kitu ambacho mchango wake ni haba? Pengine mama angempa mawazo mazuri ya kuwasilisha kunako husika.