Wanamchafua Mwendazake wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wao watabaki salama

Wanamchafua Mwendazake wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wao watabaki salama

Huu ni mwendelezo wa projo za MATAGA.Mwendazake hakuna aliyemchafua zaidi ya kujichafua yeye mwenyewe kwa maisha ya kupenda sifa,kukurupuka,kujiona bora kuliko wengine,visasi vilivyopitiliza,upigaji wa kufa mtu/ufisadi.Kuwa na roho mbaya huku akijificha kwenye koti la ucha Mungu.Jiwe alijiharibia mwenyewe kwa design ya maisha aliyoishi.Ili uwe salama mbele ya Watz leo, ni heri kumkana Jiwe na Matendo yake!
 
Wanasiasa wa Tz vichwa panzi sana. Uko kwenye utawala usiokubaliana nao badala uwajibike angalau kwa kushauri inaposhindikana ujiuzulu unakomaa humo humo as long as mkono unaenda kinywani. Leo kiongozi kaondoka unaanza kumchafua wakati ulikuwa sehem ya uongozi wake na hukuwahi kuwajibika hata siku moja! Tunakuamini vp leo?
 
Na hiyo sura ilivyo ikiwekwa kwenye pesa yetu si ni uchuro tuh,

Kwanza hiyo sura Mimi Mara nyingi huwa naichukua namtishia nayo mwanangu akigoma kunywa ujiii...!!

Hebu tuache kwanza tujenge nchi,sukuma gang wataisoma namb

😂😂😂😂😂😂😂
 
Huu ni mwendelezo wa projo za MATAGA.Mwendazake hakuna aliyemchafua zaidi ya kujichafua yeye mwenyewe kwa maisha ya kupenda sifa,kukurupuka,kujiona bora kuliko wengine,visasi vilivyopitiliza,upigaji wa kufa mtu/ufisadi.Kuwa na roho mbaya huku akijificha kwenye koti la ucha Mungu.Jiwe alijiharibia mwenyewe kwa design ya maisha aliyoishi.Ili uwe salama mbele ya Watz leo, ni heri kumkana Jiwe na Matendo yake!

CAG profesa Assad alimwambia imeibiwa 1.5 Trillion kamuundia zengwe akamtoa,

Akamleta CAG wake alieona yeye anafaa,ndiyo kaja kumvua nguo kabisa,sasa wewe unasemaje anachafuliwa??

Meko miyeyusho tuuuh,alikuwa mpigaji tuh yuleee
 
Tangu lini kusema ukweli ikawa ni kumchafua mtu?

AJabu Sana,wao walikuwa brainwashed kuwa Magufuli alikuwa malaika na hakuna makosa amefanya,kumbe alikuwa mpigaji tuuuh na yeye,mshamba kweli tan,ukithubutu kuongea tuh anakupoteza,kiko wapi leo
 
Wana mchafua kwa lipi?
Hij ripoti ya CAG iliandikwa jamaa Jiwe akiwa hai.
Inaonyesha zilikuwa zina andaliwa ripoti mbili. Na ikawa ina somwa hiyo kanjanja.
Au iliandaliwa na Chadema?
 
Watu wanamchafua bure shirika letu la ndege linapata sana faida.
 
Kwema wanachemba.

Tumeshuhudia tangu kuondoka kwa mwendazake kumekuwa na sauti nyingi sana zikipazwa kwa nguvu sana tena na wengine waliokuwa wasaidizi wake wa karibu sana kujaribu kutuaminisha kuwa mwendazake alikuwa mtu hovyo sana !!!! Wanachosahau ni kuwa na wao walikuwa watu muhimu sana tena viongozi wa mihimili muhimu katika katiba yetu na hawakutimiza wajibu wao ipasavyo kuzuia yasifanyike yaliyofanyika.

SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wetu wa sasa, alikuwa msaidizi namba moja wa Mwendazake, kama mahakamani ni mtuhumiwa namba 2 kwenye kesi, anawajibika kwa haya yaliyotokea. Kutudanganya kuwa hakuwa na uwezo wa kuzuia yasitokee ni uzandiki. Kama alijaribu kuzuia na akashindwa kuchukua hatua gani? Kuendelea kubaki madarakani ilikuwa ni alama kuwa alikubaliana au anaunga mkono yaliyokuwa yanafanyika.

JOB NDUGAI ni kiongozi wa bunge, muhimili muhimu kwenye katiba yetu,ambalo una jukumu la kuisimamia serikali. Aliwajibika vipi kama kiongozi na bungekuisimamia serikali ili kuyamulika haya yaliyotokea ? Au wakati ule aliyaona ni sawa na sasa Kuna wingu limeondoka machoni anaona hayakuwa sawa? Wabunge waliokuwepo walitimiza vipi wajibu wao katika kuyazuia haya wanayotuaminisha sasa kuwa yaliyokuwa ili yasitendeke as kwa mtazamo wao wa sasaR hayakustahili kutokea coz ni ufisadi?

Wako wengi wa kuwataja lakini naamini tunawatambua, waje sasa hadharani watuambie ni kwa nini walishiriki wizi ule au kwa nini hawakuchukua hatua kuzuia?

Kinachosikitisha ni kwamba hata ambao wangetakiwa kutumia fursa hii kujiimarisha nao wameingia kwenye praise and worship team kushangilia huyu aliyepokea kijiti wakiongozwa zaidi na chuki zao za dhahiri kwa mwendazake na kusahau jukumu lao la msingi. Yaani muda huu wangekuwa wamekomaa na hoja kuwa kama ufisadi Huu ULIFANYIKA wakati hawa waliobaki akiwemo rais aliyepo madarakani wakiwa ndio wasaidizi wakuu wa Mwendazake na wakaruhusu haya yatokee basi na wao awajibike ingekuwaje?

Unakwenda kwa wananchi kuwaambia kuwa kama haya yaliyokuwa na CCM kama taasisi wakashindwa kuyazuia basi ni tatizo la taasisi na sio mtu, kwamba tuna uhakika gani kuwa hayatatokea kama haya kwa mwingine ikiwa ni kweli kwamba mtu anaweza kuizidi nguvu hiyo taasisi?

Wakaeleza na mengine mengi kwa kadri wawezavyo kuvutia upande wao, Wasingefanikiwa? Lakini kwa sababu wameruhusu chuki zao dhidi ya JPM ziwatawale na wao wamejiunga kwenye praise and worship team!

Hawa Ndio wanasiasa wetu, ambao kwao maisha yao na chuki zao ni muhimu kuliko TANZANIA.
Wote hao na wengine wana mambo ya kujibu, time will tell, ila asifiwe Mungu Mkuu kwa kutuondolea dhahama.
 
Back
Top Bottom